Tanzania leads Kenya in the list of dollar millionaires





Nkurekebishe kitu, statistically most rich people are self made ndo wanaohesabiwa apo! In fact kma umesom hip taarifa wamesema kabia ni exclusion ya hawa politicians so inamaana most of them are self made

Cha pili Economically kipindi unadhan uchumi ni mgumu ndo kipindi watu wanapiga ela ndefu, Warren buffet alishwahi kusema kwamba kipindi uchumi ni mbovu wewe unatakiwa kununua na kipindi uchumi uko vizuri basi ndo unauza,

Cha mwisho cha kurekebisha in general uchumi wa Tanzania sio mgumu kama mnavopotray, people are making enough money and people are living well, watu wanaingiza pesa za ktosha waaendesha ndinga Kali na reports ndo kama izi list ya matajiri imeongezeka kuliko ata Kenya(THE BIGGEST ECONOMY IN EAST AFRICA) mm sio tajiri but I can testify most things mnaongea kuhusu uchumi ni non sense! Two things I can testify, your either not adding value to your bussiness or your very lazy
 
Na inavoonesha hata hao matajiri wa Kenya huenda utajiri wao ni matokeo ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma maana naona wanasiasa na viongozi wastaafu wanaongoza mfano familia za Kenyatta na Moi
 
Nimeisoma hiyo article ya citizen na nikaona imeandikwa kufurahisha kadamnasi tu. Nahisi hata mwandishi haijui Kenya kabisa. Hata hivyo kuna mahali amekiri mwenyewe kuwa ni kama taarifa za kufikirika, nanukuu; "A lack of robust data to fit into our complex econometric model on certain countries means we had to make assumptions"

Kiukweli uchumi wa Kenya uko juu na wala tusipepese macho. Jiulize kwa nini Kenya ina makampuni zaidi ya 200 yaliyowekeza Tanzania na je Tanzania wana Makampuni mangapi yaliyopo Kenya? Nchi zote za Afrika Mashariki ni soko la bidhaa za Kenya. Uchumi haudanganyi.

Angalia takwimu za bajeti za Afrika Mashariki kwa mwaka 2019/20; Kenya Tsh 66.8 Trilion, Uganda Tsh 23.6 Trillion na Tanzania 30.4, Rwanda Tsh 6.8 Trilion, Burundi 1.8 Trilion na South Sudan Tsh 3.5 Trillion (ambayo jumla ya yote ni Tsh 66.1 Trilion). Picha unayopata ni kwamba uchumi wa Kenya ni mkubwa kuliko nchi zingine zote 4 za Afrika Mashariki yote zikiwekwa pamoja.
 
Mkuu Stuxnet, hii ya bajeti ya Kenya kuwa bigger kuliko the rest of EAC combined ndio naijua leo, hivyo naunga mkono hoja yako ya Kenya ndio uchumi mkubwa, ila hoja ilio mezani its volume ya mamilionea in numbers, not per unit, yes Kenya inaweza kuwa ni uchumi mkubwa ila umeshikwa na mabilionea wachache, lakini Tanzania ikawa ni uchumi mdogo, ila umeshikwa na utitiri wa vimilionea!.

Just imagine kama mimi tuu kazi yangu ni mwandishi wa habari, na wakati wa Kikwete nilikuwa milionea mwenye TZS 100+m kwenye Account yangu, then for sure Tanzania tutakuwa na vimilionea kibao vyenye more than TZS 100m bank account ambao ni zaidi ya 300 lakini tuna Watanzania wachache wenye billions, ambao hawazidi 50, lakini Kenya wao wana mabilionea 100, na vimilionea 100, tukija kwenye total numbers, mamilionea Watanzania watakuwa ni wengi kuliko waKenya in terms of numbers lakini tukija kwenye the volume ya huo umilionea wao, Kenya wakatuacha mbali.

Kuna kitu nilikinote nikauliza humu, sikumbuki hata nilijibiwa nini!.

Je, tunaweza kujenga Tanzania ya viwanda bila kutegemea mabeberu?, Ukaribu beberu na 'next door' ni fimbo au biashara tu?
P
 
Hata BBC ipo hii habari.... Au nayo imeandikwa na mwandishi wa the citizen
 
Ndugu zangu,

Hizi ni takwimu mpya Tanzania inatajwa kuwa na mamilionea wengi wa Dola kuzidi Kenya.View attachment 1377989

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina swali la msingi sana kwa mabilionea wa Tanzania na wanamkakati gani kwenye ubilionea wao wanakuwa sehemu ya kuongeza mzunguko wa fedha ndani au serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara iwe sehemu ya hili.

Niwe mahsusi zaidi.
Mo mwaka jana alimwalika JPM kulizindua kiwanda na kusindikika ngano. Ngano ile anauza kwa soko la ndani ya Tz na nje ya Tz. Raw material ya ngano anatoa India. Alipoulizwa kama anamkakati yeye in the long run asiendelee ku-import raw wheat, hakuwa na jibu. Anyway sio jukumu lake yeye kama bepari. Ila hapa ndipo kituo cha uwekezaji, Wizara ya Uwekezaji na Biashara, Wizara ya Kilimo na umwagiliaji waingie na kuwa na mkakati ili hayo ma-tani ya ngano ghafi yanayonunuliwa India, eventally yanunuliwe hapa. Mind you, kuna virgins land in Tz hatujawahi hata kutupa mbegu.
Huo ubilionea ungekuwa na maana kwa tricke down effect iwepo, otherwise, the Citizen nao sioni kama habari yao imeshiba kwa ku-connect na Tz ya kesho iweje bora.

Bakheresa anauza maziwa. Kwa siku anachakata lita 180,000. Maziwa haya ni ya unga toka India. Hapa yakija yanakuwa reconstituted.
Tuna mkakati gani maziwa haya ambayo final product tunanunua Watanzania yazalishwe ndani??? (How dow e tap ili hiyo fedha ya kununua raw milk say lita moja ni 1,000x180,000 x siku 300 za kiwanda kufanya kazi Bil 54 zinaenda india); ukijumlisha logistics kutoka kwa mzalishaji mpaka kiwandani its more money could flow our way.
Achilia mbali kazi ya consultation ya vert doctors kwa ng'ombe wetu wangepata hela kwa soko moja tu la Bakhresa.

Waziri wetu wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Uwekezaji, je wanaona kwa jicho hilo ili hao mabilionea wafanye biashara kwa kununua ndani raw materials.
Benki ya uwekezaji TIB Development, Benki ya Kilimo TADB wao wanafikiri nini???

Ahhhh....
Tanzania its a land of endless possibilities. If at all we could combine to solve domestic problems, kuna hela nyingi sana ingebaki ndani humu na TRA kuongeza Tax base. Waziri wa Fedha anafikiria nini kuwa part ya creation of new businesses/investments maana by defaults hizo ni revenue sources kwake.

Pensio funds, zinawaza nini ili ku-create new sources of income kwa kupata wanachama zaidi kwa open venture kama hizo hapo juu.
Mie nimetaja vyanzo vi-2 tu muhtasari, ambapo tukiwekeza fedha yake ipo, kwa sasa beneficiary ni India.

Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote
 
Hata BBC ipo hii habari.... Au nayo imeandikwa na mwandishi wa the citizen
Haijalishi media gani imeripoti, mana kwenye news industry media houses zina kawaida ya kuazimana taarifa. Jikite kwenye contents zangu tu.
 
Mkuu, kuna some of the senior advocates wamefungiwa ofisi kwa kushindwa kulipa kodi, wengine wamekimbiwa na wafanyakazi kwa kushindwa kulipa mishahara. hali zimebadilika. Ofisi ya wakili mkuu wa serikali imeondoka na tenda za watu.
 
Sakehigh,

Sioni kitu cha maana cha kujibishana nawe katika bandiko lako hili.

Lakini kilicho wazi ni kuwa hakuna popote uliporekebisha katika niliyoandika.

So I reserve my detailed comment on it.
 
Mimi mwenyewe mwaka huu lazima niingie kwenye hiyo list kuongeza idadi
 
Wanaoshika mabilioni wako 50?!!

Sidhani kama Tanzania hii kuna wilaya au mji inakosa watu wanaoshika bilioni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…