Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

... kiujumla sio kwamba Egypt anamkatalia Ethiopia kujenga hilo bwawa - hapana. Anachotaka ni mkakati wa namna gani halitaathiri pakubwa maisha ya wamisri wanaotegemea hayo maji kwa kila kitu. Na mkakati mmoja wapo ni lijazwe kwa awamu ama taratibu wakati Ethiopia ana-prefer "big bang" approach. Kwa sababu za kibinadamu ningetafuta hybrid approach kati ya hizo mbili.
Nani aliwapangia namna ya kujaza Aswan Dam?
 
... kiujumla sio kwamba Egypt anamkatalia Ethiopia kujenga hilo bwawa - hapana. Anachotaka ni mkakati wa namna gani halitaathiri pakubwa maisha ya wamisri wanaotegemea hayo maji kwa kila kitu. Na mkakati mmoja wapo ni lijazwe kwa awamu ama taratibu wakati Ethiopia ana-prefer "big bang" approach. Kwa sababu za kibinadamu ningetafuta hybrid approach kati ya hizo mbili.
Hata mimi naona lijazwe kwa awamu, wakati likijazwa Ethiopia utumie umeme wa Aswan Dam.
 
Basi nchi zote zenye haki na hayo maji, TZ ikiwemo, ishiriki kuidhibiti Misri

Haya mambo magumu sana aisee nasoma comments mdogo mdogo halafu nimejikuta napata swali

Wale wamisri wanaotujengea Nyerere hydro tumekubaliama nao nini??? Isije ikawa tumewaahidi kuwaunga mkono wakimbana Ethiopia
 
... kiujumla sio kwamba Egypt anamkatalia Ethiopia kujenga hilo bwawa - hapana. Anachotaka ni mkakati wa namna gani halitaathiri pakubwa maisha ya wamisri wanaotegemea hayo maji kwa kila kitu. Na mkakati mmoja wapo ni lijazwe kwa awamu ama taratibu wakati Ethiopia ana-prefer "big bang" approach. Kwa sababu za kibinadamu ningetafuta hybrid approach kati ya hizo mbili.
Aione FRANCIS DA DON maana ukisoma comments zake unaona kabisa hajui hili.
 
Haya mambo magumu sana aisee nasoma comments mdogo mdogo halafu nimejikuta napata swali

Wale wamisri wanaotujengea Nyerere hydro tumekubaliama nao nini??? Isije ikawa tumewaahidi kuwaunga mkono wakimbana Ethiopia
Kumpiga mhabeshi misri itamchukua siku tatu tu ashaweka kambi somaliland na jibuti halafu misri wana mfumo wa kuzuia makombora wa thad na S 3000 unategemea nini
 
Mkuu,

Misri ana eneo Mediterranean Sea anaweza kuvuta maji kutokea Port Said, Alexandria na Marsa Matruh.

Misri ana eneo Red Sea anaweza kuvuta maji kutokea Sham el Sheikh, Suez, Ismailia na Hurghada.
Maji ya chumvi hayo
 
UK na USA wanaipa supports misri ili kuihakikishia Israel usalama

na muda huohuo in deep Israel hawataki kuiona misri imara ili waendelee kuwa wababe wa middle East

in short haya mambo ni mapana saana
Unafiki wa mataifa ya magharibi umejidhihirisha hapa. Wakati Egypt imefanya uchaguzi wa demokrasia, Muslim bortherhood walishinda, wakamchezea fix Morsi, mpaka Sisi akachukua madaraka. Utasikia wa magharibi wakipiga kelele pale Jeshi likichukua nchi na kudai wanahofia demokrasia kuporwa, ila kwa Egypt wamechekelea.
 
Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.

Vita kamili inanukia Kati ya Ethiopia na Misri kupigana kwaajili ya matuzi ya maji ya mto Nile, hasa baada ya Ethiopia kujenga bwawa (Gerd) kubwa la kufua umeme kwa kutoa maji ya mto Nile kujaza bwawa hilo litakalotumia mabilion ya ujazo ya maji ya Nile.

Misri kwa upande wake inahofia kuwa ujazo wa maji ya mto Nile yatakayofika Misri utapungua hivyo kuathiri maisha na uchumi wa Misri.

Kwenye ugomvi huu Ni vema Tanzania ikaunga mkono upande upi na kwasababu gani?
Hatulazimiki kuunga mkono yeyote
 
Egypt ndilo taifa la 2 nyuma ya Israeli kupokea misaada kutoka Marekani. Israeli ndio buffer zone, stabilizer katika Mashariki ya Kati. Uhai na ulinzi wa Israeli dhidi ya waarabu unalitegemea Egypt. Hivyo Egypt in silaha na ujuzi wa kufa mtu
Niambie Egypt ndio stabilizer pale mashariki ya kati sio Israel. Israel anaweza akasumbuana na kina Syria, lebanon, jordan ila kwa Egypt anajua kama wale ni watata. Hataki kujikuta anapigana na Egypt kwa sababu anajua Egypt iko well equipped ukilinganisha na majirani wengine walojaa upuuzi. Halafu vile Egypt na Gaza ndio jirani, Israel na allies wake wasingependa kuona Egypt inaanza kusupport Gaza.
 
Ni kweli kabisa Mkuu. Militarily Egypt is among the most powerful countries not only in Africa but globally. Wakati wa utawala wa Anuwar Saadat Iliwahi kuchapana na Israel katika vita ambayo ilibidi Marekani ipeleke jeshi na vifaa wakati vita ikiendelea. Mkuu wa Majeshi wa Misri alisema anaiteketeza Israel na wakati huo walishakua wameigawanya mapande mawili.

Marekani ikaiambia Misri isimamishe vita otherwise inaipiga nuclear Cairo. Saadat akaamuru Mkuu wake wa Majeshi wasimamishe vita, jamaa akakaidi akasema yupo tayari kui sacrifice Cairo lakini waiteketeze Israel!!! Anwar Saadat akamfuta kazi Mkuu wake wa Majeshi wakiwa katikati ya vita

Baadae vita vikasimamishwa na wakaingia katika mkataba maarufu wa Camp David (Yom Kippur War)
Hizo propaganda sijui umezitoa wapi, Misri haijawahi kumpiga Israel na alishapigwa vibaya mno Hadi Israel akaikalia sehemu ya Misri (Sinai)
Israeli occupation of Sinai - Wikipedia

Misri akaomba msaada kwa Marekani amuombee kwa Israel ili window majeshi Sinai, moja wapo ya masharti Ni Misri kuitambua Israel Kama nchi, na Hadi leo Misri ndio Taifa pekee la Kiarabu linaloitambua Israel Kama nchi

Hiyo Yom Kippur war ilikuwa Ni Vita ya Egypt na Syria kutaka kukomboa maeneo yao ambayo waliporwa na Israel (Sinai and Golan Heights) kwenye Six Days War, hata hivyo walishindwa, hadi USA akaja kuwapatanisha

Kuna Hadi Rais Nasser walimuua kutokana na Hili la kudhalilishwa na kuwapigia magoti Mazayuni

Misri anaweza akawa anakimbiza hapa Afrika Ila Duniani Ni mtu mdogo Sana, hata hapo Uarabuni mwenyewe Ni mtu mdogo sana
 
Pia tegemea Sudan yote, Tanzania, Uganda na wengine wote wenye maslahi na Nile na ambao wanabinywa na huo mkataba prehistoric kuwaunga mkono watoto wa mfalme Solomon na malkia wa Shebba
Hao ulowataja wote, watakuwa wanaongea tu, action zikiwa sifuri. Sudan mwenyewe alikubaliana na Egypt ET wasijenge hilo bwawa. Kama sikosei katika huo mkataba Sudan na Egypt waliwekwa kundi moja la kumilikishwa Nile. Kikubwa nchi ulizotaja zitajikita kwenye diplomacy rather than confrontation. Ila USA, UK na wenzao, watajikita kwenye supplies za military. Although sio kwamba USA na allies wake watapeleka majeshi yao, lakini wataipa silaha Egypt za uhakika katika kumpiga Ethiopia ikibidi.
 
Yaan nchi zote zinazotumia mto Nile tuungane Misri watatupiga mpaka tuchakae msicheze na hiyo nchi jeshi namba kumi na moja duniani ndo upeleke wahabeshi
Haaaa na tutachakaa kwelikweli hawajui ya kwamba licha ya Misri kuwa ndani ya Afrika lakini kijeshi iko dunia nyingine kabisa.
 
Hizo propaganda sijui umezitoa wapi, Misri haijawahi kumpiga Israel na alishapigwa vibaya mno Hadi Israel akaikalia sehemu ya Misri (Sinai)
Israeli occupation of Sinai - Wikipedia

Misri akaomba msaada kwa Marekani amuombee kwa Israel ili window majeshi Sinai, moja wapo ya masharti Ni Misri kuitambua Israel Kama nchi, na Hadi leo Misri ndio Taifa pekee la Kiarabu linaloitambua Israel Kama nchi

Kuna Hadi Rais wao walimuua kutokana na Hili la kudhalilishwa na kuwapigia magoti Mazayuni

Misri anaweza akawa anakimbiza hapa Afrika Ila Duniani Ni mtu mdogo Sana, hata hapo Uarabuni mwenyewe Ni mtu mdogo sana
Misri duniani niyakumi na moja Israel ya kumi nambili wacha Israel kubebwa ila misri ningumu sana kama unaufahamu mkataba wa Camp David utaelewa tu
 
Na kwa upande wa Ethiopia kuna Tanzania, Uganda, Sudan and probably South Africa
As said before, hakuna katika hao watakao mpa military support, wataitana AU na kusisitiza wakae Mezani. Egypt ni mlinzi wao USA na ISrael na allies wengine, kwa sasa hawapo tayari Egypt iwe destabilized, Sisi wanaenda nae vizuri.
 
Katika vita una judge nani atashinda kutokana na uhalisia uliopo kwa wakati huo. Una jeshi la namna gani na liko equiped kiasi gani na utayari lilionao kwa mafunzo. Hivi vyote vinaibeba Misri unapoilinganisha na Ethiopia. Labda kama kuna teknolojia ya haraka na gharama reasonable waliyonayo Ethiopia kubadili yale ma Boeing ya Ethiopia Airlines yawe heavy bombers labda wanaweza kuchukua hata round kwenye ring na Mafarao
Teknolojia sio decisive peke yake kuamua nani atashinda Vita, historia inaonyesha hivyo

Marekani keshachezea kichapo huko Vietnam, Huko Afghanistan pia, Taliban ambao Ni wakulima tu wamemchosha hadi anatoa jeshi Sasa hivi
 
Misri bhana wapuuzi kweli eti wana mkataba Tanzania tusitumie yale maji nilimkubali sana Lowasa kulisimamia lile mpaka maji kuanza kutumika ukanda wa kaskazini huko...ilikua ajabu sana maji mengi ila hawaruhusiwi kutatumia Kama ilivyo sasa....Misri alibebwa na wakoroni hapo mwenye haki ni Ethiopia maji yanapita kwake ayatumie.....

Mmisri mpuuzi sana. Yani sema tu haiwezekani, ila kama vipi tungebana wasipate hata kikombe.
 
Kwa hiyo kama sio vilema mtapiga mbizi kufika Misri kuipiga. Au mtatumia mitumbwi kwenda Suez canal?
Misri ina wanajeshi active zaidi ya laki moja. Rais wao wa sasa ni Field Marshall, anatumia sana budget kwenye jeshi. Misri kamdindia Turkey pale Libya na yupo anajiandaa kupeleka majeshi ndo huyuhuyu unataka tumchangie.

Vita hautatumia mapanga na mishale mnayotumia uko kwenu Tarime.
Haaaa mkuu huyu mshikaji sijui anaichuliaje Misri aisee maana anaongea kirahisi sana.
 
Back
Top Bottom