Tanzania na China zasaini mkataba wa uendelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka Mwanza - Isaka

Dar-Moro=300Km

Moro-Makutupora=426Km

Makutupora-Isaka=435Km

Isaka-Mwanza=220Km

Isaka-Rusumo=371Km

Kwa nini kazi zisiende kwa mfuatano ili hata ngoma ikikwama njiani ruti iwepo ya kuishia hata Isaka.

Wachina watamaliza na kukabidhi Isaka-Mza huku kipande cha Makutu-Isaka kikiwa bado hata tenda haijatangazwa halafu anaingia Rais mwingine na kusema reli siyo kipaumbele chake,mradi unaachwa kwenye mataa kama katiba mpya.
Alieruka kutoka section 2 hadi five analijua vema hilo ndio maana karukia huko ili beberu mwingine akiingia ikuru asije akakata bomba itamlazimisha kuunga,anayo experience ya bagamoyo port jamaa sio mbumbumbu anajua kusoma na kuandika.
 
Dar-Moro=300Km

Moro-Makutupora=426Km

Makutupora-Isaka=435Km

Isaka-Mwanza=220Km

Isaka-Rusumo=371Km

Kwa nini kazi zisiende kwa mfuatano ili hata ngoma ikikwama njiani ruti iwepo ya kuishia hata Isaka.

Wachina watamaliza na kukabidhi Isaka-Mza huku kipande cha Makutu-Isaka kikiwa bado hata tenda haijatangazwa halafu anaingia Rais mwingine na kusema reli siyo kipaumbele chake,mradi unaachwa kwenye mataa kama katiba mpya tunakuwa tumepoteza pesa bure.
Hapa tumefichwa jambo mkuu.
 
tunapongeza sana sana ndugu zetu wachina.tumpongeze pia kwa masharikiano yenye kuleta usulubu wa win win situation0
 
"Rais Xi Jinping nimemuomba watusaidie katika miradi mikubwa mitatu kule Njombe, nimemuomba watujengee KM 48 kule Zanzibar, nimemuomba watusamehe madeni yetu tuliyokuwa tumekopa, likiwemo lile tulilolibeba wakati tunajenga reli ya TAZARA" MagufuliJP

Taarifa: EastAfricaTV
 
Unajidai dona kantry alafu unaomba kusamehewa mkopo

Hivi na sisi tunaweza kuomba kusamehewa mikopo tuliyokopa kwenye mabenki?
 
Jamani wana JF wenye mlengo usio na nia njema kwa taifa letu tuache kulaumu hovyo.

Sisi kama Watanzania tunahitaji reli,maana reli itapunguza gharama za maisha kwa 40%. Hivyo kwa mkataba wa ujenzi wa reli ulisainiwa leo ni jambo jema kwa nchi yetu.

Tuache tabia ya kulaumu na kuponda kila jambo,China wamekuwa rafiki za watanzania kwa muda mrefu. Na wamekuwa msaada kwetu kila tunapowahitaji.Kabla na baada ya vita vya Kagera tulipata hali ngumu ya kiuchumi,China walitushika mkono, tusisahau.

Sioni kama ni jambo jema kuanza kuponda huu mkataba kisa tu ni wafuasi wa vyama vya upinzani ambavyo vimefanya vibaya kwenye uchaguzi uliopita. Habari za kuleta hisia kuwa wachina ni matapeli sio nzuri.

Pia tuwaamini viongozi wetu,sidhani kama wanaweza kuingia mikataba mibovu kiasi cha kuiweka rehani nchi yetu.

Maoni; SGR ikikamilika itakuwa na manufaa kwa kila mtanzania,tuache siasa za kizandiki na kupinga maendeleo.
 
Wachina ni matapeli a.k.a matajiri uchwara, na viongozi wetu wana 10% kwenye huo mkopo wa China. Kama ni kuwaamini viongozi waamini ww, lakini sio kila mtu anaweza kuwaamini viongozi walioko madarakani kwa wizi wa kura.
 
Kuidharau China kuwa ni tajiri uchwara sio hoja ya msingi. Utapeli wa taifa la China upo wapi? Unatakiwa China imrkuwa na msaada mkubwa sana kwa Tanzania usio na harufu ya kibeberu miaka nenda rudi.
 
Back
Top Bottom