Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Kusimamishwa kazi bila kuchukuliwa maelezo ya awali ni sahihi kwa mjibu wa sheria za kazi...!!? Au barua yakusimamishwa kazi na kuchukuliwa maelezo kipi huanza kati ya hivyo viwili.
Kwa sekta ya Umma Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya 2002 na Kanuni zake za 2003 zimetoa mwongozo wa kushughulikia mashauri ya Nidhamu kazini.

1. Inaweza na taarifa ya uchunguzi kuhusu suala fulani ambalo Mwajiri anadhani kuna uvunjifu wa sheria.
2. Ripoti ndiyo itaonyesha ni mfanyakazi gani anahusika na vitendo vya uvunjifu wa sheria au Kanuni za ndani
3. Mwajiri atamuandikia Mfanyakazi husika barua kwa tuhuma ambazo ana muhimu na kumpa muda wa kujieza

3. Baada ya muda inatakiwa Mfanyakazi atawasilisha maelezo ya tuhuma husika kwa Mwajiri. Kama Mwajiri ataridhika na maelezo ya mtuhumiwa basi shauri litafungwa.

4. Kama Mwajiri hajaridhika ndipo atamsimamisha kazi mfanyakazi.

5. Ataunda Kamati ya kusikiliza shauri la mfanyakazi ambalo wajumbe wake wanapaswa kuwa maofisa wenye cheo zaidi ya cheo cha mtuhumiwa.

6. Kamati itamuita mtumiwa na kumpa mashtaka mtuhumiwa na muda wa kujibu tuhuma kwa mwandishi.
 
Naomba unitumie hizo Sheria kwa 0762904054(WhatsApp)

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Upo mkoa gani wewe mkuu?
 

Kwa masuala yote ya kukiukwa vipengele vya mkataba (breach of contract agreement) kama mfano hilo ulilotaja unatakiwa kufungua shauri ktk Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya Kikazi (tunaitwa CMA) katika mkoa uliopo/unaofanyia kazi

Kwa masuala yote uvunjifu wa sheria za kazi (breach of labour laws) mfano kufanyishwa kazi zaidi ya masaa ya kisheria bila kulipwa malipo ya ziada (overtime), kulipwa ujira ulio chini ya viwango vya kisheria, kutokupewa likizo, kubaguliwa sehem ya kazi n.k haya ya nature hii unawasilisha ktk Ofisi ya Idara ya Kazi ktk mkoa wako ulipo/unakofanyia kazi ili wayashughulikie
 
Habari wakuu!.

Naomba kujulishwa kwa mujibu wa sheria.Ni mambo gani uangaliwa kwenye fedha za kujikimu anazopewa muajiriwa mpya pindi anapo report kazini?.Na je,tofauti ya malipo ya fedha ya kujikimu kwa waajiriwa wa level moja serikalini kutofautiana uzingatia nini?.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Naomba uweke wazi kwenye hili hapa : zaidi ya miaka miwili sijapatiwa mkataba wa kudumu:

malipo ninayoyapata hayaendani na viwango kisheria Nina bachelor degree lakini nalipwa chini ya laki 6 hili swali kwa mujibu ya minimum wage order ya mwaka 2013 inahainisha kila sekta na kiwango cha pesa yake sasa ungesema unafanya sekta ipi ili upewe jibu je iyo pesa ni kubwa au ndogo

sipo kwenye mifuko ya kijamii hapa wanakuwa wametenda makosa 2 kwa mujibu wa sheria ya nssf ya mwaka 1997 namarejeo yake ya 2018 ni kosa kwa muajiri wa sekta binafsi kutojisajili na mfuko sasa inawezekana hajajisajili na mfuko ndio maana hata wafanyakazi wake hawachangii nssf ilo kosa la kwanza kosa la 2 kutokukulipia wewe kama mfanyakazi wao ambapo kisheria anatakiwa apigwe penati ya asilimia 10% kwa kila mchango wa kila mwezi kwa muda huo wa miaka 2

hata Ikitokea nafukuzwa kazi sina cha kujitetea kuna mamlaka husika ambazo hutatua kesi zote baina ya muajiri na muajiriwa inaitwa tume ya utatuzi na usukuhishi ( CMA) hivyo haki yako haitapotea

Nini cha kufanya kama una uhakika wa kupata kazi nyingine wafungulie shtaka mahakama ya kazi iliyopo karibu na wewe kama upo dar es salaam zimegawika kwa mkoa mfano kinondoni, ilala na temeke na utawapelekea samansi ya kesi na wito wa kuitwa mahakama ya kazi na madai yako yatakuwa kama ifuatavyo

kufanyishwa kazi bila kuwa na mkataba kwa muda wa miaka 2
kutoenda likizo kwa muda wa miaka 2
kutochangiwa kwenye mfuko wowote wa kijamii
kulipwa mshahara kima cha chini tofauti na maelekezo ya minimum wage order ya 2013 ila hii inategemea upo sekta ipi

Angalizo utakapoanza hayo mambo hakikisha unakazi nyingine ipo mkononi.
 

ipo hivi kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007 kuhusu mkataba wa muda maalumu kukoma wenyewe pale muda wake unapofika tuseme mkataba wako ulitakiwa kuisha 2020 january na ilipofika boss wako hakutoa notes ya kuonesha mkataba utakapokaribia kuisha siku 28 kabla kwamba hawatakupa mkatba mpya ikafika mwezi wa 2 wakakulipa mshahara mwezi wa 3 akakulipa mshahara hapo sheria inatambua mkataba ule umekuwa mpya yani mi miezi 12 mingine sasa akija kukuachisha kwa kigezo mkataba uliisha na muda ulikuepo kwenye mktaba kuisha na yeye kukaa kimya kosa ni lake mwenyewe na anatiwa kulipa miezi iliyobaki.
 

Safi majibu mazuri sana japo kuipata iyo haki sasa hapo ndipo ilipo changamoto
 
Per diem ndio nini?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je muajili asipo toa mkataba kwa muda wa miaka 2 then mwishon ana kufukuza kazi je yupo sahihi au ana kosa na je nikipewa mkataba siku ambayo ana nifukuzisha kazi ndipo Ni sain je nikubali au nigome msahada jaman
 
Naomba kufahamu Kuwa mfano kampuni aipeleki pesa ktk mfuko wa jamoi nssf kwa muda wa miaka miwili akuna ata sent tano na ninapo kwenda nssf Wanadai awanaditell za kuniusu Mimi Kama kweli michango yangu ina kwenda nilipo kuwa nafanyia kazi napewa salary slip ambazo zinaonesha ukatwaji wa pesa na kupelekwa kwao je endapo ikitokea gafra kampuni yangu imesepa je pesa zangu nazipataje angali nssf Wana kanusha kuwa awaja pokea pesa za michango yangu na kampuni Ina dai imepeleka pesa Nini ushauli je Mimi natakiwa kuwalipot kampuni au nssf
 
Kama NSSF wanatimiza majukumu yao wanapaswa wawe wamemshtaki Mwajiri wako kwa kutowasilisha michango yako kwenyebtawi lao lililo karibu na Mwajiri wako.

Kama Mwajiri kasepa itakuwa imekula kwako
 
Kama NSSF wanatimiza majukumu yao wanapaswa wawe wamemshtaki Mwajiri wako kwa kutowasilisha michango yako kwenyebtawi lao lililo karibu na Mwajiri wako.

Kama Mwajiri kasepa itakuwa imekula kwako
Kweli Ni tatizo tunapo kwenda kuwapa tarifa nssf wanasema wanalifanyia kazi miaka sasa
 
Thanks kaka naomba msaada wako pia kwa hili. Kazin kwetu tumeambiwa kwa njia ya sim kuwa tutatumiwa form ya kusain ili kuchukua rikizo ya miezi mitatu isiyokuwa na malipo je ni haki kisheria?. Na kingine jinsi ya kukokotoa holidays endapo unahitaji kuacha kazi saraly 300 kwa mwezi
 
Na je akifanyiwa termination hakuna haki zake za msingi ukilinganisha na haki ambazo angepata akifanyiwa early retirement?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu

Sheria ipoje ikiwa mfanya kazi kaacha kazi baada ya kumaliza likizo lakin yupo ndani ya mkataba an vp swala NSSF kwa tajir kutoa barua na kutotoa barua no amri yake?


Sent using Jamii Forums mobile app

Sheria ya shirika la taifa la hifadhi ya jamii marejeo ya mwaka 2018, inaweka wazi kabisa itafanya malipo ya mwanachama wa aina 2
a) kuachishwa kazi maana yake ikiwemo ukomo wa mkataba au kuachishwa kwazi kwa sababu yoyote ile kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini mwaka 2004 na kanuni za ajira na mahusiano kazini mwaka 2007
b) Kupunguzwa kazini

Fomu ya NSSF/UB1 inasehemu za kuweka tiki katika vipengele tajwa hapo juu ila ukiacha kazi mwenyewe NSSF haina ilo fao kwa sasa

Kumbuka: Malipo haya atalipwa tu mfanyakazi ambaye hana ujuzi ila kwa mfanyakazi mwenye ujuzi atalipwa 30% ya jumla ya michango yake ila kama ilo utaliona gumu basi utasubiri ukifika miaka 55
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…