Tetesi: Tanzania Daima Hali Siyo Shwari, Mhariri Mkuu, Ndugu Neville Meena Atimuliwa Kazi

Tetesi: Tanzania Daima Hali Siyo Shwari, Mhariri Mkuu, Ndugu Neville Meena Atimuliwa Kazi

Inachekesha sababu lazima alijua wanalipwaje, ila sababu ya Mh. JPM hakuna njia ingine ya kupata vya mikato mikato.

Namba inasomwa na wengi kumbe
 
Kwani wewe ni mmoja kati ya 14?punguza hasira.
Punguza mizaha.Horrible people hamna nyuma wala mbele kama zile kaptura za miaka ile.Unaweza jaza trashes hapa kisha ukishamaliza unakimbia bila kuaga.huko ni kukosa adabu.
 
Tusiusmee moyo, yote yanawezekana. Nani alijua anaweza kuuza chama kwa FISADI? Nani alijua kuwa hakuwa analipa kodi kwa takribani miaka 20?
Mahakama ya mafisadi imekosa kesi Sasa nashangaa unaposema Mh. MBOWE ameuza Chama kwa fisadi. Hilo Swala la kodi ni hila za kisiasa kutaka kumdhoofisha MBOWE
 
CCM wakongwe, wao tatizo lao walilikabili kikongwe , huko kwa watani wao sijui!
Hapana CCM wameuzia selikali shule chakavu kimiundombinu na kielimu sekondari Omumwani huko Bukoba kwa mabilioni,CDM hayuko serikalini atauza nini?
 
Awamu hii
Mlikuwa mnamuogopa Mbowe kuliko mungu
Mtamkimbia tu
Mtu mgeni akija nchi hii anaweza kudhani Mbowe au Lowassa ndio viongozi wa nchi hii na Magu ndio kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kama atakuwa anafuatilia trend ya hoja zenu.
 
Hapana CCM wameuzia selikali shule chakavu kimiundombinu na kielimu sekondari Omumwani huko Bukoba kwa mabilioni,CDM hayuko serikalini atauza nini?
Si aliuza chama kwa billion kumi mwaka jana
 
Mbowe wa ajabu sana anakwepa kodi halafu halipi mishahara watumishi wake DU!

Punguza 'upenzi'. It ruins your reasoning capacity. Nyinyi ndio mnao turudisha nyuma na chama chenu cha Mafisadi.
 
Gazeti litaendeshwaje na watu 14??
Wanatosha sana.

Kwanza siungi mkono timua timua yoyote kwa sababu zozote zile lakini ni ukweli uliowazi awamu hii ya 5 sijui imekuja na nini, hivyo biashara zinapukutika, mauzo yanashuka, media nyingi zinashindwa kulipa mishahara, naifahamu TV moja kubwa ina staff 400, imetangaza retrenchment itapunguza staff 200 na kubaki na 200!.

Mimi mwenyewe Studio yangu ya PPR ilikuwa na Staff 15 nikipanga jengo zima la NHC pale Mkwepu lenye 8 rooms huku nikilipa kodi ya TZS 3.M kwa mwezi, sasa nimeshindwa, jengo nimeachia na kuhamia Posta House nimepunguza 10 people tumebaki watu 5 tuu! .

Tunatumia ICT na kufanya multiple tasks
1. Mimi Boss ndio mkurugenzi, maneja na paymasters malipo yote kwa Mpesa
2.Chief Camera ndio mtu wa light ndio mtu wa sound
3.Chief editor ndio editor ndio mtu was graphic.
4.Office manager ndio receptionist ndio secretary
5.Dereva ndio mtu wa logistics, ndio mesenja.

Hivyo hata hilo Gazeti kama hali ni ngumu watu 14 wanaendesha gazeti.
1. Chief Editor
2. Sub Editor
3. Business Editor
4. Sport Editor
5. Feature Editor
6. Chief Photographer
7. Staff Photographer
8. Chief Reporter
9. Staff Reporter
10. Sports Reporter
11. Page Maker
12. Graphic Editor
13. Marketing Manager
14. Circulation Manager

Kazi nyingine zote zitafanywa online na freelancers kuanzia reporters, photographers hadi freelance sales.

Kiukweli Magufuli ametuweza.

Paskali
 
View attachment 454642

Kuna taarifa kuwa jana tarehe 04 Januari, 2017 Katika ofisi za gazeti la Tanzania Daima kulikuwa na patashika Nguo kuchanika. Kwa mujibu wa mdakuzi wa taarifa hii, chanzo cha patashika hiyo ilitokana na UKATA unaoukabila uongozi wa gazeti hilo, hali iliyopelekea Watumishi kutolipwa mishahara yao yapata miezi MITANO sasa. Habari zaidi zinasema mhariri Mkuu wa Tanzania Daima, Ndugu NEVILLE MEENA ametimuliwa kazi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuingiza wafanyakazi wengi wasiyo kuwa na tija kwa gazeti huku wakilipwa mishahara mikubwa.

Wakati huo huo Mmiliki wa gazeti la Tanzania Daima ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), FREEMAN AIKAELI MBOWE ametoa maagizo ya kuwatimua wafanyakazi wangine na kuwabakiza kumi na nne(14) tu.
Nao wanaisoma namba.
 
Back
Top Bottom