Tanzania haijapate Mwinjilisti Mwingine mwenye nguvu kitaifa kama Moses Kulola sababu aliondoka bila kukabidhi mtu kipawa alichokuwa nacho

Hiyo ni biashara mzee tena serikali ilitakiwa ikusanye Kodi yake pale
 
Humjui BULUDOZA wewe?



Hivi Kwanini ajiita hilo jina ?

Lilianzaje?

Mimi naona kama ni kujikweza, Mbona Mitume wale wa kanisa la kwanza hawakuwa na hizo mambo ya majisifu?

Sema wanyakyusa bana ! Namfikiria Lusekelo naye huwa anapenda kujisifu yeye anajiitaga katapila sijui nani vile?!

Natamani angekuwa humbled ingependeza zaidi na Utukufu wote atazidi kupewa Bwana!
 
Kifupi Kwa uinjilisti ni kidogo mno tu kufikia viwango vya akina Moses Kulola,Billy Graham au Renhard Bonke vya kujikita tu kwenye injili ya kuleta wokovu tu watu watubu dhambi na kuacha
Watu wazito sana hawa umewataja mkuu, japo mimi si mtu wa dini lakini nawaheshimu sana hawa watu, enzi hizo wazazi wangu walipata wokovu kwenye mkutano wa Reinhard Bonke.(nilikuwa mdogo, wazazi ndo waliniambia) ile injili ilibadilisha sana maisha yao.

Kipindi nakua naikumbuka sana mikutano ya Moses Kulola tukiwa na familia hakika alikuwa na wito wa kweli kwa Mungu.
 
Uzi una makandokando, anayeongelewa ni Muinjilisti na sio mchungaji Wala muombezi
 
Hiyo sio kazi ya Kulola. Kama Kulola alipewa na mtoaji basi mtoaji huyo huyo ndiye mwenye huo wajibu wa kujua jinsi ya kuvuna mavuno yake.
 
Alipigwa na askari ambae SAwa na mwanae ndio ikawa chanzo cha kifo chake. Alifungwa sababu ya injili.
Elezea kwa kina ndugu,sababu ya kupigwa ni ipi na ilikuaje mpaka akafungwa
 
Matunda ya idadi ya wanaookoka mikutano yake

Biblia inatamka wazi mtawatambua kwa matunda yao

Mwinjilisti hapimwi kwa jina kujiita Mwinjilisti Moses aliketa maefu kwa kanisa kupitia huduma yake

Uinjilisti sio cheo ni kazi
Ulipima vipi kuwa waliookoka Ni kweli wameokoka kwa Kristo?
Au kwa macho ya Rohoni!
[emoji1787][emoji1787]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Atoe Bure, gharama za uandaaji wa maji Ni sadaka za waumini?
Kwani sadaka anazopewa anataka anunue magari mangapi?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Lusekelo ni Mnyakyusa au Mkinga?
 
Huyo Moses Kulola kuja kumshinda Diana Bundala kwenye uinjilist May be aende direct mbingun kusoma gospel ndo aje ashindane. Yule mama ni shindikanaa coz yeye mbingun anaendaga daily
Diana Bundala anafanya uinjilisti gani?. Maana hamuamini Yesu.
 
Uinjilist ndio kufanya kitu gani?? na uchungaji ni kitu gani??
Uinjilsiti ni kupeleka habari njema kwa wasioamini au waliopo dhambini, wakati mchungaji ni kuchunga wale walioamini wasirudi nyuma dhambini
 
Nadhani mwinjilisti wa kwanza wa kilokole aliitwa Harris Kapiga miaka 1928, wakaja akina Andrea shimba, baadae miaka ya 1960 ndio wakaja wainjilisti Moses Kulola, Lazaro na Kiwia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…