Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Hakika,

Hili suala waongee wafikie tamati, either Misri ampatie mchango Ethiopia wa Bwawa na watapatiana umeme au alipe Ethiopia asimamishe na kuchukua umeme kutoka Aswan, Misri.

Yote kwa yote, wasilete vita maana Afrika wakimbizi wanafakiria Tanzania tu.
kwa hatua walitofikia sioni mwenye uwezo wa kuwazuia Ethiopia
 
Egypt wanajiona kama wakoloni. Hawatufai. Hata5kutoa maji Ziwa Victoria wanang'aka.

Ethiopia ni wenzetu zaidi. Ni moja ya nchi zilizokuwa upande wetu wakati wa vita dhidi ya Iddi Amin.

Tunajua Egypt wapo kwenye kwenye ujenzi wa bwawa la Stieglers.
 
Yeye Misri ni nchi gani inayompangia masharti katika matumizi ya maji ya mto Nile?
Inatakiwa Nchi zote ambazo ni chanzo cha mto Nile zimame kwa umoja wao kupinga ukoloni wa hao Mafarao.
Yaani huyu mwarabu alivyo na roho mbaya hata sisi huku tukinywa maji ya ziwa Victoria yeye roho inamuuma.
Nchi zote zisimame kwa pamoja kupinga huu ukoloni wa Misri, hili swala sio la Ethopia peke yake, maana wakishawadhibiti Wahabeshi wataleta tena chokochoko zao kwa nchi nyingine.
Kwani nani aliipangia Tanzania kuwa mmiliki wa mlima Kilimanjaro.
Nani aliipangia Tanzania kumiliki eneo kubwa la maji ya ziwa Victoria na Kenya iwe na eneo dogo, kwanini wasigawane asilimia sawa na Uganda.
Kwanini Rwanda, Burundi nao wasiwe na eneo la ziwa.
Kwanini Uganda wapo landlocked wakati Tanzania ina bandari kama tatu.
Kwanini DRC iwe kubwa sana na yenye mali nyingi wakati Rwanda na Burundi ni ndogo na hazina maliasili.

Hayo maswali na mengine mengi yanafatia kwenye swali lako.
Misri ndo hakujipangia mipaka yake. Waliopanga matumizi ya maji ndio waliopanga mipaka ya Tanzania. Mbona sisi tulipigana na Iddi Amin alipotaka kuibadilisha?
Kenya wakisema Kilimanjaro ni ya kwao utatumia vigezo gani kusema si yao ni ya kwetu. Utatumia vigezo vilevile ambavyo Misri wanatumia, MKATABA. Na nchi zote za Afrika zilikubaliana kuheshimu mikataba ya kugawana milki. Hata sisi Tz na Malawi tunagombea ziwa Nyasa, kitakachofanyika ni kusoma na kutafsiri mkataba unasema ziwa linagawanyika kivipi.
 
Nadhani wanachokosea Misri ni kutumia vitisho katika hili ila kiubinadam nadhani nchi zinatakiwa kumuelewa maana hamna kitu essential kwa uhai na usalama wa Taifa kama maji. Sasa em fikria Nile ndo chanzo cha maji baridi kwa wananchi wa Misri halafu leo usikie kuna mtu anafanya shughuli zake zinazoweza kuathiri negatively flow ya maji ya mto husika kuja kwako. Utajisikiaje? Ulishawahi kupigwa na jua halafu ukakosa maji ya kunywa! Ndo wanachokihisi wamisri unapoingilia flow ya mto Nile.
Tutangulize utu na ubinadamu kulihukumu hili
Kwa hio yeye pekee ndie mwenye haki ya kuwanywesha wananchi wake wote zaidi ya milioni 100 maji ya mto nile, ila sisi tulivyotaka kupeleka mradi wa maji ya kunywa dodoma tokea ziwa victoria alitujia juu na kutuzuia?
Kwenye mto huo huo yeye amejenga bwawa kubwa Aswan la kuzalisha umeme hakuna mtu aliyemuuliza, ila kitu hicho hicho Ethopia anataka kufanya anampiga marufuku.
Mwambieni huyo Mmisri kua mimi nimeshaamua kama yeye hataki watu wengine wanywe maji ya mto Nile basi pia awakataze na wananchi wake kunywa hayo maji, na pia kama hataki wengine watumie maji ya mto Nile kuzalisha umeme basi na yeye pia aache mara moja kuzalisha umeme kupitia maji hayo ya mto Nile.
 
Kwani nani aliipangia Tanzania kuwa mmiliki wa mlima Kilimanjaro.
Nani aliipangia Tanzania kumiliki eneo kubwa la maji ya ziwa Victoria na Kenya iwe na eneo dogo, kwanini wasigawane asilimia sawa na Uganda.
Kwanini Rwanda, Burundi nao wasiwe na eneo la ziwa.
Kwanini Uganda wapo landlocked wakati Tanzania ina bandari kama tatu.
Kwanini DRC iwe kubwa sana na yenye mali nyingi wakati Rwanda na Burundi ni ndogo na hazina maliasili.

Hayo maswali na mengine mengi yanafatia kwenye swali lako.
Misri ndo hakujipangia mipaka yake. Waliopanga matumizi ya maji ndio waliopanga mipaka ya Tanzania. Mbona sisi tulipigana na Iddi Amin alipotaka kuibadilisha?
Kenya wakisema Kilimanjaro ni ya kwao utatumia vigezo gani kusema si yao ni ya kwetu. Utatumia vigezo vilevile ambavyo Misri wanatumia, MKATABA. Na nchi zote za Afrika zilikubaliana kuheshimu mikataba ya kugawana milki. Hata sisi Tz na Malawi tunagombea ziwa Nyasa, kitakachofanyika ni kusoma na kutafsiri mkataba unasema ziwa linagawanyika kivipi.
Brother Armata kiuhalisia upo sahihi, lakini ukifuatilia watu hawapingi Misri kutumia Mto Nile bali wanapinga Misri kutaka kutumia mabavu na kuweka zuio na kuingilia suala la taifa jingine.

Misri itumie diplomasia kutatua suala, iketi meza moja na Ethiopia wakubaliane huyu maji atapata vipi na huyu umeme atapata vipi, basi hakuna la ziada.
 
sio silaha yoyote ambayo ni tishio kwa Ethiopia ambayo wanayo misri

mchakato hapa ni kuipiga Ethiopia na iwe koloni ili isijaze maji kwenye bwawa au watumie air force yao kushambulia bwawa (hit and run)

sioni ndege ambazo zinaweza kutekeleza hiyo mission bila kudunguliwa

alafu hawa Ethiopia army huwa wanafanya mazoezi kwa kudungua ndege za kenya in Somalia unajua kwa nn ?
Wakenya ni majuha usishangae wapo upande wa Misri,,
 
Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.

Vita kamili inanukia Kati ya Ethiopia na Misri kupigana kwaajili ya matuzi ya maji ya mto Nile, hasa baada ya Ethiopia kujenga bwawa (Gerd) kubwa la kufua umeme kwa kutoa maji ya mto Nile kujaza bwawa hilo litakalotumia mabilion ya ujazo ya maji ya Nile.

Misri kwa upande wake inahofia kuwa ujazo wa maji ya mto Nile yatakayofika Misri utapungua hivyo kuathiri maisha na uchumi wa Misri.

Kwenye ugomvi huu Ni vema Tanzania ikaunga mkono upande upi na kwasababu gani?
Sijakuelewa labda unisahihishe umesema Ethiopia ni chanzo kikuu cha mto nile,kivp wakati tunajua souce kubwa ni ziwa victoria
 
Na hii program ya kupeleka maji ya Victoria mjini Dodoma makao makuu ya nchi, siku moja nasi tutatunishiwa misuli na hao washenzi.

Ninakumbuka Wakati wa Lowasa akiwa waziri wa maji alipoanzisha kampeni ya kuvuta hayo maji kuyaleta Shinyanga, hao washenzi walianza kuleta ngebe, lakini sikuelewa kilichoendelea baadaye!
 
Brother Armata kiuhalisia upo sahihi, lakini ukifuatilia watu hawapingi Misri kutumia Mto Nile bali wanapinga Misri kutaka kutumia mabavu na kuweka zuio na kuingilia suala la taifa jingine.

Misri itumie diplomasia kutatua suala, iketi meza moja na Ethiopia wakubaliane huyu maji atapata vipi na huyu umeme atapata vipi, basi hakuna la ziada.
Misri katumia ubavu gani kama wameita majadiliano na Ethiopia kagoma kushiriki. Mabavu gani yametumika wakati wanakaribisha mjadala mezani. Kuna mwanajeshi wa Misri kalipua bwawa, au lini wametishia kutumia jeshi.

Kwanza Misri alishabadili msimamo wake kwenye mjadala uliopita. Aliomba maji yajazwe kwa hatua, Ethiopia inataka kuyajaza kwa mkupuo jambo la hovyo kabisa. Pia Misri aliomba maji yasihamishwe mkondo maana yatapungua kwenye channel. Sasa ng'ang'ania alafu watumie jeshi uone Ethiopia anavyokaa asubuhi na mapema. Kwanza hakuna hata ya kupigana direct, kuna kabila la Wahoromo wakipewa silaha wanapigana wenyewe na serikali yao.
 
Vita kwa ajili ya maji haiko mbali, chanzo halisi cha mto Nile ni Lake Victoria. Time will tell
 
Misri katumia ubavu gani kama wameita majadiliano na Ethiopia kagoma kushiriki. Mabavu gani yametumika wakati wanakaribisha mjadala mezani. Kuna mwanajeshi wa Misri kalipua bwawa, au lini wametishia kutumia jeshi.

Kwanza Misri alishabadili msimamo wake kwenye mjadala uliopita. Aliomba maji yajazwe kwa hatua, Ethiopia inataka kuyajaza kwa mkupuo jambo la hovyo kabisa. Pia Misri aliomba maji yasihamishwe mkondo maana yatapungua kwenye channel. Sasa ng'ang'ania alafu watumie jeshi uone Ethiopia anavyokaa asubuhi na mapema. Kwanza hakuna hata ya kupigana direct, kuna kabila la Wahoromo wakipewa silaha wanapigana wenyewe na serikali yao.
Oke, mie nawaombea amani, utulivu na kunufaika mto Nile.
 
Sijakuelewa labda unisahihishe umesema Ethiopia ni chanzo kikuu cha mto nile,kivp wakati tunajua souce kubwa ni ziwa victoria
Hata maji ya ziwa Victoria Kuna pahala yanakotoka, lakini Kuna white Nile na blue Nile ambayo inakutana pahala na kutengeneza Nile inayokwenda hadi Misri. Blue ndiyo inayochangia maji mengi kwenye Nile watanisahihisha Wana geography. Blue Nile inatoka Ethiopia/Eritrea huko
 
Endapo ikitokea vita basi hata Misri na Ethiopia watapigana pasipo sababu za msingi, na Tanzania katika vita hiyo inabidi iwachape wote.

Vyanzo vya mto Nile ni mkanganyiko mkubwa na watu wanachukulia kwa wepesi.

White Nile, inawezekana* chanzo chake ni Rwanda/Burundi, Mto Kagera au Ziwa Nyanza (Victoria).

Blue Nile kwa hakika chanzo ni Ziwa Tana, Ethiopia.

Great Nile the mixer of White and Blue Nile inaanzia Khartoum, Jamhuri ya Sudan baada ya White x Blue Nile kuungana na kuendelea Ardan, Cairo hadi Alexandria.

Sasa sijaelewa wanaenda kupigana sababu ya Greater Nile, White Nile au Blue Nile?

Kama wanapigana sababu ya Greater Nile basi Tanzania awaadhibu wote kwa kushirikiana na Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Sudan. Endapo chanzo cha mapigano ni Blue Nile basi Ethiopia ana haki ya kumpiga Misri na kwa White Nile bado Tanzania ana haki ya kuwachapa wote.
Nimeimeza kama ilivyo nitaipeleka kijiweni huko nionekane mtaalam.

Nitasimulia kila kwenye kilinge hadi ikae kichwani.

Salute kwako.
 
Na hii program ya kupeleka maji ya Victoria mjini Dodoma makao makuu ya nchi, siku moja nasi tutatunishiwa misuli na hao washenzi.

Ninakumbuka Wakati wa Lowasa akiwa waziri wa maji alipoanzisha kampeni ya kuvuta hayo maji kuyaleta Shinyanga, hao washenzi walianza kuleta ngebe, lakini sikuelewa kilichoendelea baadaye!
Maji ya Nile lazima yaje kuleta kizaazaa kikubwa. Inasemekana Vita ya tatu ya dunia itakuwa Ni kugombania maji.

Hata Israeli ilitakaga kuwaadhibu waarabu kwa kuugeuza uelekeo wa maji ya Nile kuingia bahari ya Hindi kupitia shinyanga singida, Dodoma, morogoro hadi bahari ya Hindi.

Lakini pia Ni rahisi kuweka sumu kwenye maji yanayokwenda kwa waarabu kutokea Ethiopia na nchi nyingine za bonde la Nile
 
vita huwa inamatokeo ya kushangaza sio kama misri atajaribu kufanya ujinga wa kuishambulia kijeshi Ethiopia

tusiwabeze Ethiopia ni taifa kongwe na wana historia nzuri saana kijeshi sasa sioni kama misri anaweza kuipiga na kufikia malengo kwa kutumi kuweka military base Somaliland dhidi ya Ethiopia

Sent using Jamii Forums mobile app
Geographic location ya Ethiopia iko vizuri kivita dhidi ya Egypt.
 
Hata maji ya ziwa Victoria Kuna pahala yanakotoka, lakini Kuna white Nile na blue Nile ambayo inakutana pahala na kutengeneza Nile inayokwenda hadi Misri. Blue ndiyo inayochangia maji mengi kwenye Nile watanisahihisha Wana geography. Blue Nile inatoka Ethiopia/Eritrea huko
Blue Nile inatoka Ziwa Tana, Ethiopia ni mchango kwa Greater Nile kwa asilimia 24, White Nile ni mkanganyiko inaweza kuanzia Ruvyironza, Nyabarongo (Rwanda x Burudani) na Mto Kagera kuelekea Ziwa Nyanza (Victoria) na kuanza safari kueleke Jinja, Juba hadi Khartoum kuungana na Blue Nile kutengeneza Greater Nile.

Chanzo cha Ziwa Nyanza (Victoria) ni mito mingi katika uwanda wa bonde la ufa kuu upande wa magharibi ya Afrika Mashariki (Kanda ya Ziwa Nyanza, Kusini Uganda, Rwanda na Burundi).
 
Sasa inapoelekea ikitokea vita basi itahusisha Misri, Ethiopia, Jamhuri ya Sudan, Sudan Kusini, Uganda na Tanzania + (Rwanda na Burundi).

Tanzania yenye mchango mkubwa wa mto huo haitakiwi kukubali mkataba wa 1919's huko, Tanzania imepata uhuru 1961 na haikuingia mkataba huo, hata Ethiopia itumie hiki kigezo.

Unless, kila mtu atumie rasilimali zake katika mipaka yake, na hapo Ethiopia anamiliki Ziwa Tana na Blue Nile katika eneo lake.
Mzee kwani mipaka ya nchi zetu tuliiweka sisi? Mbona Ni wakoloni haohao?
 
Back
Top Bottom