Tetesi: Tanzania Daima Hali Siyo Shwari, Mhariri Mkuu, Ndugu Neville Meena Atimuliwa Kazi

Uko sawa kabisa..mbn agency nyingi za matangazo wako wachache na wanafanya kazi kubwa...ingawa kweli timua timua sio nzuri
 
Mkuu asante kwa mchanganuo.
 
Huu ndiyo umbea na ushankupe! Taarifa hizo uwe nazo wewe tu hata wadau walio kazini wasiijue?
 
Itabidi amuulizie kinara wa kununua magazeti yaliopepesuka,Rostam
 
narudia tens wandugu tushiriki kujadili mambo ya msingi yatakayotukwamua toka hapa tulipo,,tuachane na minor issues kama hizi
Lingekuwa gazeti la uhuru mngebanana humu. Posts hata 5000 zingefika ndani ya masaa mawili. Wapiga deal watajulikana tu awamu hii
 
...dah,aisee pole sana mkuu;kweli Mayalla ni Njaa!..itabidi ujiite Shibe sasa!
...ila sijaelewa,kama mambo yanaenda kwa idadi ndogo ya watu Magufuli kawawezaje sasa;au mnalipualipua bora liende?
 
..labda wasomaji wengi wa gezeti hilo walikuwa wapiga dili.

..sasa kwasababu Magufuli amewabana wapiga dili basi mauzo ya gazeti nayo yamedorora.

magazeti yaliyokuwa yanaendeshwa kichama chama lazima yaanguke chama kikipanda nalo linapanda kikishuka nalo linashuka na hili nilishaawahi kumuonya mbowe gazeti lijitegemee na sio kila siku kukesha kukisifia chama hata kama kuna madudu
 
magazeti yaliyokuwa yanaendeshwa kichama chama lazima yaanguke chama kikipanda nalo linapanda kikishuka nalo linashuka na hili nilishaawahi kumuonya mbowe gazeti lijitegemee na sio kila siku kukesha kukisifia chama hata kama kuna madudu

..true.

..lakini pia biashara nyingi zimeyumba kwa hiyo hata hili gazeti nalo lazima mauzo yake yashuke na wamiliki wajipange upya.

..ila usitegemee wataajiri zaidi hata kama mauzo yataongezeka.

..Kitakachotokea ni kwamba watajenga utamaduni wa kufanya kazi na watu wachache.

..that is my prediction kwa biashara zote ambazo zinapunguza wafanyakazi sasa hivi.
 
...dah,aisee pole sana mkuu;kweli Mayalla ni Njaa!..itabidi ujiite Shibe sasa!
...ila sijaelewa,kama mambo yanaenda kwa idadi ndogo ya watu Magufuli kawawezaje sasa;au mnalipualipua bora liende?
Standard ya Professionalism kwenye production inataka kila mtu a play role moja tuu ila kutokana na ukata, kazi hakuna!, hivyo media nyingi zita cut staff isipokuwa TBC na Clouds tuu!, kazi zikizidi, unakodisha watu,
1.Producer
2.Director
3. Camera 1
4. Camera 2
5. Camera 3
6. Sound
7. Light
8. Editor
9. Presenter
10. Grip
11. CCU
12. Costume/make up
13. Set up/location
14. Logistic
15. Production manager

Kutokana na ukata tumebaki wanne tuu na mmoja ofisini!.
1. Producer ndio una tafuta location, una fanya set up, unadirect, una present, una produce unatafuta na una manage.
2. Cameraman 1 ana set camera zote, sound, light kisha anakaa kwenye main camera na kuzicontrol kwa remote
3. Editor ndio huyo huyo atakaa kwenye CCU na ndie ata fanya graphics
4. Mtu wa logistic ndio huyo huyo anakuwa grip man na handy man.
hakuna mambo ya makeup wala costumes hivyo timu ya watu 4 mnamaliza kazi, ila kwenye live lazima wote wawepo.
Paskali
 
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida Mh. Mbowe amekiri kuwa na hali mbaya ya kifedha katika kuendesha kampuni yake.

Kutokana na hali hiyo amelazimika kupunguza wafanyakazi na kupunguza mishahara kwa wafanyakazi wake.

Hii imekuja baadaya ya kuripotiwa kuwa kumekuwa na hali ya kutoelewana katika Mbowe na Mhariri Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na Mbowe.

Mbowe akiri hali ni ngumu, apunguza mishahara na idadi ya wafanyakazi katika kampuni yake - SWAHILI TIMES

Naona sasa kila mtu anajifunza kubana matumizi.
 
Sawa, kitu cha muhimu ni ajipage ili arudishe Mali zote alizokopa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…