Tanzania imekumbwa na ugonjwa mpya unaitwa matatizo ya kupumua

Tanzania imekumbwa na ugonjwa mpya unaitwa matatizo ya kupumua

Mtapenda

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2011
Posts
1,114
Reaction score
2,070
Habari zenu wanaJF,

Ni wiki sasa Tanzania tunatangaziwa watu maarufu wanafariki kwa matatizo ya kupumua tena ni wengi mno sasa ni wakati wa serikali kututangazia haya matatizo ya kupumua yanasababishwa na nini!?, Dalili zake pamoja na tahadhari ya kuchukua..

Ni dhahiri kwamba mh rais kama alivyosema hatujawahi shindwa vita yoyote sasahivi vita ya Corona imeisha imebaki vita mpya ya matatizo ya kupumua.

Ni wakati wa kuambiwa ukweli haya matatizo ya kupumua ni yepi maana now days hatupewi taarifa za wagonjwa wa Corona, waliofariki na waliopona tangu hotuba ya mh raisi isemwe akiwa Chato.

Sahivi taarifa za ugonjwa wa Corona tunazipata kutokea uganda kwa madereva wetu wa maroli..

Mficha maradhi kifo humuumbua na pia kama tatizo la kupumua ndio Corona kwanini isisemwe tuu ili tatizo lijulikane kama zito ata kupata misaada kwa mataifa mengine.

Ukweli lazima usemwe hali ya Corona nchini ipoje maana kuna watu wanadhani janga hili limeisha kumbe ndio limepamba moto...

Ni hayo tu huu ugonjwa wa matatizo ya kupumua ndio Corona mpya ama mbadala wa neno Corona.
 
Hapa ndipo waafrika tunapoonekana na kuitwa washenzi.


Hawa sijui ni vibaraka wa ccm wametumwa! Kule Tanga, Mafia, mtwara, dar ndio usiseme watu wanakufa na wengine wanakutwa kariakoo wamedondoka na kisha maiti hutelekezwa bila msaada wowote....very sad aise!
 
Back
Top Bottom