Umepoteza muda kuja na huu uzi. Taratibu za kutengeneza mikataba ya kibiashara zinaendelea.

Kama nyinyi mnaona haya mauzauza yanayoendelea pale TPA yanawafaa, tambueni kuwa tunapoteza wateja kwa maelfu wa nchi jirani kwa uendeshaji wa kimagumashi unaofuga wezi kila kukicha.

Wafanya biashara halisi wanataka hata kesho mwekezaji aanze kazi, kule Mtwara wanamtaka mwekezaji ili wauze korosho zao vizuri.

Nyinyi mnaoshinda humu JF mkipiga fitina na majungu, hamna faida yoyote kwa watu wenye kutaka kweli kufaidika na ufanisi wa uendeshaji bandari kisasa.
 
Nyuma ya hili Sakata la Bandari Kuna mengi sana ya kujifunza na kuyatazama ukiangalia tu licha ya huo unaosemwa kuwa ni mkataba kuwa na changamoto nyingi lakini pia imekuwa Kama EXIT DOOR ya mambo ya kisiasa kumbuka kabla ya yote hayo hakukuwa na mikutano Wala Uhuru huo wa watu kujieleza kwahiyo baada ya Rais aliyepo Sasa kuruhusu mikutano na maridhiano

Wapinzani ndo haya yote yanaonekana kwahiyo sikatai changamoto za Bandari lakini hili limechagizwa Sana na watu kunyimwa haki ya kuongea kwa miaka kadhaa hasa kipindi Cha Magu kwahiyo makoo yanawasha ndio maana baada ya kutokea hili kila mtu ameamua tu kuongea ili mradi muwasho utoke kooni nawasilisha
 
HIS DEATH WAS PLANNED , IN THAT HE WAS ASSASINATED
Yeah, that's what every stupid a.k.a fool a.k.a futile a.k.a dumb a.k.a dull a.k.a laughable a.k.a irrelevant a.k.a ludicrous a.k.a ill-advised person thinks.
 
Ni kweli usiopingika bandarini kuna janja janja nyingi sana ambazo zinapelekea mapato kupotea.

Kwa mfano; Nina kijana wangu ambaye alienda Zanzibar kununua Mashine kwa ajili ya kiwanda chake cha mbao. Alipofika bandari salama alikasimiwa kodi inayofikia milioni moja na elfu kumi na tano, alilipa akapewa risiti ya tshs 250,000/ na kuambiwa nenda tu hakuna mtu atakuuliza chochote.

Jamaa pesa imemtembelea ila hana kisomo wala sio mbishi jamaa akaondoka na kupita na mzigo wake. Mambo km haya yanaonyesha haja ya kuwapa watu kuboresha ukusanyaji wa mapato na utendaji.

Ila hili haliondoi haja ya kuingia mkataba wenye maslahi kwa taifa tofauti na huu ambao wajuvi wamechambua na kutuonyesha matobo yako wapi.
 
Hili ndilo CCM walipaswa walifanye na sio kusema wanaopinga hawataki uwekezaji wa DP world.
 
Sote tunajua hilo Boss. Ila mkataba uliopo mezani niwa kifisadi
 
Hapo ni utashi ndio hauko. Dunia ya leo ushuru wa forodha unaweza andika risiti iliyo na kiasi kidogo ili ubakie na chenji kubwa. Na tena bidhaa yenyewe mashine ya mbao? E-Govrn wako wapi kutengeneza mifumo?
 
Uongo mtu hakuna kitu kama hiko,bandari zetu kama ccm zimewashinda chadema watazisimamia vizuri kaa pembeni achana na bandari zetu.
 
Kivipi mkataba hauna maslahi kwa taifa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…