Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na Kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza bandari ya Dar es Salaam
Game changer anatakiwa haraka kubadili upepo! Ili tutoke kwenye mambo ya bandari.
 
Habari!
Sheria za nchi zipo
Katiba ipo
Mahakama ipo
Mabaraza ya watumishi yapo
PCCB ipo
Police ipo
Tume zipo
Kama hivi vyote vipo na serikali imeshindwa kuvitumia kudhibiti uvujaji wa mapato TPA je, ni chombo gani kitaweza kupambana na Mwekezaji asituibie?
Kama tatizo ni watumishi wa BANDARI kwanini serikali iseme ajira zao ziko salama?
DP World anahitaji watumishi wezi?
Watakaokuwa na maisha marefu wataona mengi
 
Mama ajiuzulu kulinda heshima kiduchu aliyobaki nayo

6B358783-1445-4036-AE31-C678F8C37139.jpeg
 
Wafanyakazi wa bandari wengi wao watoto wa CCM mtoto wa muheshimiwa flani.

Kumuondoa kwenye kula yake inakuwa ngumu sana, kuna kundi dogo linafaidi keki ya nchi.
 
Badala ya kukiri kushindwa kuendesha na kusimamia bandari,

Ilitakiwa warudi Kwa wananchi, tu ngechagua chama na Serikali ya chama kingine chenye uwezo wa kusimamia bandari, kudhibiti wizi na kuongeza ufanisi.

Ni Tanzania pekee haya yanatokea.

Mmekiri kushindwa, MTUPISHE 🙏🙏
 
🤣🤣🤣Kawajibu Arusha leo,yeye ni kazi,maneno hana time nayo, yani anasema ye ni mtu wa action 🤣🤣🤣
Wananchi ndo bosses wa viongozi,

Jeuri ya mtumishi kumjibu hivyo boss wanatoa wapi?
 
Mkataba tushamaliza kuusaini na kuupitisha kwa kishindo ni wakati sasa wa kuanza utekelezaji mara moja bila kuchelewa. Pongezi sana kwa Rais Samia kwa kuona mbali sana, hii fursa tulikuwa tunaisubiri kwa mda mrefu sana. Ndugu watanzania tuendelee kumuunga mkono Rais katika juhudi za kuikomboa Tanzania.

Uzi tayari
Screenshot_20230629_232817_Google.jpg
 
🔥🔥🔥 Tz itakua kama Dubai...
Ila nawaonea huruma wanaume wa Dar na hivi hampendi kufanya kazi, Waarabu watafanya kweli show show...
 
Mkataba tushamaliza kuusaini na kuupitisha kwa kishindo ni wakati sasa wa kuanza utekelezaji mara moja bila kuchelewa. Pongezi sana kwa Rais Samia kwa kuona mbali sana, hii fursa tulikuwa tunaisubiri kwa mda mrefu sana. Ndugu watanzania tuendelee kumuunga mkono Rais katika juhudi za kuikomboa Tanzania.

Uzi tayariView attachment 2673657
Chawa mpya kaja naye !
 
Kutegemea watu wa nje waje wakujengee nchi yako kwa mikataba mibovu ni ukichaa wa hali ya juu.
 
Huu ni mwendelezo ule ule:

Wananchi walio wengi hawautaki mkataba huu.

Kwani serikali nyie mnamwakilisha nani?
 
Back
Top Bottom