stakehigh
JF-Expert Member
- Aug 9, 2019
- 7,134
- 4,556
Kuna vitu vya ajabu sana duniani.
Hata wakisema Tanzania idadi ya mabilionair imeongezeka kwa asilimia 90, endapo mie sio miongoni mwao au sifaidiki na chochote haina tija sana kwangu endapo sitazitumia hizo taarifa kujikwamua na hali niliyonayo.
Unawezakuwa unabishana hapa na Mkenya kwamba mabilionair wamepungua lakini kumbe huyo unaepigizana nae kelele haumkamati hata kidogo.
Hapa ingefaa hizi taarifa kujadiliwa kwa kuangalia mambo gani yamepelekea kupungua au kuongezeka kwa utajiri? Endapo ni siasa safi, mbona tunaambiwa Tanzania kwa sasa sio rafiki kwa biashara?
Na kwa harakaharaka Kenya ni kama kiuchumi wako vizuri na mazingira ya uwekezaji yanavutia, Je hizi taarifa zinazingatia vitu gani vya msingi?
Na mwisho kila mmoja kuona anahusika au kunufaika namna gani na hizi taarifa?
Kutambiana kwa kurushiana vijembe haitakua na manufaa sana.
Unaambiwa ufaulu umeongezeka kwa kiasi kikubwa wakati wewe umefeli, inaingia akilini kweli kupokea hizo taarifa? Utafurahia hizo taarifa tu endapo uko miongoni mwa waliofaulu.
Itategemea na wewe unavozichukulia. Hizo tarifa hazipo apo kukunufaisha kwa sababu na Wao walivoanza maisha hawakupata izo taarifa wanufaike , misingi ni ile ile kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na kujituma! You obvious not expecting anything from these news as an advantage but its a good sign of increasing purchasing power