Mkenya ambaye atajifanya hadi sasa haijui Tanzania ilivyo atakua na matatizo, kwanza kwa awamu hii, ina maana wanahabari hawakumbuki jamaa aliyekimbilia huku kama ameliwa risasi 38, yule anaitwa Tundu Lissu. Halafu hiyo ndio nchi unakwenda kuhoji hoji.
Watz waachwe wlivyo watajauana wenyewe, ikitokea una shughuli lazima uende kwao huko, jitie ububu kabisa, wala hata usitazame taarifa zao za habari maana utajikuta unaongea kuzihusu maana wengi hatujazoea wanachopitia, utajisahau udhani uko kwenye nchi yenye uhuru kama kwetu.
Piga kimya, shughulika na issues zako kisha geuza mara moja, kama vipi agiza magazeti ya Kenya, yapo yanauzwa huko.