Sa 7 mchana
JF-Expert Member
- Dec 30, 2018
- 5,214
- 10,276
Usiamini kila unachosikia, Ilo ni dili mzee wangu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwamba alikuwa hamng'unyi maneno 🙏🏿Ukiona mpaka hawa wapambe na wapinzani wa Magufuli wameanza kuelewa somo bhs jua hali ni mbaya. Mange kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost na kuandika
“sikudhani ingekuja kutokea siku kwenye maisha yangu nikakubalina na kitu alichosema Magufuli. This is all your fault Mama Samia. Alichosema Magufuli ndio mkataba ambao wewe umeukubali sababu ya kuwasikiliza hao mafisadi waliokuzunguka.
Mtanzania yoyote anaesapoti hili dili la DP World na Tanzania ana maslahi yake binafsi la sivyo basi ana utindio wa ubongo......
Alafu na nyie watu wa Magu msianze na comments za oooh!! tulikwambia Magu this Magu that. Tayari naumia roho vya
kutosha kukubaliana nae kwenye hii issue sasa msiniongezeee maumivu...... Na msimamo wangu bado uko pale pale kuhusu Magu ila kwa hili la bandari Magu na ubipolar wake was 100% right.”
View attachment 2650058
View attachment 2650059
Najua mpo wengi mnamchukia mzee baba ila Moyoni mnamkubali mzee baba. Muda upo tutaimba pamoja hapa.
Aisee..Kubinafisha Bandari, viwanja vya ndege na vitu vinavyofanana na hivyo,
Ni kusema lolote na Liwe!
Bandari ni eneo nyeti linalobeba siri nyingi za nchi, kadhalika viwanja vya ndege
Kujaribu kuvibinafisisha, ni kuondoa pazia ili kila mwenye kuchungulia ataona kila kilichochumbani
Duh!...Taifa hili ni mali ya watu wachache wengine tupo kusindikiza tu watu wanao faida [emoji513] ya taifa.
Nisawa nakuuza nyumba nakwenda kulala kwa jilaniKubinafisha Bandari, viwanja vya ndege na vitu vinavyofanana na hivyo,
Ni kusema lolote na Liwe!
Bandari ni eneo nyeti linalobeba siri nyingi za nchi, kadhalika viwanja vya ndege
Kujaribu kuvibinafisisha, ni kuondoa pazia ili kila mwenye kuchungulia ataona kila kilichochumbani
Akili kama hizi ndio zimejaa bongo hii na ndio zinautunza umaskini wetu. Very primitive mindset.Acheni ujima nyie,huko ulaya kwenyewe bandari zinaendeshwa na wawekezaji na sio serikali,hao DP world wanaendesha bandari nyingi tu ulaya yan mje kulalamika kwa iko kibandari chenu uchwara,ngojeni waje hao DP muone kama kuna meli itakaa bandarini siku 3 au wiki kule out anchor kusubiri kuingia bandarini,hao meli ndani masaa tu ishadischarge na kuondoka na nyingine inaingia,acheni upuuzi na ujuha
Nionyeshe Jambo kubwa tulifanya likawa na tija.Tuwe na akiba ya maneno
Ufaidike wewe kama Nani?hivi, tukiwapa DP world hii bandari, tutafaidika na nini, manake kodi hatutapata wao ndio watasimamia? au nini, tuelewesheni. sisi tutabaki kufaidika na nini?
kama Mtanganyika. ongea kama mwanaume usitafute mabwana hapa mbuzi we.Ufaidike wewe kama Nani?
Kwahiyo mikataba yenye terms za kipumbavu tukubali tu!!Akili kama hizi ndio zimejaa bongo hii na ndio zinautunza umaskini wetu. Very primitive mindset.
SSH anataka tutoke hapa tulipo, tusiendelee kuacha fursa ya kiuchumi ikawa inapotea kila kukicha. Tunajenga SGR halafu bandari iendelee kuwa ya kijinga yenye misusuru ya foleni zisizo na tija, ambazo hutengeneza mazingira ya rushwa kila siku.
Tunapenda sana kufuga ujinga na kuutetea kwa hoja nyepesi za kisiasa. Hata kile kifo cha shabiki mmoja pale uwanja wa Taifa mechi ya Yanga vs USM Algiers chanzo ni rushwa tu, wangeweza kufungua milango saa tatu asubuhi lakini hawakutaka wakasubiri saa saba mchana ili uwepo msongamano wa watu na wao ndio muda wao wa kutengeneza pesa rahisi rahisi.
Siasa za kijinga zimetupotezea sana muda na hatuumizwi na hali hii hata kidogo tunaona poa tu kuishi kama mdudu aliyefungiwa ndani ya chupa tupu ya bia!.