Tanzania kuna familia ambazo zinaishi kifalme bila Watanzania kuzifahamu au wamepiga kimya tu

Watoto wa baba wa taifa wapo waliowahi kujaribu kugombea uongozi wakafeli hata uchaguzi mkuu uliopita walijaribu. Tukija kwa JK , Mwanawe aligombea akapata na mkewe aliteuliwa na JPM je angekataa? Sioni jitahada za JK kwenye hilo.
Mkono mtupu haulambwi mkuu ndio maana wengine hawapati lakini wengine wanapata !! Usiseme wewe huyajui hayo hapa kwetu !!
 
Na kadri mda unavyozidi kwenda wanazidi kujiimarisha huko tuendako itakuwa ngum sana kuwaondoa
 
Hakuna jipya hapo. Reference ni familia ya Bush au Clinton huko USA.
 
Mwalimu amesomea, kwani hao walisomea wapi huo uwaziri, ubunge na urais? Kama sio kupendeleana kwa manufaa yao binafsi,
Acha wenge wewe
Kazi ya kuomba kura na kusomea ipi ngumu?

Unazan zamani mpaka kupata nafasi ya kusomea ualimu ilikuwa lelemama?
 
Mkuu hapo unamaama kwamba wanaofaidi kodi zetu kwa kiasi kikubwa hapa nchini ni hizo familia tatu tu.

Familia ya Jakaya Kikwete.

Familia ya Alhassan Mwinyi

Na Ya Rais Samia Suluhu.

Hapo upo sawa kabisa.
Umekuaje siku hizi?au umesahaulika kwenye keki ya Taifa?yaani Awamu zote zinakupita mkuu?

Acha utani
 
Halafu ndo wanajiita swala 5.mbafuu kabisa.
 
Yaani baba Rais mstaafu, mtoto anakuwa Rais tena, hivi kweli watanzania milioni sitini wote hao hakuna wakuchukua nafasi hiyo?!!!.

Kweli Kama ambavyo maji hutiririka kutoka nchi kavu kuelekea baharini kwenye maji mengi, basi na uongozi wa Tanzania upo hivyo.
 
Nyerere
mkapa
Magu
RIP. ALL .. wote wapo Mlengo mwingine .. (huohuo ulowaza) sioni alama zao zaurithi why ... muda utatupa majibu
 
Daah,ila jiwe alipigwa vita kila kona Aisee.yaani kila alilofanya lilionekana Halifai ,Mungu akaona apumzike tu.

zile kelele ni kwa kua ni Rais alietokea nje ya mfumo wao,hawakutarajia Rais atoke kwingine

 
Swali ni kwamba kwani watadhibitiwa na taasisi gani au sheria gani itawazuia , kama ni hivi hivi basi itakuwa hivi hivi tu hata waje chauma !!
Kweli katiba mpya ni muhimu sana at the very least waondoe kinga kwa Viongozi wote through ammendment.

Viongozi wawe wana-declare vipato na assets zao kabla ya kupewa uongozi na kila mwaka kuwe na audit ya mapato yao.

Mtu anapata ubunge, ukuu wa mkoa, uwaziri, mkuu wa Taasisi za serikali, urais, baada ya mwaka ana mabilioni.

Inabidi achunguzwe na aeleze amezipataje, amefanya biashara gani halali na aonyeshe documents zote.

Viongozi wasichaguliwe kiholelaholela. Muhimu kuwe na confirmation hearing kwa viongozi wote wakubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…