Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Nina uhakika bila Ujio wake Kaka wa Twita ambao umekuwa ni wa Tija zaidi Kwetu Kitaarifa ( tena zile Nyeti kabisa ) pamoja na Yule Dada wa Instagram Mabadiliko haya ' Kandamizi ' ya Vifurushi vya Simu yasingefanyika.

Vifurushi vyote mmebadilisha, vile vya Chuo ( University Offer ) mmeondoa vyote ( hasa Airtel ) na Kupandisha Gharama maradufu ili Kutukomoa Wanyonge ( Masikini ) akina All - Rounder and the likes nchini.

Najua wapo Wapumbavu na Wanafiki watakaofurahia ila nina uhakika Wao na hasa hasa haya Makampuni ya Simu hayakuangalia kwa umakini Madhara makubwa Kwao Kibiashara ( Kimapato ) na wameogopa Kusimama imara kwa Serikali na Kukubaliana Kwao kutumaliza Sisi Wateja wao kama hivi.

Hatua hii itapelekea Watanzania wengi Wanyonge ( Masikini ) kuacha hata Kutumia Simu hali itakayoshusha Mapato kwa Kampuni husika na hatimaye katika Kujilinda Sokoni nao wakaamua Kupunguza Wafanyakazi hivyo kupelekea hali kuwa mbaya zaidi.

Ni Serikali isiyojielewa tu popote duniani inaweza kutumia Nguvu nyingi Kupambana na Adui yao Mmoja kwa Gharama za Kuwatesa ( Kuwaumiza ) walio wengi ambao ni Wanyonge wakijidanganya kuwa hapo wanamuweza na watatuweza hadi Sisi Wafuasi ( Followers ) wake.

Hivi Serikali husika ingekuwa inafanya ( inatenda ) mema na kwa haki huyo Adui yenu wa Twita ( Kaka ) na Yule mwingine wa Instagram ( Dada ) wangeweza Kuibuka na Kuwaumbueni na Uongozi wenu wa hovyo hovyo uliojaa Hila nyingi kiasi kwamba hadi wengine Mwenyezi Mungu kaamua Kuwatwaa ghafla ili Watanzania tuliobaki tuendelee kuwa na Amani na Furaha?

Halafu mlivyo Majuha ( Wapumbavu ) mmesahau kuwa ' Tozo Kandamizi ' na ' Tozo Komoa ' hizi mlizokuja nazo zitapunguza sana tu pia Mapato yenu kama Serikali na hatimaye mtarudi tena kule kule kuomba Misaada kwa Wakubwa akina WB, IMF, Uingereza, Marekani, Sweden, Ufaransa, Norway, China na Finland bila kusahau na zile nchi zilizopo Arab League pamoja na Waafrika Wenzetu waliotuacha Kimaendeleo Kitambo Egypt na South Africa.

Aliyewaambieni kuwa Watanzania wote watumiaji Mitandao huwa wako 24/7 kuwasoma tu hao Maadui zenu Kaka wa Twita na Dada wa Instagram pekee ni nani? Wengine kuwepo tu mfano hapa Mtandaoni JamiiForums kumetusaidia Kuongeza Maarifa yetu, Ufahamu mkubwa lakini pia tunapata Faraja ya Akili na Afya ya Moyo kwa burudani za Kimawazo ( Kiuwasilishaji ) za hapa Jamvini.

Wengine uwepo wa hii Mitandao ilisaudia tutulie na tuachane na Mawazo ya Kukaba Watu, Kubaka hovyo, Kupiga Punyeto hadi Mikono pamoja na Vidole Kuvimba, Kukaa Vijiweni na Kunywa sana Gongo bila kusahau Kuvuta Udi Karaha ( Bangi ) hivyo basi huenda kwa hatua yenu hii ya Kipumbavu na iliyojaa Chuki na Ukatili Kwetu Watanzania wengi basi tukaanza Kurejea katika Uovu tuliouacha Siku nyingi tu.

Msiponiona tena hapa JF jueni nami All - Rounder ni Mhanga Mwandamizi ( Mkomavu ) wa hatua hii hivyo kutokana na Ufukara wangu mkubwa sina uhakika kama nitaviweza hivi Vifurushi vipya vya Waziri Faustine Ndugulile.

Na wale Matajiri wa Kununua Vocha na Kuweka Mabando ya kutosha nawatakieni tu kila la kheri. Nimesikitika na Kuumia mno ila hukumu Kamili kwa Waziri Ndugulile na Makampuni yote ya Simu yaliyokubaliana nae pamoja na Yule aliyeshika Usukani sasa wa Kikatiba Serikalini namuachia Mola ( Maulana ) na najua atanijibia na atatujibia tu kama ambavyo alitujibia pia ghafla Wiki chache zilizopita.
 
Nchi zingine walifaulu Je ?!. Sisi hata katiba tu tumeshindwa.

Hizi serikali za weusi mpaka pressure. Bila hivyo hamna kitu.

Odhis *
Sisi hatupo tayari kuhatarisha maisha yetu ila naiona siku ambayo kizazi chenye nyongo kali kikipandisha vurugu itayotokea ndio utakuwa mwisho wa Tanzania dhalimu inayoitwa Tanzania ya Amani.

Nchi hii wanaonufaika ni kundi dogo ambalo liko kwenye nafasi za utawala. Hii hali itafikia siku itachokwa sababu kuna watu hawana la kupoteza.

Hio ndio itakuwa siku ya ukombozi.
 
Wakuu,

Kama kweli tunaamini katika uhuru wa mawazo kama haki ya kikatiba, na kama kweli tunaamini katika uwajibikaji wa viongozi, basi naomba huyu waziri Ndugulile asome ninayoandika kama jinsi yalivyo.

Wewe waziri Ndugulile, waziri mwenye dhamana kwa niaba ya serikali; una akili timamu!?

Nauliza swali? Unazo zilizotimia?

Hivi, zile mbwembwe zote za kujigamba na kujitutumua kwamba mtahakikisha vifurushi vinakuwa vya bei nafuu, ndio matokeo yake haya tunayoyaona hapa?

Yaani wewe waziri, unaweza kuwafanya watanzania milioni zaidi ya sitini kuwa ni wapumbavu na mbumbumbu?

Ukakimbia kwenda kujitungia kanuni haramu na za kitapeli ili kuhalalisha wizi?

Ulisikia wapi dunia ya leo, data zinakuwa ghali namna hii?

Katika nyakati za utandawazi ambapo maisha yote yanategemea digital devices, kwanini ufanye uhuni wa namna hii?

Sifahamu lengo ni nini? ama ni mbinu za kubinya watu wasipate access ya mtandao?

Ndugulile, nikueleze tu kwamba, maisha ya watanzania wengi hayazunguki kwenye muhimili wa siasa pekee.

Kama lengo ni kuwabinya watu kisiasa, basi hilo ni lengo mfu lisilo na uhalisia.

Mitandao ndio maisha yetu, ndio chakula chetu na kipato chetu. Tusivurugane.

Tunahitaji vifurushi vishuke bei. TAFADHALI.
Alichotufabyia yatosha atoswe Leo kutoka 2000 1 GB kwenda 2000 400 MB Mia 6 MB zimeenda nabndungulile

Screenshot_20210402-090531.png
 
Sidhani kama Ndugulile ana kosa, yeye ni mtekelezaji tu kama wengine muhimu tupambane mitandao ya simu ipunguziwe kodi vifurushi vitashuka automatically. Mitandao ya simu inatozwa kodi kubwa sana ambayo inasababisha gharama kupanda na kuumiza watumiaji wake. Ndugu yangu unafikiri 2T aliyoitamka jana Dr Mpango itapatikana kwa miujiza, matunda ya hiyo 2T ndiyo haya...
Ndugulile ni middle man between us na kwa upande mwingine kuna mitandao ya simu , Huyu ni mwakilishi wa serikali , hana ujanja wa kukwepa lawama , ili awe huru ajiuzulu haraka
 
Mimi hufatilia masomo na kujifunza huko YouTube Sasa kuongeza gharama Mara dufu ni zaidi ya ychawi, mama Samia aangalie hii Hali, Kama ile ya kwenye makodi Hadi watu wakafunga biashara ndio wakaja kugutuka
Kwa kweli tuanzishe uzi wa kumchuria yule jamaa aliotuponza. Dr. RELATIVE out pls!!!
 
Naanzisha rasmi kampeni ya kuhakikisha tunapata Waziri mpya wa Teknolojia baada ya huyu aliyepo kushindwa kwa makusudi kudhibiti bei ya vifurushi mitandaoni .

View attachment 1741015

Ewe mwananchi ni jukumu lako tena la haki kuhakikisha viongozi wabovu wanang'oka kwa namna yoyote ile ili nchi yetu isonge mbele , Madaraka ni kama mbio za kupokezana vijiti , Ndugulile ameshindwa kuwasaidia wananchi hivyo ni vema akang'oka ama akang'olewa .

Mungu ibariki Tanzania .

Tutakuwa tunamuonea tu,hili lipo nje ya uwezo wake,usidhani wenye kampuni za simu waliamka tu asubuhi na kupandisha bei.....lazima kuna kibano kwenye kodi wamepewa hivyo wana shift burden kwetu walaji...

Angalia issue ya cement,ilianza mdogo mdogo kwa kuadimika na bei kupanda na sasa nadhani unaona bei ya cement huko uliko na tumeanza kuizoea,hata vifurushi tutavizoea.
 
Akifukuzwa we unafaidika nini?
Najuta kuwa Mwafrika, Hivi kabisa mtu unakaa kushangilia mwingine afukuzwe kazi kisa umeshindwa kujaza bando??
Aisee 🤦‍♂️
 
Dawa yao ni tuchague mtandao mmoja,tununue laini zake, tu-divert namba zetu pendwa kwenda kwenye namba zetu mpya ili tusikose mawasiliano ya muhimu. Kisha tuzime laini za mitandao mingine.

Tuwaoneshe kuwa ni sisi ndio wenye maamuzi, na sio wao.

** Kama una wazo bora zaidi ya hili ruksa kuleta**
 
Alisema MB moja itauzwa kwa sh 3 hadi 5
Hatukumuelewa [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Tsh 10,000/= GB 3

Ukichukua Tsh 10,000 ÷ 3000 MB
Unapata Tsh 3.33 per MB
... hili alitamka tu lakini sijui kama alikuwa anajua anachokiongea. Ni vigumu sana kuelewa mambo kama utakuwa na nafasi kubwa halafu huna maamuzi maana enzi ya shujaa kila kitu kilikuwa kinatoka kwake.
 
Nadhani ulikua mpango wa muda mrefu wa mfalme kuzima ukosoaji! Maana vijana wangapi au viongozi wangapi ni wabobevu wa TEHAMA walishindwa kuwekwa kwenye hiyo wizara ?

Hadi kumuweka Daktari ambaye Serikali/ Wazazi walipoteza Rasilimali kumtengeneza halafu anakuja kusimamia vitu asivyojua ABC zake huku Hospitali kukiwa na uhaba hadi watu wanaambiwa hawaruhusiwi kuhudumu Hospitali binafsi na Serikalini! Naona Huyu Faustine ni wakati wa kuvaa stethoscope na kurudi wodini...
 
Back
Top Bottom