Tanzania Kinara wa Kupokea hela za msaada kutoka USAID Afrika nzima. Yasemekana tutaathirika sana

Tanzania Kinara wa Kupokea hela za msaada kutoka USAID Afrika nzima. Yasemekana tutaathirika sana

Kisiwa chetu cha Amani chenye Rasilimali nyingi kinapokea misaada ya mabeberu na Mabepari takribani Milioni 512 Kila Mwaka. Imeelezwa.

Gazeti la Euronews limetaja kuwa Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi zitakazo athirika kutokana na Hatua ya Donald Trump na Elon Musk kusitisha misaada hiyo.

Gazeti hilo limeleza Tanzania yenye watu Milioni 65 linapokea kiwango sawa na Nigeria yenye watu 220Milioni.

Kalagha Bahooo........Hizi hela huwa zinaenda wapi mbona ni nyingi sana?View attachment 3224545
Mimi nimefurahishwa na Trump kukata misada. Japo kuwa nasikitika kuwa watu wasio kuwa na hatia wataumia sana. Ila ukweli ni kwamba viongozi wa afrika wengi ni matahila.

Ebu imagine hakuna bara lenye wagojwa wengi wa ukimwi kama Africa, miaka yote mijitu inanunua mav8 ila dawa za kupunguza makali ya ukimwi wanaachia wahisani wasaidie. Karibu kila sector mhimu za Africa karibu kila nchi Asilimia 60% ya budget ni misaada ya wahisani. Na mijitu inavaa suit kila siku kwenda ofisini? Sasa kama mnategemea misada kuendesha nchi ofisini mnaenda kufanya nini?
 
Wewe uko hapa Tanzania Huwa zinatumika vizuri na hao NGOs?

Magufuli alitaka kuwafuta

Mwigulu alitaka wapitishie hela Serikali for monitoring ila wakapiga makelele ikaishia.

Trump futa huo ujinga,wanakula tuu hizo hela hakuna wanachofanya
Mwigulu alitaka afanye monitoring au washirikiane na wenzie kudhulumu sehemu ya hizo fedha?!
 
Serikali inataka hela za NGOs zipitie kwao ili waanze urasimu kuzitoa na kusumbua watu.
Huu ndio ukweli, hela zinahitajika kumbe wao wamezipeleka kwenye kununua mabasi ya CCM🀣 matokeo yake zinaanza story na ubabaishaji. NGO's walifanya vyema kukataa upumbavu huo sababu serikali yetu inajulikana ilivyo inapokuja swala la pesa.
 
Tanzania ni mshirika muhimu wa U.S katika ukanda huu wa Afrika. Katika kipindi cha miaka 30 tumetembelewa na "active presidents" wa USA 3 (linganisha na nchi zingine za Afrika katika kipindi hicho).

Orodha ya viongozi wa U.S. (Rais & Makamu) waliowahi kutembelea Tanzania wakiwa madarakani (Chanzo: Mtandao)

1. Richard Nixon – 1969 (President)
2. Bill Clinton – 1998 (President)
3. George W. Bush – 2008 (President)
4. Barack Obama – 2013 (President)
5. Kamala Harris – 2023 (Vice President)

Mwaka jana 2024, PEPFAR iliadhimisha miaka 20 ya mafanikio katika kuisaidia nchi yetu kukabiliana na maradhi ikiwemo TB/HIV (Taarifa za tukio ziko mtandaoni, kasome).
Baraka Obama alikuja Tz mwaka gani
 
Kisiwa chetu cha Amani chenye Rasilimali nyingi kinapokea misaada ya mabeberu na Mabepari takribani Milioni 512 Kila Mwaka. Imeelezwa.

Gazeti la Euronews limetaja kuwa Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi zitakazo athirika kutokana na Hatua ya Donald Trump na Elon Musk kusitisha misaada hiyo.

Gazeti hilo limeleza Tanzania yenye watu Milioni 65 linapokea kiwango sawa na Nigeria yenye watu 220Milioni.

Kalagha Bahooo........Hizi hela huwa zinaenda wapi mbona ni nyingi sana?View attachment 3224545
Acha tujifunze namna ya kujtegemea. TUmezoea misaada hadi tunaitana chawa.
 
Wanyimwe misaada wauze ma V8 yao, watauza tshirts na hata hizo bendera zao.
 
Back
Top Bottom