Tanzania na Equinor / Shell yasaini mradi wa thamani dola bilioni 30

EnHeee, nimeliandika hili sasa hivi hapo juu.
Ni kama laana inatuandama vile.
Kwa jinsi hii tunayokwenda nayo, sijui kama kutatokea wakati nasi tukawa watu wa kusema tuna uwezo wa kutengeneza chochote!
Worst wana peleka watu Aberdeen University kwa zaidi ya miaka 10 chuo chenye kila aina ya degree ya hayo maswala you name it. Na kuna sponsored degrees za Shell inasomesha watu kibao kila mwaka kwa hela zao.

Mpaka leo hatuna tu hao wataalamu.

Usiku mwema.
 
Tanzania imesaini makubaliano ya kikazi na kampuni ya Norway iitwayo Equinor sambamba na kampuni ya Kijerumani Shell na hivyo kupelekea kuanzishwa kwa mradi wa ujenzi wa kusafirisha gesi asilia ambao unakadiriwa kugharimu dola bilioni 30.

Mradi huo uliotangazwa Jumamosi unakadiriwa kwamba uwekezaji wote unaohitajika kufanywa utakamilika 2025, na huduma ya kituo cha gesi asilia kusini mwa pwani ya Lindi unakadiriwa kuanza kutolewa mnamo 2029-2030.

Jambo hilo linaifanya Tanzania kupiga hatua moja mbele katika juhudi zake za kuanza kusafirisha gesi yake nje ya mwambao zake, zenye ujazo wa futi milioni 57 ( ujazo wa mita bilioni 1,630)
 
Wewe uko upande wa Negative tuu!
Hivi sisi ni wa Mwanzo duniani kuchimba Gas?
Watu wengine bana kujitia kujua kila kitu, wakati erikali ina watalamu bobezi najopo la washauri lawataalamu wazalendo na kutoka nje, Hivi tunakosaje kuto kuwa na Imani na serikali yetu ?
Miminadhani ni Hatua njema, Mapungufu yakijitokeza yata tatuliwa accordingly na siyo kupiga siasa kwenye uchumi.
 
Nina imani kuwa wazungu wamesaini mkataba huu huku wakiwa na 'pressure' kubwa ya kutaka kumkomoa Putin na kutaka kuiweka Afrika mikononi mwao dhidi ya mahasimu wao!
KWANINI, KWA MAZINGIRA HAYA, TUSIWE 'OPTIMISTIC' NA KUTARAJIA, HATIMAYE, KUFIKA NCHI YA MAZIWA NA ASALI? (SIO KULAMBISHWA TENA! 😅)
 
Paskali bwaa,
wewe umeambiwa hizo ni gharama za mradi,siyo mapato yatakayoingia nchini.Kabla ya kuushabikia twambie ni kiasi gani na kwa namna gani sisi tusio na elimu,mitaji na uwezo meadi huo utatunufaisha!
 
Hapa tukubali Jiwe alituchelewesha sana. Hii signing ilipaswa kuwa imefanyika tangu 2015, lakini uzalendo uchwara ukaingizwa kuturudisha nyuma. Right now na hii vita ya Ukraine tungekuwa tunavuna dola.
 
Hapa tukubali Jiwe alituchelewesha sana. Hii signing ilipaswa kuwa imefanyika tangu 2015, lakini uzalendo uchwara ukaingizwa kuturudisha nyuma. Right now na hii vita ya Ukraine tungekuwa tunavuna dola.
Kwenye hii gesi ya sasa unavuna dola ngapi? watu tumebakia kushabikia matrilioni ya pesa bia kujua contents za contract. Unaweza kujikuta umemshikia mtu anakamua ng'ombe wako maziwa, halafu akabeba maziwa yote wewe ukabaki umeambulia kale ka harufu ka maziwa.
 
What is the alternative? Maana tunalalamika sana, nini njia mbadala? Ni rahisi kusema usichotaka, sema unachotaka tukione halafu tukupe mrejesho.
 

Hiyo ni adhabu utakayopewa nchi ambayo inasheria ya mazingira na sehemu ya mkataba wako.


Na hayo ni madhara ya nchi maskini uchafuzi huo huo ukifanyika africa serikali zetu aziwezi kufanya kitu kwa sababu sio sehemu ya mkataba; mpaka tukawashitaki kwao ambapo wanabwana na sheria za corporate social responsibility.

Halafu wewe unaona ni sawa kuacha kuingiza hayo mambo mapema.
 
Ndio maana nikamwambia Pascal Mayalla hujui chochote kuhusu oil and gas. Sijataka kuongea haya. Hata mozambique wa kwao ni $20b. Kwetu ni $30b. How
 
Sio Mtwara wewe matako! Lindi,
 
Issue ni umri na kujadili au knowledge mkuu. Soma costs za LNG duniani, kisha angalia analysis ya TzLNG by NRGI alafu ndio uje hapa
 
Tusichotaka ni kubaki na harufu ya maziwa wakati maziwa yote yakiwa yamebebwa........nafikiri kama wewe ni critical thinker utakuwa umenielewa vilivyo.
Narudia tena, ni rahisi kusema usichotaka kuliko kusema unachotaka.
 
JPM alikataza mikataba isiwekwe wazi Wala kupeleka bungeni kwa kujitoa kwenye Open Governance Initiative kwa madai kwamba ni "Siri nyeti za serikali, ikiwekwa wazi itahujumiwa na mabeberu".

Ila kwakua waTanzania ndio hatujui kuhoji tukapiga makofi, sasa hiyo imeshaset precedence wote watafanya Siri!!
 
Video inayoonesha jinsi gesi asilia inavyochimbwa katika bahari kuu, kuchachatwa, kutayarishwa kuwa bidhaa kamili na kisha kusafirishwa kwa meli maalum kupelekwa ktk masoko ya dunia :

Liquified Natural Gas: From Treatment To Transport | ExxonMobil


Learn how liquified natural gas (LNG) can transform the energy industry, opening up the door to renewable energy production and distribution. Natural gas will be the world's fastest-growing energy source by 2040 thanks to its versatility, abundance and clean-burning qualities. There are an immense number of opportunities to cultivate, produce, transport and distribute this impactful resource to communities around the world, providing much-needed energy to those that need it. Natural gas has the potential to change how we think about power and the value it provides on a global scale. Watch how LNG can power urban communities by providing heat, electricity and the tools needed to build essential infrastructure.

00:12 What is natural gas?
00:22 Where can you find natural gas resources?
00:37 Where does the natural gas value chain start?
00:55 How do you treat and process natural gas?
01:30 How do you transport liquid natural gas?
01:55 How do you liquify natural gas?
02:18 How do you store natural gas?
02:48 How do you ship liquid natural gas?
03:32 How do you distribute liquid natural gas?

Discover why the liquified natural gas value chain is essential to so many people across the globe.

Source : ExxonMobil
 
Mbona TPDC wanao wataalamu na kuna interview ya DG wao akieleza shughuli za kuvumbua mafuta ambazo zimetumia wataalamu wa kiTanzania.

Tunakosa tu maybe vifaa na experience ila wataalamu mbona wapo wengi tu. Sema wengi wanakua poached na mataifa makubwa sababu ya maslahi makubwa kuliko Tanzania. Embu tuweni optimistic kidogo sio Kila kitu kulalamika tutafika lini?
 

Sasa kwanini tunawatumia wataalamu wa nje kwenye majadiliano; halafu wanaacha kuweka key issue katika framework za HGA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…