Iddi Mwambasi
Member
- Jul 20, 2019
- 6
- 1
Habari,
Naomba mtu anielekeze jinsi ya kukokotoa acting allowance
Private au serikalini?Wadau naomba kujua sheria ya kazi inasemaje kwasasa hivi kuhusu
1.Notice of termination.
2.severance pay.
Wadau naomba kujua sheria ya kazi inasemaje kwasasa hivi kuhusu
1.Notice of termination.
2.severance pay.
Swali lako nitalipa ufafanuzi kama ifuatavyo na wajumbe wengine watachangia pale nitakapopungukiwa
masuala yote ya kazi yanasimamiwa na sheria na kanuni zinazojulikana kama ( SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI YA MWAKA 2004 na KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI MWAKA 2007) sasa tuanze kufafanua kwa mujibu wa maswali yako.
Notice of termination.
Kwa kutumia Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya Mwaka 2004 kifungu cha 41 kinaeleza wazi ni siku 28 ndio pande zote mbili zinatakiwa kutoa taarifa za Notice of termination. ikieleza sababu na muda pia kuna masharti ya utoaji wa Notice of termination haiwezekani mtu yupo likizo alafu umpe Notice of termination pia mfanyakazi hutakiwi kukataa kufanya kazi kipindi cha Notice of termination
Lakini katika Notice of termination kwa mfano una mkataba wa muda maalumu Notice of termination itatolewa ikikupa taarifa kwamba hautaongezewa mkataba pindi pale mkataba wako utakapofika mwisho maana yake mkataba wako utakoma wenyewe pale muda utakapofika mwisho hii ni kwa mujibu wa KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI YA MWAKA 2007 kifungu cha 4
Notice of termination hutegemea sababu maana yake kuna sababu kama 4 za kupewa Notice of termination na kila sababu inautaratibu wake wa kufatwa 1. Mwenendo mbaya 2. Kutohitajika 3. Kupunguzwa kazini 4. Kutokuwa na uwezo au kukosa uwezo baada ya kuajiriwa hizi sababu zote Notice of termination hutolewa kwa kufatwa taaribu tofauti tofauti sasa hapo inategemea wewe umeangukia wapi
severance pay
Hii kwa kiswahili tunaita kiinua mgongo mahesabu yake huwa ni mshahara wa siku 7 kwa idadi ya miaka uliyotumikia kampuni husika mfano mshahara wako kwa siku ni 10,000 na umekaa kwenye kampuni miaka 2 itakuwa hivi 10,000*7*2=140,000 hivyo kitakachobadilika ni iyo idadi ya miaka uliyotumikia kampuni husika sasa sheria ipoje ili uweze kupata
SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI MWAKA 2004 kifungu cha 42 ipo hivi unatakiwa kutumikia angalau miezi 12 kampuni husika, pia usiwe umeachishwa kazi kwa mwenendo mbaya kama Wizi na makosa mengine ya utovu wa nidhamu
Ila unapolipwa kiinua mgongo unatakiwa malipo mengine uwe umeshalipwa bila kupunjwa kama likizo na je kuachishwa kazi kwako kulifatwa taaratibu halali za kisheria
Natumaini hata wengine watakuja kuongeza nilichochangia mimi natanguliza shukrani
Mkuu asante sana kwa ufafanuzi wako lkn nina maswali mawili hapo kutokana na maelezo yako.
1.ulisema kuna sababu kama nne ambazo zinaweza kutumika kama kigezo cha termination na ukataja kigezo kimojawapo ni kutotakiwa,sasa hii kutotakiwa inakuwaje au inakuwa na vigezo gani?ina maana kama muajiri hanipendi ana uwezo wa kuniachisha kazi bila sababu na sheria inamruhusu?
2.Napenda kujua pia kwenye kipengele cha mwenendo mbaya kazini,ni vitu gani ambavyo mfanyakazi akivifanya vinatafsiriwa kama mwenendo mbaya kisheria?
Mkuu sawa nimekuelewa kwenye hilo swali namba 2 sawa halina utata,lakini kwenye majibu ya swali namba moja bado linanitatiza yaani kwa mfano umeajiriwa kwenye kampuni halaf ukawa huendani nayo labda kwenye team work au ktk mambo mengine uliyoyataja,sasa swali linalonitatiza ni kwamba watawezaje kupata evidences za kupeleka kwenye mahakama ili ikubalike kwamba kweli huendani na team work yao?Kutohitajika hiki kiswahili chake ndio changamoto ila naamini tutaelewshana tu kifungu cha 22 kanuni za ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2007 ipo hivi mfano una mahusiano mabovu na wafanyakazi wenzako tunakuweka kundi la kutohitajika kuna hii ipo sana sehemu kama CASINO Kuna wale wateja wakubwa wanaocheza kamari hata za milion 200 anaweza kusema kwa meneja wako kwamba kila nikija hapa nikimuona huyu muhudumu sijisikii amani nazani unaelewa kinachofuata au kuna ile kampuni ina utamaduni wa team work sasa ikaonekana wewe huendani na huo utamaduni inakuwa ngumu kuendelea kuhitajika kwenye kampuni hiyo au wewe unafanya kazi microfinance na tunajua zina riba kubwa ila huwezi kuja kusikia mfanyakazi wao kakanusha kwa chochote ukifanya hivyo tunasema huendani na utamaduni wa kampuni. hapo ndo point ya kutohitajika inapokuja.
mfanyakazi akivifanya vinatafsiriwa kama mwenendo mbaya kisheria? 1. KUCHELEWA 2 DHARAU 3. ULEVI WA KUPINDUKIA 4. KUPIGANA 5. KULETA HASARA KUBWA KWA KAMPUNI 5. MAKOSA MENGINE YA KINIDHAMU
mfano unamahusiano mabaya na wafanyakazi wenzako kinaitishwa kikao cha pamoja na wafanyakazi yataandikwa maudhurio ya wafanyakazi na maridhio ya kikao kimaandishi alafu unaondolewa ili kutohatarisha usalama eneo la kazi sasaMkuu sawa nimekuelewa kwenye hilo swali namba 2 sawa halina utata,lakini kwenye majibu ya swali namba moja bado linanitatiza yaani kwa mfano umeajiriwa kwenye kampuni halaf ukawa huendani nayo labda kwenye team work au ktk mambo mengine uliyoyataja,sasa swali linalonitatiza ni kwamba watawezaje kupata evidences za kupeleka kwenye mahakama ili ikubalike kwamba kweli huendani na team work yao?
mfano unamahusiano mabaya na wafanyakazi wenzako kinaitishwa kikao cha pamoja na wafanyakazi yataandikwa maudhurio ya wafanyakazi na maridhio ya kikao kimaandishi alafu unaondolewa ili kutohatarisha usalama eneo la kazi sasa