Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

meli ishang'oa nanga, haiwezi kurudi kwenye gati kupakia wachelewaji

nchi za wenzetu ishu kama hii iliyodokezwa mapema sana ili kupima upepo nchi zima wangeshapinga na kulaani na wasingethubutu
 
Chonde chonde serikali rudisheni bei za awali za vifurushi maana viliendana na kipato cha watanzania walio wengi kwa mfano halotel kwa shilingi 1000/= watu walijipatia GB1 na dakika 10 kupiga halotel-halotel kwa wiki moja sasa imebadilika shilingi 1000 ni Mb 420 na dakika 15 kwa wiki kweli watanzania watumudu gharama hizi kwa kipato chao hiki cha milo miwili kwa siku?wanafunzi wa vyuo wategemea boom watamudu gharama hizi kweli za vifurushi? Wenye internet cafe je? Vijana ambao wamejiajiri kutumia internet watamudu gharama hizi?

Serikali za mataifa mengine ziko bize kuhakikisha gharama za maisha za wananchi wao zinakuwa katika hali nzuri yaani ya chini ili kila mwananchi afaidike na huduma mbalimbali zenye ubora mfano Obama care. Nyie mko bize kuwaza kupandisha gharama za maisha za wananchi ili mfaidike nyie na familia zenu maana posho na mishahara mnajilipa vizuri haishuki inapanda kila uchwao alafu ndo mnajikuta wazalendo nambari moja wakati posho na mishahara mnalipwa na watanzania wavuja jasho mlio wapa jina Wanyonge badala ya kumfanya atoke kwenye unyonge nyie mnafanya kila njia awe mnyonge zaidi hopeless kabisa viongozi wa taifa hili.

Angalieni upya basi maamuzi yenu au ndo njia ya kutaka watu wasiwe wanaingia kwenye social media ambazo ndo zimekuwa kimbilio baada ya kufa kwa uhuru wa habari nchini?

Serikali mkikaa kimya na kushindwa kutatua changamoto hii kama mlivyo feli kwenye sukari na mafuta ni dhahiri kwamba tunaongozwa na watu wenye kutetea matumbo yao na sio watanzania.
 
Tumeamua kuminya like mnachokiita uhuru wa habari indirectly. Bora iwe hivi Ili vijana wafanye kazi, maana vitoto vilikuwa vikimliki tu itel vunakuwa vinaweka bando la buku, afu vinakuja kusumbua humu, na kutukana hovyo.Bora mitandao iwe ni kwaajili ya vibopa,maana huwa tunajielewa sana.

Asante sana serikali ya awamu ya sita😅.
 
Leo tarehe 1/4/2021 makampuni ya simu yamefanya mabadiliko makubwa katika vifurushi vyao.

Wamepunguza vifurushi kwa kiasi kikubwa hasa vifurushi vya data, sitaweka hapa kifurushi kimoja baada ya kingine lkn kwenye mitandao yetu hilo lipo.

Nenda kwenye menu tu nadhani utakutana na upuuzi wote

Nini nataka kusema?
Wakati dunia inakimbia kwa kasi kwenye technolojia sisi tunajirudisha nyuma tena kwa kasi kubwa na wala hapa siyalaumu haya makampuni ya simu kwani yenyewe yanapokea tu order toka Serikalini.

Kama wananchi wa kawaida kabisa tunaiomba Serikali iweze badilisha hiv vifurushi haraka sana maana wanachokifanya ni kurudisha juhudi za maendeleo ya kisayansi nyuma.

Na kwa vile tuna Serikali mpya nina hakika watashughulikia hili haraka sana na wala hawatasubiri hadi mwezi upite maana kilichofanyika ni zaidi ya upuuzi wa hali ya juu.

Kama Serikali itashindwa rekebisha hili basi tutajua hamna mpango na wananchi wa kawaida na mengi mnayoyaongea ni porojo tu

Naomba kuwasilisha.
Bora limeenda.
 
Wananzengo nadhani tumeona mabadiliko ya vifurushi vya mitandao,jamaa wamefanya mabadiliko ya kufa mtu,huku uswahilini tunasema wameua sisimizi kwa nyundo,sidhani kama kuna mnyonge anaweza kununua mb400 kwa tsh 2000,
Kwa zaidi ya miaka miwili nimekuwa nikitumia T-Connect Plus ya ATCL ambayo ni 10K for 10GB kwa wiki! Leo hii wameshusha kutoka 10GB hadi 4.5GB!!
 
Kila ulimi utakiri mbele ya CCM
Ikiwezekana GB 1 inunuliwe kwa sh 10K, Ili mitandaoni tubaki watu tunaojielewa. Maana vijana waliacha kufanya kazi kabisa, kijana wa BAVICHA akimiliki itel alafu akaweka bundle la 1000,ilikuwa ni kero sana maana wanachojua ni matusi tu na kufatilia umbea mitandaoni.
 
Sio kila anayeshinda mtandaoni anapiga umbea na udaku, wengine ndo eneo letu la kazi
Basi endelea kuoperate kulingana na kiwango chako cha mtaji, na ulipe kodi. Na kama hauna uwezo wa kumudu hizi gharama za vifurushi,nikushauri toka Sasa Jf ukatafute hela.
 
wapenda movies ndio tunaumia zaidi
Mkuu usiseme wapenda movies tu,Mimi mwezi Wa tano nilitegemea kuanza masomo Yangu kwa njia ya mtandao ambapo kuna conference inafanywa kupitia zoom,ni takribani saa moja na zaidi,unadhani kwa GB 1.333 kwa shilingi 2000,itanibidi niwe na shilingi ngapi ndo niweze kufanya shughuli hii? Hii ni hatari sana .

Nakumbuka ndugai akiwa bungeni aliwahi kulaumu vijana kushinda mitandaoni bila kufanya kazi akawa anawaza namna ya kuwafanya watu wafanye kazi nasi kushinda mitandaoni,nadhani haya ndo majibu kwa hoja ya ndugai.

Hatari sana ,wanaoumia haoa so wakosoaji waserikali pekee Bali ni wananchi wote,Mungu aingilie kati
 
Ikiwezekana GB 1 inunuliwe kwa sh 10K, Ili mitandaoni tubaki watu tunaojielewa. Maana vijana waliacha kufanya kazi kabisa, kijana wa BAVICHA akimiliki itel alafu akaweka bundle la 1000,ilikuwa ni kero sana maana wanachojua ni matusi tu na kufatilia umbea mitandaoni.
Watapoona mapato kutoka makampuni ya simu yameshuka, waturudi kurekebisha hizi bei bila kuombwa ingawa watatumia kisingizio cha serikali sikivu.
 
[emoji16][emoji16]
IMG-20210402-WA0044.jpg
 
Unajielewa wewe zwazwa!
Kama huna hela ya kumudu hizi gharama ndogo za vifurushi, toka Sasa Jf uende ukafanye vibarua mitaani upate hela.Hilo ndo Taifa tunalotaka,lisilo kuwa na vijana wanaoshinda mitandaoni kutafuta umbea.

Au mwambie KOGOGO akununulie bando😅.
 
Back
Top Bottom