Waziri wa nishati vs DG? . Hapa sasa ni kama tutakuwa tunapoteza muda kujadili hiliDG wa TPDC kasema tuna wataalamu kwenye eneo la gesi hasa kwenye upstream wapi nimemquote January? In fact yeye kaongelea eneo la sheria that's all so mie nimestick na alichosema Bwana Mataragio maana ndio yupo ground.
Hakukuwa na sheria mahususi by then mpaka 2015 in fact regulations zimetungwa 2018 kipindi Cha JPM ila mpka anafariki hakuna mkataba uliopelekwa bungeni kinyume kabisa na sheria hii. Pia ripoti za ukaguzi za TEITI zilipaswa ziwekwe bungeni ila serikali haikuwahi kuziweka wazi kinyume kabisa na sheria Wala regulations za utekelezaji wa sheria hiyo!!Ukisikia maajabu ndio haya sasa Tanzania imekubaliana na EITI(TEITI) tokea 2009, we unaleta story za 2015
Baada ya Tz kuingia EITI hiyo 2009 ni mkataba gani uliwahi kuwekwa wazi?
Unaona SasaHakukuwa na sheria mahususi by then mpaka 2015 in fact regulations zimetungwa 2018 kipindi Cha JPM ila mpka anafariki hakuna mkataba uliopelekwa bungeni kinyume kabisa na sheria hii. Pia ripoti za ukaguzi za TEITI zilipaswa ziwekwe bungeni ila serikali haikuwahi kuziweka wazi kinyume kabisa na sheria Wala regulations za utekelezaji wa sheria hiyo!!
Tusihamishe mjadala, topic inahusu gesi watu wamedai mikataba ya gesi ndio hayo madai yapo chini ya TEITI Act ya 2015. Sasa issue ni kwamba maadam aliyetunga kanuni za sheria hiyo hakuheshimu sheria hiyo then ni makosa kumlaumu mama Samia kutoweka mikataba wazi.Unaona Sasa
Hivi ili kupeleka mkataba bungeni na kuwa wazi Ni lazima uwe umejiunga EITI?
Kenya, South Africa, US ni moja ya nchi ambazo hazipo EITI, je nao mikataba haipo wazi na haipelekwi bungeni?
Vipi kwa mikataba ambayo haihusu natural resources? Mbona nayo haipelekwi bungeni kujadiliwa kwa miaka yote?
Tuliwahi kuingia mikataba mingi kwenye reli, shirika la ndege n.k mbona nayo haikupelekwa bungeni?
Au unafikiri tatizo la mikataba kutopelekwa bungeni ni kwenye issues za natural resources tu?
Nimehamishaje mnadala? Nimekuonyesha kuwa suala la mikataba kuwa wazi na kupelekwa bungeni wala halihusiani na kuwa EITI kwa kuwa hata kwenye mambo mengine ambayo sio ya natural resources bado mikataba haiendi bungeni Wala kuwa waziTusihamishe mjadala, topic inahusu gesi watu wamedai mikataba ya gesi ndio hayo madai yapo chini ya TEITI Act ya 2015. Sasa issue ni kwamba maadam aliyetunga kanuni za sheria hiyo hakuheshimu sheria hiyo then ni makosa kumlaumu mama Samia kutoweka mikataba wazi.
Hoja Iko hapo, hayo ya US na SA hayaingii hapa maana mifumo Yao ya serikali za majimbo ni tofauti na huku ndio maana kuna states zinaruhusu bangi zingine hapana, each state negotiates for itself which is not the case in Tanzania.
Mkuu french, naendelea kusisitiza, as long as hakuna yeyote alitupa details za ni nini kilichosainiwa, then hoja za bandiko langu hili, Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe! still stands.LNG lazima ijengwe onshore. Kuna pipes zitatoka bahari kuu sehemu vilivyopo visima mpaka kwenye mtambo wa lng ambao upo onshore. Hapo ni umbali kama wa km 200 hivi. Kwenye huu mtambo sasa gesi itabadilishwa kutoka kwenye mvuke na kuwa kimininika. Hii ndio maana halisi ya LNG yaani Liquified Natural Gas (LNG). Ukitaka kujenga offhore unaweza pia, ila itaitwa FLNG kwa maana ya FLOATING LIQUIFIED NATURAL GAS. Hii FLNG ni meli special zinajengwa na kuelea sehem ya visima vya gesi na kufanya kazi ya kubadilisha gesi kuwa kimiminika
Kwanza ni $40B sio $30B 👇11 Juni 2022
Dar es Salaam, Tanzania
Serikali ya Tanzania yasaini mradi wa thamani ya dola za Kimarekani 30 bilioni na mashirika makubwa ya Equinor la Norway na Shell la Uingereza kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi asilia yaani LNG (Liquified natural gas) ambao umeshuhudia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo jumamosi tarehe 11 June 2022.
Mradi huo wa kuchakata gesi upo baharini katika kina kirefu mkoani Lindi wenye thamani ya shilingi za kitanzania trilioni 70 (dola za Kimarekani 30 bilioni).
Ujenzi wa mradi huu utatoa ajira ya wafanyakazi 7,000 katika kujenga miundombinu pia mtambo wa kuchakata na utachukua miaka 7 kukamilisha ujenzi wake.
Mradi huu ni wa aina yake unaotaka ujuzi wa hali ya juu kuukamilisha hivyo utajumuisha wataalamu wa ndani na nje kuhakikisha unakamilika kwa wakati na unategemewa kubadilisha kabisa uchumi wa mkoa huu wa kusini mwa Tanzania pia uchumi wa wakaazi wa eneo hili la Tanzania.
RAIS SAMIA AFICHUA MRADI ULIVYOMSHINDA AKIWA MAKAMU WA RAIS - "MAMBO YALIKUA MENGI"
Rais Samia ameshuhudia utiaji saini makubaliano ya awali ya mkataba wa nchi hodhi (HGA) wa mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia.
DAR ES SALAAM, June 11, 2022
Tanzania signs gas project deal with Equinor and Shell
- Tanzania's government, Norway's Equinor and Britain's Shell signed a framework agreement on Saturday that will bring them closer to starting construction of a $30 billion liquefied natural gas (LNG) project, live video from the event broadcast on state TV showed.
Hujui chochote kuhusu miradi ya mafuta na gesi.
Hilo ndiyo tatizo , wataalamu wapo , Ila tatizo ni uzembevwa serikali on how Ku utilize hao watu , tumeendekeza siasa Tu , utaalamu umetupwa KuleWewe umeshuka toka sayari gani, au ulikuwa kwenye pango gani ambako hukujua historia ya nchi hii hadi hapa tulipofikia leo?
Accacia alipokuwa anazoa mali hapa hao wataalam unaowasema walikuwa wapi, kama hawakuwa sehemu ya uhujumu?
Ndiyo, wataalam wapo, tena wengi sana katika kila nyanja unayoweza kuifikiria ndani ya nchi hii, lakini hawatumiki ipasavyo, na mbaya zaidi wengi wao wamekuwa ni sehemu ya matatizo ya nchi yetu, kwa sababu wanashiriki kuihujumu na hao wanasiasa wa CCM.
Tunakosa uongozi wa kuwatumia vizuri wataalam hawa wafanye kazi na kutumia elimu yao kwa manufaa ya taifa letu.
Na hili haswa ndio la muhimu , we need technology transfer apart from monetary benefits , huwezi kujenga uwezo WA nchi kiteknolojia kama hauinvest kwa wasomi WA nchi yako. Na hili linafanyika Kwa agreement Kati ya muwekezaji na serikali , Ile proportionality ya wafanyakazi WA kigeni na wazawa ni muhimu Sana kuzingatiwa . Watu wapate nafasi za kazi humo , tena positions nyeti za teknologia na usimamizi ili wapate ujuzi ambao utalinufaisha taifa hata mradi ukiisha , WaAfrica tubadilike , si watu wetu kuajiriwa kama makuli nk halafu hamna technology transfer , that's dumbEeeenHeeee!
"Na sisi tukiweza kutap teknologia wanazokuja nazo..." China na Tanzania, vitu mbalimbali kabisa, mkuu wangu Zitto Jr..
Kulikuwa na takwa la uwepo wa kuwafundisha waTanzania kupata uwezo/uzoefu kwa makampuni yanayowekeza, na ilikuwa kumewekwa kiasi cha mwekezaji anachotakiwa kuleta watu wake..., hili limelegezwa kwa jina la kuvutia uwekezaji. Na muda wa hao wageni wanaoajiriwa ulikuwa na kikomo kabla ya kumpata mTanzania kushika nafasi, hilo nalo limelegezwa au halipo kabisa.
Najua unaelewa ninachokisema hapa.
Kwa hali hii ya uvutiaji wa uwekezaji, huwezi kamwe kusema utajenga uwezo wa wananchi wako 'kutakeover' majukumu na kujenga uwezo wa wananchi wako. It's just a joke!
The guy was a real bumKwenye suala la uvunaji gas, ni kati ya makosa makubwa ya ajabu aliyoyafanya Magufuli. Leo hii Tanzania isingekuwa inafukuzana na vikodi vya kwenye Mpesa.
Mapato ambayo yangepatikana kwenye mradi wa gas, yakilinganishwa na dhahabu, yangekuwa sawa na kulinganisha bahari (gas) na tone (dhahabu) la maji.
Lakini Kivuruge aliharibu, wawekezaji wakaondoka, alipogundua kuwa ameharibu akaanza kuwasihi kwa siri warudi, wakagoma. Walipogoma akaanza kuongea uwongo eti gas ya Tanzania imeuzwa kwa wachina? Wajinga, bila hata ya kujiuliza imeuzwa kwa namna gani, wakamwamini.
Leo ni kama tunaanza upya,wakati tulikuwa tumekaribia hatua ya uzalishaji.
Hapo ndiyo unaona jinsi mtu mmoja anavyoweza kuleta madhara makubwa
Acha ujuaji na ubishi WA kipuuz ,Hivi huelewi kwamba hata Marekani enzi za akina Washgton nchi ilikuwa ni maskini?
Hapo Ulaya kuna nchi ngapi zilizokuwa na uchumi mzuri nyakati za akina Mao?
Hili nalo unataka uwe mjadala wa kuhalalisha upepari kuwa ndiyo njia pekee ya kuleta mabadiliko katika maisha ya watu?
"Reverse Engineering", nani hakufanya reverse engineering hata leo hii!
Zitaje hizo nchi za kijamaa zenye uchumi mkubwa kuliko nchi za kibepari , msiwe mnaandika vitu kama mazwazwa , unajua hata maana ya ubepari na ujamaa ?Ubepari sio utajiri wa uchumi mkubwa, uchumi mkubwa ni brain
Kuna nchi nyingi tu zina mfumo wa kibepari ila zimezidiwa uchumi na nchi za kijamaa