a4afrika
JF-Expert Member
- Apr 13, 2012
- 1,456
- 1,459
Ni miradi miwili tofauti. Huu ni wa Lindi, unaosemewa si wetu tena ni wa Mtwara.Tatizo mikataba yenyewe ni siri yule alisema kuna wizi huyu anasifia basi hujui nani umuamini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni miradi miwili tofauti. Huu ni wa Lindi, unaosemewa si wetu tena ni wa Mtwara.Tatizo mikataba yenyewe ni siri yule alisema kuna wizi huyu anasifia basi hujui nani umuamini
Huu sasa ndio mradi wa kweli wa maendeleo ya kweli wenye impact ya kweli kwenye uchumi wa nchi yetu kwasababu mradi huu ni mradi wa FDI, doleri bilioni 30 sawa na Trillion 70 za madafu, zinaletea kutoka nje zinakuwa injected ndani ya nchi yetu!, hii sio kitu ndogo!.
Japo bado hatujajua contents za huo mkataba, but definitely ule wasiwasi wangu kuhusu Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe! unakwenda kutokea!. Kuna kitu nilikisema hapo kuwa Tanzania tusipokuwa makini, kinakwenda kutokea, kwa ya juu juu niliyo sikia, nilichohofia kisitokee, ndicho kinakwenda kutokea!.
All and all, tumefika mahali lazima tukubali matokeo...
Pia Waziri wa Nishati, Mhe January Makamba, hili amelizungumza vizuri hapa
P
Ndio maana ukaambiwa kwenye gesi hujui kitu. Sasa ulikuwa unasifia nini na wakati hujui?Kiukweli on technicalities na costings mimi ni zero!. Nadhani hata hiyo LNG plant site kuwa off shore it has something to do with cost.
P
Kusimama na kumtetea Magufuli ni kujitoa ufahamu na kujivunjia heshima, pamoja na kwamba alikuwa na kelele nyingi sana za hadaa, kuwazubaisha wananchi.Sasa JK si walisema ni fisadi ndio maana nahoji kwa huyo mzalendo, msafi, malaika, kwanini alitamka kujitoa OGI iliyolazimu disclosure of matters with public interests kama mikataba ya rasilimali n.k?? Mpaka mikataba ya Bombardier, Ndege za ATCL kukamatwa ikawa Siri, Makubaliano ya Serikali na Barrick yakawa Siri maana hatujui hiyo kampuni inaendeshwa kwa mkataba upi n.k
Sasa kituko wafuasi wa mzalendo wanamuita Mama fisadi (Of course CCM wote wezi) anauza nchi kisa mikataba ya gesi haijawekwa wazi. Sasa ndio najiuliza huu unafiki ni kwa faida ya nani? Aliyezuia utekelezaji wa TAIT ni nani? Aliyeitoa Tanzania OGI ni nani??
Ndio natoa taarifa sasa kwamba mama naye hawezi iweka wazi sababu hata mtangulizi wake hakuweka na ndio hapo nasema JPM aliweka precedence mbovu.
Duh, hebu ifafanue vizuri hii mkuu 'Gobole', mbona inatisha?The fact kua reserve yetu in term of cubic ni less than mozambique bt mradi wetu una cost more than them must be a red flag, hakuna mzungu anafanya hio biashara kichaa, unless wamekaa gharama kubwa in purpose ili ROI ichukue muda mrefu.
Kwani china iliendeleaje? Si mpaka ilipofungua mipaka yake na ikashusha labor cost, masharti ya uwekezaji, Kodi, thamani ya pesa n.k Ili wawekezaji wamwagike na Leo hii imeshakua na viwanda vya wenyeji imetapakaa sababu ya technology spillover in fact na sisi tukiweza ku tap teknolojia wanazokuja nazo then tutaweza kuwa na local capacity ila hakuna nchi iliendelea bila FDI maana uchumi unahitaji fedha za kigeni na heavy manufacturing sector for value addition.Kama huwezi kuona kasoro kubwa iliyopo katika utaratibu wetu katika kuwawezesha na kuwatumia wataalam wetu hadi hapa tulipofikia kama taifa, miaka 60 na zaidi baada ya uhuru; nadhani hiyo "optimism" unayoiomba sijui itapatikana lini, baada ya miaka mia?
Bottomline ni kwamba kama tunavyotawanya raslimali alizotujalia Mwenyezi Mungu, ndivyo hivyo hivyo tunavyotawanya raslimali ya watu wetu, wataalam wengi tulio nao kwa kutowapanga vizuri, kuwawezesha ili waweze kutumia utaalam wao kwa manufaa ya taifa hili.
Hadi hapo tutakapopata uongozi unaotambua kasoro hii na kuirekebisha, tutaendelea tu kuwa vitegemezi kwa hawa hawa wanaokuja kuzoa mali zetu na kuendelea kutuachia ufukara wetu.
Mkuu Zitto Jr, ninakumbuka tulishalizungumzia hili la wachina kati yako na mimi, kama siyo wewe, basi nitakuwa ni pengine mkuu Yoda.Kwani china iliendeleaje? Si mpaka ilipofungua mipaka yake na ikashusha labor cost, masharti ya uwekezaji, Kodi,
EeeenHeeee!in fact na sisi tukiweza ku tap teknolojia wanazokuja nazo then tutaweza kuwa na local capacity ila hakuna nchi iliendelea bila FDI maana uchumi unahitaji fedha za kigeni na heavy manufacturing sector for value addition.
Usihangaike na kuitafuta makaratasi yahusuyo haya uliyoyazungumzia hapa, kwa sababu ninafahamu vyema jinsi gesi ile ilivyokuwa ikiungua kule Kilwa wakati inavumbuliwa na watu wetu wenyewe.2. Alafu kama haufahamu exploration ya mafuta nimesahau ni Safu ya milima gani ila wametumika wataalamu wa TPDC kwenye process nzima. Kuna document moja ntaipandisha humu inaeleza Miradi kadhaa ya gas exploration huko Mnazi Bay na Mtwara ambayo TPDC walikua involved directly kwenye process. So sio kama hatuna wataalamu Wala uwezo nadhani tunakosa tu Capital ya ku facilitate hizo gharama na hauwezi ukakopa Mradi mkubwa hivo na hauna uzoefu sidhani kama Kuna nchi zingekubali ku risk.
Kwenye suala la uvunaji gas, ni kati ya makosa makubwa ya ajabu aliyoyafanya Magufuli. Leo hii Tanzania isingekuwa inafukuzana na vikodi vya kwenye Mpesa.
Mapato ambayo yangepatikana kwenye mradi wa gas, yakilinganishwa na dhahabu, yangekuwa sawa na kulinganisha bahari (gas) na tone (dhahabu) la maji.
Lakini Kivuruge aliharibu, wawekezaji wakaondoka, alipogundua kuwa ameharibu akaanza kuwasihi kwa siri warudi, wakagoma. Walipogoma akaanza kuongea uwongo eti gas ya Tanzania imeuzwa kwa wachina? Wajinga, bila hata ya kujiuliza imeuzwa kwa namna gani, wakamwamini.
Leo ni kama tunaanza upya,wakati tulikuwa tumekaribia hatua ya uzalishaji.
Hapo ndiyo unaona jinsi mtu mmoja anavyoweza kuleta madhara makubwa
Kipindi Cha chairman Mao au Chiang Kai Shek China ilikua na uchumi Gani ndugu yangu, sembuse Japan was a power but China ilikua maskini kuna mpaka wakati watu zaidi ya million 20 walikufa kwa njaa.Mkuu Zitto Jr, ninakumbuka tulishalizungumzia hili la wachina kati yako na mimi, kama siyo wewe, basi nitakuwa ni pengine mkuu Yoda.
Sikubaliani na hii dhana potofu kabisa kwamba wachina walisubiri kuingia watu wa nje ndipo maendeleo yao yakapatikana.
Huu ni upotoshaji.
Ukisema "kupata msukumo" wa haraka katika maendeleo yao, hapo tunaweza tukajadili hilo.
Mchina amejiandaa mwenyewe, kwa juhudi zake hadi hapo alipoamua kuingia duniani kuungana na wengine. Mchina alikuwa na ujuzi wake wa kufanya mambo, ndiyo maana mashirika yake yapo duniani kote leo hii, na hakuna anayetilia mashaka juu ya uwezo wake katika jambo lolote.
Huwezi kusema, haya yote aliyaokoteza harakaharaka katika miaka mitano baada ya kufungua nchi yake.
Mkuu acha kauli za jumla jumla, binafsi nimewahi fanya tafiti nikagundua kuna huduma nyingi tu za kiafya tulikua tunazifuata India na kwingineko ila kwa sasa zinafanyika bongo tena hospitali za serikali na tukaestimate gharama iliyookolewa na tukakuta Mabilion yameokolewa ila nyie hamuoni hayo mnaangalia tu gap ilipo. Hata makampuni ya ndege kuna pilots weusi wengi kuliko miaka 20 nyuma so tusijilimit kwamba kuna sekta hatuwezi tap technical know-hows etc.EeeenHeeee!
"Na sisi tukiweza kutap teknologia wanazokuja nazo..." China na Tanzania, vitu mbalimbali kabisa, mkuu wangu Zitto Jr..
Kulikuwa na takwa la uwepo wa kuwafundisha waTanzania kupata uwezo/uzoefu kwa makampuni yanayowekeza, na ilikuwa kumewekwa kiasi cha mwekezaji anachotakiwa kuleta watu wake..., hili limelegezwa kwa jina la kuvutia uwekezaji. Na muda wa hao wageni wanaoajiriwa ulikuwa na kikomo kabla ya kumpata mTanzania kushika nafasi, hilo nalo limelegezwa au halipo kabisa.
Najua unaelewa ninachokisema hapa.
Kwa hali hii ya uvutiaji wa uwekezaji, huwezi kamwe kusema utajenga uwezo wa wananchi wako 'kutakeover' majukumu na kujenga uwezo wa wananchi wako. It's just a joke!
Kuna sovereign wealth fund imefunguliwa so gesi ya Mtwara kwa inayouzwa mapato yataenda kwenye huo Mfuko ambao unainvest in multiple projects nje na ndani ya nchi.Tuambie mapato yanayopatikana kwenye gas Mtwara umefaidika na nini mpaka sasa???
Ziara ya mheshimiwa rais huko Oman ameongozana na January Makamba waziri wa nishati, waziri atumie wasaa huu kuangalia suala la gesi asilia LNG Oman wamefanikiwa vipi nasi tuige