Tanzania kuna familia ambazo zinaishi kifalme bila Watanzania kuzifahamu au wamepiga kimya tu

Tanzania kuna familia ambazo zinaishi kifalme bila Watanzania kuzifahamu au wamepiga kimya tu

Unakuta kwenye familia moja baba ni Rais mstaafu, mama ni mbunge na Mtoto ni mbunge na ni naibu waziri, hii familia inahitaji shamba kwa ajili ya kulima chochote au ni kuitegemea serikali tu?

Familia nyingine unakuta baba ni Rais mstaafu, Mtoto ni Rais na Watoto wengine wawili ni wabunge hii familia bila serikali inaweza kuishi?

Familia nyingine mama ni Rais , Mtoto ni mbunge na mkwe ni mbunge na ni waziri.

Huu mfumo umekaa sawa au nimekuelewa tofauti?
Ndio maana hawataki kusikia habari za katiba mpya ya Warioba
 
Huku kwetu Baba mshona viatu
Mama mchoma vitumbua
Mimi muendesha boda boda
Sister Fundi chereani
Brother Balozi wa nyumba 10
Watoto wote shule vidumu ufagio hakuna aliyekatiza form 4.

Kuna siku hii familia yetu itatoa Mkuu wa Wilaya au Katibu Kata !.
Mpaka MTU ashikwe mkono na wenye nguvu !
 
Kuna wakati huwa namkubali sana J.K Nyerere jamaa alikua mzalendo wa kweli sana

1. Jaribu kumlinganisha Nyerere kwa mtazamo wa umuliki wa mali kwa kuwaangalia maraisi wengine wa Afrika katika kipindi chake, angalia maraisi hao walipokuwa madarakani na baada ya kustaafu

2. Nyerere alidiriki kufunga ubalozi wa Israili na kufuta mahusiano nao licha ya kuwa Nyerere alikua mkatoliki haswaaa, lakini alifanya hili kuonyesha kuchukizwa na uvamizi wa Israili katika ardhi ya Palestina

Na hili alilifanya licha ya msaada mkubwa tu wa ujenzi wa UDSM na MUHIMBILI HOSPITAL ya leo

3. Alikubali lawama za udini kwa Wazee wa Dar es Salaam lakini alisimamia misingi ya usawa kwa wote aliishia kutoa shukran za teuzi kwa nafasi mbalimabli za watoto wa waislamu walioshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika na sio kuleta udini katika serikali kama walivyokuwa wakitaka wao

4. Jamaa alikua na uwezo mkubwa sana wa kuchomeka na kurithisha familia na watoto wake katika nafasi za meza kuu ya nchi lakini hakufanya hivyo na aliwaacha wapambane wenyewe kupitia demokrasia

Ukiachana na Hawa matapeli kama kina Kakobe, Lusekelo, Mwamposa n.k.

J.K Nyerere alikuwa nabii wa kweli Tanzania na unabii wake ulishatimia na wote tumeshuhudia kwa macho
 
Maisha msongamano sana.Dah!Hizi ndizo nyuzi chokonozi.Anyway,waache waishi hivyo kama hawaleti fujo.😂😂😂😂
Yule mzee late Nyerere alichemka sana kwa upande huu asee, pamoja na mazuri aliyoifanyia hii nchi kwa issue ya familia yake sijui kwa undani na sitaki kufuatilia au kujua nini alifanya.

Although ni wazi angefanya as we seeing now ahahahaa sijui feedback from wazee wa nyuma ya keyboard na wamasiasa wangelia na hiyo familia.

But kwa hawa waliotoka na wanaoendelea kupitia mfumo huu hakuna kizazi chao kitakuja kukosa kushika madaraka nchi hii, course tayari ukiwa kiongozi wa kisiasa lazima mwanao aletwe kwa nguvu kushika wadhifa wowote anaopewa.
 
Katiba mpya haihusiani na hilo wala, inaweza ikawepo lakini bado yakawa yanatokea

Kwanini tuandikie mate mjomba? Katiba iliyopo tumeyaona na ni halali kwa mujibu wa Katiba.

Bado hudhani tusijaribu mustakabala mwingine:

1. Utakaozuia wizi na ujambazi wa kura kama wa 2019/20?
2. Utakatoa fursa sawa kwa wote?
3. Utakahakikisha uwepo wa tume ya uchaguzi?
4. Utakaompunguzia rais madaraka ya u Mungu mtu kama ilivyo sasa?
5. Nk nk?

Kwani kwa sasa na kwa mujibu wa katiba vyeo rais hugawa kama njugu tu?

Hudhani hawa kina Riz moko, January, Nape, Mchengerewa na wengi wa namna hiyo fursa za kujiajiri haikuwa muhani nao kuwahusu?

Au wewe uko kwenye familia hizo na hapa niko kwenye kumpigia mbuzi gitaa tu?
 
Mkuu hapo unamaama kwamba wanaofaidi kodi zetu kwa kiasi kikubwa hapa nchini ni hizo familia tatu tu.

Familia ya Jakaya Kikwete.

Familia ya Alhassan Mwinyi

Na Ya Rais Samia Suluhu.

Hapo upo sawa kabisa.

Na bado huoni umuhimu wa katiba mpya?
 
Ardhi yenye tutuba itaendelea kutoa mazao bora
Ardhi ya Mobutu, ardhi ya Obote ardhi ya Kaunda, ardhi ya Gaddafi, ardhi ya Sadam na nyingine nyingi tu mbona bado hazijatoa mazao bora ?? Usicheze na Mwenyezi Mungu !!
 
Kwetu sisi hata si wavivu kabisa. Tuanaamka assubuhi mapema na jembe. Chai yetu ugali na mlenda ni kazi kwa kwenda mbele. Wanatuita wanyonge. Hatujui suti hatujui tiles na msouth, hatujui mboga tatu, bia haituimudu japo kazi tunapiga.
Hao wanatuambia kilimo ni uti wa mgongo kumbe sisi kinatupinda mgongo.
Siasa imewapaisha angani tukiwatazama kwa mshangao!!!!
I feel you bro..
 
Mtandao una gharama zake boss....

Rejea ule wa mwaka 2003-2005 ulihusisha wakubwa kutoka pande muhimu kuanzia siasa,utumishi mpaka dini.

Hii mitandao ya kwetu huku chini inatusaidia Sana kutukwamua kwenye hali ya kimaisha tunayopitia huwezi kuifananisha na hiyo ya hao wakubwa.
Kwanza huwezi kutengeneza mtandao kama wewe mwenyewe huna kitu na huna jina. Labda utengeneze mtandao wa VICOBA.
 
Na wewe pambana familia yako iishi kifalme.
Soma sana,
Fanya kazi kwa juhudi sana.
Tafuta konekeksheni sana,
Jipendekeze sana sehemu sahihi kwa wakat sahihi
AU
Pigani katiba mpya itakoyotoa fursa kwa yoyote mwenye talents na jitihada
Suala la maisha mazuri halina uhusiano na kusoma sana. Wapo wasomi wakubwa tu, kama anavyosema mbunge Msukuma,mnaongea naye mkitaka kuagana anakuomba elfu kumi.
Ni vizuri kuuangalia mfumo wetu kwa ujumla, kuona watanzania wanawezaje kupata access kwenye fursa zinapopatikana pamoja na raslimali tulizo nazo nchini.
 
Back
Top Bottom