Tanzania hatujawahi kuwa na Marais au Mawaziri ambao kabla ya madaraka waliwahi kuendesha mradi wowote na wakafanikiwa

hujawahi kuanzisha kitu chochote kikafanikiwa, unawezaje kuongoza nchi kwenye mafanikio? tusidanganyane
 
Mleta kataja uraisi, ubunge na uwaziri.
Wengine Amir Jamal na Alnur Kassim
 
Unajua maana ya uongozi. Kama wananchi wana changamoto ni juu yako kuwaongoza. Unajua ninyi mmelemazwa na huu uongozi wa CCM ambao rais na viongozi wanakuwa pale kwa manufaa yao. Huijui dunia wewe ndiyo maana. Kiongozi mzuri ni yule anayejua udhaifu wa anaowaongoza na kuurekebisha. Ni nini sasa maana ya uongozi kama hujui kinachowasibu watu wako na kurekebisha?
 
Siyo lazima kuanzisha. Urais unahitaji mtendaji mzuri mwenye maono. Tusidanganyane.
Mwenye maono atajulikana vipi? Au ni kumchomeka kwenye uongozi kwanza halafu ndiyo tujue kama ana maono au hana? Na wakati huo tunakuwa hatuna tena uwezo wa kumgusa,tutamjuaje before?
 
Mkuu kwani katiba inaweza kutumika na viongozi waliolelewa na mfumo wa kuteuliwa tu, na haiwezi tumika kwa hao waliofanikiwa private sector?
Marais wazuri wengi huwa ni wale walitokea private sector na hawakuwa na ukiritimba, team za maswahiba wakuwalipa vyeo, njaa njaa na kutozoea luxury, wamezoea delegation of power uko kwenye makampuni yao, wamezoea kufanya mambo kwa malengo na kujipima mafanikio au hasara, sio washamba. Mtu aliyedumu serikalini miaka 30 hawezi kuleta mageuzi akiwa Rais, kayajulia wapi?

Nikupe mfano mwingine, jeshi la Marekani mara nyingi halichagui kamanda ambaye alifukuza mke, alitelekeza mtoto, alimpiga mke, alitishia kuua, aliwahi kulewa akaendesha gari. Unajua kwanini?

Kama kulea familia ya watu wanne unaowalisha mwenyewe tu huwezi, vipi tukikupa command ya brigade nzima yenye silaha kali na wanajeshi wakorofi ambao umewakuta?

Kama ulilewa ukaendesha gari na ni kinyume cha sheria, that means unaweza kuwa na abuse of power tukikupa.

Kama ulikuwa unapiga mke, maana yake una temper sasa ukiongoza ndegevita zenye mabomu ya nyuklia itakuwaje?

Ndio maana Marekani ina Rais mmoja tu aliyekuwa bachelor, na ni mojawapo ya Marais wao wa hovyo kuwahi kutokea, na ndiye alisababisha American civil war. Baada ya hapo huwezi kuwa eti unaogopa kuoa (kuongoza mtu mmoja) alafu unataka tukupe nchi ngumu USA uongoze.

Katika mambo madogo mengi na experience ya mtu tunaweza jua tabia yake itatufaa kiasi gani. Bila hivyo tunajikuta na Rais ambaye ni rahisi kumtuhumu alipiga mtu risasi akiwa ikulu.
 
sawa kabisa
 
Mwenye maono atajulikana vipi? Au ni kumchomeka kwenye uongozi kwanza halafu ndiyo tujue kama ana maono au hana? Na wakati huo tunakuwa hatuna tena uwezo wa kumgusa,tutamjuaje before?
ni hatari sana kupima maono ya mtu akiwa madarakani. wakati hajawahi kutuonesha kwa vitendo namna ya kufanikisha jambo.
 
asante mkuu kwa elimu kedekede
 
Rais Gerald Ford ni watu wawili tofauti na bilionea Henry Ford. Rais Ford hakuwa bilionea wala mfanyabiashara bali career politician.
 
Sahihi, tatizo ni katiba zaidi.
 
Na matatizo makubwa ya taifa yanatokana na hilo.

Watu wenye kufanya maamuzi makubwa ya taifa hawana uzoefu wowote katika sekta wanazozitolea maamuz
 
Huu ni mtazamo potofu sana, kuongoza nchi ni tofauti sana na kuendesha kampuni.
Bill Clinton ambaye ni career politician, mojawapo wa marais bora kabisa wa Marekani aliicha US na ziada ya bajeti(surplus), Bush Mfanyabiashara aliyerithi uchumi imara kutoka kwa Clinton aliiacha Marekani na deni kubwa, vita visivyoisha(endless wars) pamoja na matatizo makubwa ya uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…