BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 4,548
- 11,901
Leo mchana Ruto anajindaa kwa kile kinacho aminika ni hotuba ya kupunguza baadhi ya mawaziri wake na kuunganisha baadhi ya wizara ili kubana matumizi ya pesa za walipa Kodi wa nchi ya kenya ambao ndio wanaoumia na mzigo mkubwa wa kuendesha Serikali.
======
Rais Ruto ametoa hatua zifuatazo kupunguza matumizi ya Serikali;
Kwa Tanzania hali ni tofauti, huku tunahimiza kulipa kodi ambayo sana inatumika kuendesha Serikali hasa hasa kununua Magari ya anasa.
Tuna hadi Naibu waziri mkuu cheo cha mchongo ambacho hakipo kikatba ila kimewekwa kwa sababu za siasa na mzigo tunabeba sisi.
Ukiachana na hayo bado tuna Baraza la Mawaziri kubwa sana na sana limekaa kimchongo sana.
Tanzania tuna Baraza kubwa sana la Mawaziri nazani kiliko hata Kenya ilivyo, na baadhi ya wizara zimekaa kimchongo hazina maana yoyote ile zaidi ya kuongeza mzigo kwa wananchi.
Huku tunahimizwa sana hata na mwigulu tulipe Kodi, Ila tusicho kijua hio kodi inatumika kugharamikia anasa za Watawala wa hili Taifa, huku wananchi wakiendelea kuwa masikini.
Na Watawala hawako tayari kupunguza Mzigo wa Baraza la mawaziri kwa sababu limekaa kisiasa hasa kulipana fadhila.
Pia, soma=> Yanayojiri Maandamano Kenya: Vifo vya waandamanaji vyafikia 26 baada ya watu wawili waliokuwa wakiendelea kupatiwa matibabu kufariki

- Punguzo la bajeti kwa shilingi Bilioni 177
- Fidia ya wote walioumia na kupoteza maisha wakati wa maandamano ya muswada wa fedha
- Ukaguzi kamili wa deni la Taifa kufanyika ndani ya siku 90
- Kusitishwa kwa nafasi za CAS
- Kusitishwa kwa safari zote za umma zisizo za lazima
- Hakuna afisa wa Serikali kushiriki katika harambee
- Hakuna kununua magari ya maafisa wa Serikali kwa mwaka mmoja isipokuwa vyombo vya usalama
- Hakuna bajeti kwa mke wa Rais, naibu Rais au mke wa waziri mkuu
- Kampuni za Serikali 47 zimevunjwa
- Gharama za ukarabati kupunguzwa kwa nusu
- Matumizi ya siri yameondolewa
- Washauri wa Serikali wamepunguzwa kwa 50%
- Wafanyakazi wote wa Serikali kustaafu miaka 60 bila muda wa ziada kuongezwa