Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Naanzisha rasmi kampeni ya kuhakikisha tunapata Waziri mpya wa Teknolojia baada ya huyu aliyepo kushindwa kwa makusudi kudhibiti bei ya vifurushi mitandaoni .

View attachment 1741015

Ewe mwananchi ni jukumu lako tena la haki kuhakikisha viongozi wabovu wanang'oka kwa namna yoyote ile ili nchi yetu isonge mbele , Madaraka ni kama mbio za kupokezana vijiti , Ndugulile ameshindwa kuwasaidia wananchi hivyo ni vema akang'oka ama akang'olewa .

Mungu ibariki Tanzania .
Afukuzwe tu maana hafai kabisa
 
Hii ni ishara tosha hata mikataba wanayo tusainia nchi za nje huwa tunapigwa yote, kama mkataba na kampuni za ndani zinawaingiza chaka na Je za mabeberu wataweza.

Pengo la kukosa upinzani bungeni ndo linatumiza zaidi sbb nileteeeni Gwajimaaaaa
Hatari sn
 
Wakuu,

Kama kweli tunaamini katika uhuru wa mawazo kama haki ya kikatiba, na kama kweli tunaamini katika uwajibikaji wa viongozi, basi naomba huyu waziri Ndugulile asome ninayoandika kama jinsi yalivyo.

Wewe waziri Ndugulile, waziri mwenye dhamana kwa niaba ya serikali; una akili timamu!?

Nauliza swali? Unazo zilizotimia?

Hivi, zile mbwembwe zote za kujigamba na kujitutumua kwamba mtahakikisha vifurushi vinakuwa vya bei nafuu, ndio matokeo yake haya tunayoyaona hapa?

Yaani wewe waziri, unaweza kuwafanya watanzania milioni zaidi ya sitini kuwa ni wapumbavu na mbumbumbu?

Ukakimbia kwenda kujitungia kanuni haramu na za kitapeli ili kuhalalisha wizi?

Ulisikia wapi dunia ya leo, data zinakuwa ghali namna hii?

Katika nyakati za utandawazi ambapo maisha yote yanategemea digital devices, kwanini ufanye uhuni wa namna hii?

Sifahamu lengo ni nini? ama ni mbinu za kubinya watu wasipate access ya mtandao?

Ndugulile, nikueleze tu kwamba, maisha ya watanzania wengi hayazunguki kwenye muhimili wa siasa pekee.

Kama lengo ni kuwabinya watu kisiasa, basi hilo ni lengo mfu lisilo na uhalisia.

Mitandao ndio maisha yetu, ndio chakula chetu na kipato chetu. Tusivurugane.

Tunahitaji vifurushi vishuke bei. TAFADHALI.
Usiweke maneno mengi leta takwimu za bei kwa nchi zinazotuzunguka,usilalamike tu
 
Sidhani kama Ndugulile ana kosa, yeye ni mtekelezaji tu kama wengine muhimu tupambane mitandao ya simu ipunguziwe kodi vifurushi vitashuka automatically. Mitandao ya simu inatozwa kodi kubwa sana ambayo inasababisha gharama kupanda na kuumiza watumiaji wake. Ndugu yangu unafikiri 2T aliyoitamka jana Dr Mpango itapatikana kwa miujiza, matunda ya hiyo 2T ndiyo haya...
Hata huyu mpango hafai aisee na bado anasisitiza trillion mbili bila kuangalia Hali halisi yeye akiwa waziri wa fedha kaua uchumi aisee, kwani enzi za kikwete yeye alikuwa anafanyaje maana hawa wazee wa task force kutumia nguvu kwenye kukusanya Kodi bila mazingira halisi kumeua uchumi na maelfu ya biashara kufungwa
 
Uyu waziri Hamna kitu kabisa.alichoongea na kinachotokea tofauti kabisa.aje atuambie kwanini amutudanganya.
Ni bora angewaacha watuibie.
 
Hongera Mimi nilikuwa natumia Airtel ya chuo wamefuta hyo Sasa gb 1 elfu tatu loh, awamu ya wanyonge si mchezo hela hamna ila kila kitu kinapandishwa juu
Ndio kulimia meno kwenyewe huku.

Lakini wamasemaga katika nchi zote za EAC tz pekee ndio yenye bei rahisi za vifurushi
 
Lawama zote abebeshwe hayati magufuli, yeye alishasema anatamani malaika ashuke afunge mitandao, wakumlaumu ni hayati ,na kundi lake humu na serikalini waliokuwa wanamuabudu, Yaan yule mzee miaka mitano ijayo kama angeendelea kuwepo, kwa hakika nimeamini maji tungeita "MMA

Ndiyo maana Mola akatuepusha nae tu.
 
Nadhani ulikua mpango wa muda mrefu wa mfalme kuzima ukosoaji! Maana vijana wangapi au viongozi wangapi ni wabobevu wa TEHAMA walishindwa kuwekwa kwenye hiyo wizara ?

Hadi kumuweka Daktari ambaye Serikali/ Wazazi walipoteza Rasilimali kumtengeneza halafu anakuja kusimamia vitu asivyojua ABC zake huku Hospitali kukiwa na uhaba hadi watu wanaambiwa hawaruhusiwi kuhudumu Hospitali binafsi na Serikalini! Naona Huyu Faustine ni wakati wa kuvaa stethoscope na kurudi wodini...
Mwendazake mwenyewe hayupo duniani katuachia msala sisi aisee, hawa viingozi wawe wanafikiria na sisi raia aisee
 
Rest in peace night bando halotel wameondoa aiseee zile muvi sijui Nita download vipi ?!
 
Watapoona mapato kutoka makampuni ya simu yameshuka, waturudi kurekebisha hizi bei bila kuombwa ingawa watatumia kisingizio cha serikali sikivu.
Nalijua hilo,ila mpaka ifikie hatua hiyo baadhi ya vijana watakuwa wamejua nafasi yao katika jamii.
 
Naomba huu uzi uwe maalumu kwa ajili ya kuhamasisha kila mdau na kila mwenye mapenzi mema kususia huu uharamia wa ndugulile na waliomtuma.

Sisi ndio walaji wa vifurushi. Tunaweza kuamua kununua, kususa au kuacha.

Sisi ndio tunaoshikilia roho ya haya makampuni uchwara yanayoendeshwa kihuni na kienyeji kwa siasa za kubangaiza bangaiza.

Tukiamua kususia haya makampuni kwa wiki japo mbili tu, wanaweza kupata hasara isiyoweza kulipika wala kurudishwa.

Natoa wito kwa kila mmoja, kwa mitandao yote ya kijamii na kwa vyombo vyote vya habari kuhamasisha kususia haya makampuni kwa muda endelevu mpaka pale watakapotambua thamani ya kuwa na nidhamu ya biashara.

Hii kampeni ya kususia haya makampuni ifanywe kwa nguvu zote kila kona ya nchi hii kwa muda endelevu usiojulikana ukomo wake.

Sisi ndio walaji. Wasitubabaishe.

Lazima tuelezane ukweli kwamba, wewe ndugulile ni mtu mwovu.

Unapenyeza mikakati miovu na conspiracy za kuzima sauti za watu kupitia mgongo wa mitandao.

Hatuwezi kuwa watumwa wa conspiracies. We are free people in a free country.

Tuwajibishane.
 
Leo tarehe 1/4/2021 makampuni ya simu yamefanya mabadiliko makubwa katika vifurushi vyao.

Wamepunguza vifurushi kwa kiasi kikubwa hasa vifurushi vya data, sitaweka hapa kifurushi kimoja baada ya kingine lkn kwenye mitandao yetu hilo lipo.

Nenda kwenye menu tu nadhani utakutana na upuuzi wote.

Nini nataka kusema?

Wakati dunia inakimbia kwa kasi kwenye technolojia sisi tunajirudisha nyuma tena kwa kasi kubwa na wala hapa siyalaumu haya makampuni ya simu kwani yenyewe yanapokea tu order toka Serikalini.

Kama wananchi wa kawaida kabisa tunaiomba Serikali iweze badilisha hiv vifurushi haraka sana maana wanachokifanya ni kurudisha juhudi za maendeleo ya kisayansi nyuma.

Na kwa vile tuna Serikali mpya nina hakika watashughulikia hili haraka sana na wala hawatasubiri hadi mwezi upite maana kilichofanyika ni zaidi ya upuuzi wa hali ya juu.

Kama Serikali itashindwa rekebisha hili basi tutajua hamna mpango na wananchi wa kawaida na mengi mnayoyaongea ni porojo tu

Naomba kuwasilisha.
Si mnakataa kwamba nyie siyo wanyonge sasa mwalalamika!!
 
Ni ngumu kususa!

Lakini si mnasema SERIKALI ipo kusaidia wananchi wake!

Mitano tena
 
Back
Top Bottom