Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Mchakato ulikuwepo lakini hawakuthubutu kuchukua hatua ya ghafla ya kupandisha gharama kiasi hiki.Kwa kifupi ni kama walikuwa wanasubiri mwendazake apite na sasa hawana woga wowote.Inasikitisha
Na huo mchakato ulianzaje bila kuwa na baraka za magu?

Na kama ulianzia kwake na akaubariki ina maana hakujua matokeo yake?

Na kama alijua kwann aliruhusu uanze?
 
View attachment 1740133
Royal bando

View attachment 1740134
Mega bando kwa wiki

View attachment 1740136
Internet kwa wiki

Kwa mabadiliko haya ya vifurushi kwa nini Waziri Ndugulile asijiudhuru kwa kuudanganya Umma wa Watanzania. Tuliaminishwa kwamba vifurushi vitapatikana kwa gharama nafuu, imekuwa kinyume chake.

Kwa heri Halotel, niliwapenda lkn ndo basi tena. Na jana nimetoka kuwapigia chapuo kuwa mko vizuri, kumbe sikujua masaa machache yajayo ingekuwaje.

Baada ya kutoa yangu moyoni, tujuzane wapi pa kukimbilia kwa sasa.
Kabisa wakuu tujuzane wapi pana unafuu kidogo tukimbilie huko maana kama Halotel hali ni tete eti Sh.1000 = MB 420 plus dakika 15(allnet) kwa wiki, hivi hawa jamaa wako serious kabisa
 
Wakati nchi za wenzetu hata bei ya mkate ikipanda, watu huungana kama Taifa na kupinga hata kwa maandamano yanayohatarisha maisha yao jambo ambalo ni adimu sana kwa nchi yetu kwani hatuna umoja na zaidi tumetawaliwa na unafiki na ubinafsi- mtu mpaka aguswe ndio ajue kuna tatizo.

Kwa mfano, serikali ilipopandisha makato ya Bodi ya Mikopo kutoka asilimia 8 mpaka 15 ya basic salary, kuna watu hawakujali na zaidi waliwakajeli wale waliokuwa wakilalamika kwa maneno ya kuudhi: acheni kulalamika, dawa ya deni kulipa, lipeni na wengine wasome, kazi yenu kupinga kila kitu, n.k.

Wasichojua Watanzania ni kuwa, watawala wameshagundua udhaifu wetu na ndio wanautumia kufanya wanayoyafanya. Kama tungeungana kama Taifa kupinga ongezeko la makato ya Bodi ya Mikopo na mambo mengineyo, sidhani kama leo wangefanya hichi walichokifanya, hivyo watanzania tunaendelea kuvuna tulichopanda kwa miaka hii sita na bado tutavuna zaidi mpaka pale tutapoweka unafiki na ubinafsi pembeni.

Binafsi nimefurahi sana kwani ongezeko hili litagusa watu wengi na hivyo ule unafiki wa tusubiri mpaka mtu aguswe hautakuwepo na hili ndio funzo.

Naomba nimalize kwa kusema hivi:

Kama wewe uliunga mkono mtoto wa mwenzio kunyimwa mkopo kwa hoja alisoma shule za gharama, basi na wewe usilalamikie ongezeko hili la vifurushi kama unamiliki smartphone ya malaki ya pesa.

What goes around, comes around.

CCM oyeeee na hii ndio legacy ya Shujaa wa Africa- ukipenda boga, penda na ua lake.
 
Thanks, for your kind reply,

Umenena vema sana, tena sana...!

Lengo la komenti yangu si kusema kwamba mawasiliano sio basic need, that is why nimetumia neno "huenda".

Huenda ni two side statement.

Walaji tunategemea gharama ya vifurushi iendelee kushuka hata kwa serikali kutoa ruzuka.

Sasa pale gharama mlizotegemea zishuke then zinapanda, unaitafsiri vipi Serikali? Ndio nikasema Huenda imeona huu uhitaji hauna msingi.

Je ni sahihi hazina msingi? Naiomba Serikali iangalie haya maoni yako.
Serikali imeshindwa kuona hili kwa jicho pevu tu, kuna watu wanaabeti na wanakatwa 20% ya kile wanachoshinda. Kuna watu ni Youtubers wanalipia leseni< = than 5M kwa mwaka, kuna watu wanalipia sponsored ads instagram. Kuna watu kula yao ni kupitia kupost matangazo Facebook na Instagram na ndio platform rahisi na ya pekee kuibua talents!

Kwa roho mbaya na chuki binafsi upandishe gharama ili watu washindwe kumudu kutumia mitandao. Toeni hizo ajira basi na mlipe watu mishahara stahiki ili tuwaone mna hata maana. Sio kukalia siasa na kugandamiza watu wasio na hatia.
 
Kwa ukweli kuhusu hili lala bando Mimi naona kama bado halijakaa sawa kabisa🙌🏻
 
Ni upuuzi wa hali ya juu kutosikiliza malalamiko ya watu wengi kama ilivyokuwa kwa jiwe .Mwisho wake ndio kama tulivyoona mtu anapatwa na matatizo watu wanasherehekea.Viongozi mjifunze kutusikiliza wananchi wenu.Hizo nafasi hamtakuwa nazo milele
Yaani kuna watu wanafanya vitu kwa kujiskia halafu yakiwakuta wanataka tuhuzunike wote.
 
😂😂😂😂, dah

Halotel mega bando ya 10k hakuna tena na ile ya 1000 imepigwa panga hatarii. Bando ya youtube 1k kwa 1.2gb haipo tena

Tusubiri voda hiyo tarehe 2 kama sio 20mb kwa buku sijui😅 na 10k kwa 200mbs sijui.
Hizi ni mbinu za kupiga pin social networks specifically whatsapp na Utube, hawataki wananchi kutumia Voice over IP kuwasiliana hapo si ajabu Waziri anashirikiana na makampuni ya simu kuwakomoa wateja ili wasitumie cheaper means za kiwasiliana kwa njia ya simu - hapo naona Mama Samia aingilie kati kwa sababu data zinatumiwa sana wa wananchi,vyuo vya elimu, wizara ya afya na taasisi nyingi nyeti hapa nchini ku stream data muhimu za kuelimisha - ingekuwa vyema kama vingerudishwa vifurushi vya zamani ,mimi nilifikiri biashara huria zinaji regulate zenyewe without Govt intervantion.
 
Hii ndio ilikuwa sera ya Magufuli katika akuhakikisha mitandao ya kijamii watu washindwe kuitumia, maana alishasema anatamani malaika washuke wafungie mitandao.
Alafu kashuka malaika MMOJA TU ndo kamtoa mzee kwenye uso wa dunia na kaiacha mitandao yote inafanya kazi kama kawaida! Kweli Mungu alisema tukiwazacho sie binadamu si sawa na yeye alivyopanga au anavyowaza...

Maisha yanaenda kasi sana, muda mchache na mambo ni mengi...
 
Bei za vifushi kufikia 1st April na 2nd April hazishikiki. Kwa mujibu wa ISP's inadaiwa hiyo moderation iliyofanywa na TCRA. Kiufupi ninahitaji kujua ni nini chanzo cha kupanda kwa gharama hizo kiasi ambacho sisi wengi hatuwezi afford?
Walifanya hivyo iliposikika tu sauti watu sasa wamekataa kuitwa wanyonge,japo huu ulikuwa mpango wa magu
 
Sasa ni rasmi tumestaafishwa kufuatilia movies, series, tutorials kwa njia ya mtandao.

Bando la usiku limeondoshwa

Halotel hongereni

Upande wa zantel kwa huku Zanzibar

Kutoka GB 3 kwa siku kwa shilingi 2000 hadi mb 900 kwa shilingi 2000

Watu wa Airtel vipi huko?

donor country imekuwa sembe country
Ina sikitisha sana tatizo viongozi wetu hata wanapoona nchi zinapigania kuenda hadi 6g wao wanadhani ni kwa ajili ya tweeter na facebook si kwa ajili yakuboresha maisha ya watu wao kielimu kiafya usalama NK ni mpaka tutapoweza kuongozwana watu wenye maarifa ndio maendeleo ya kweli yatakuja najiuliza webnar na online courses tutazisomaje kwa mkabala huu angalau zile za usiku zilikuwa zinatusaidia inabidi ukeshe upate maarifa
 
[emoji23]Utadhani tunaota
Hahaha!! Unajua ilinibidi kwanza nicheke mimi peke baada kuona hayo mabadiliko ya vifurushi, halafu hapo unaambiwa ndy wamepunguza je, kama wamepandisha si ndy wangetuua kabisa hawa watu..
 
Serikali imeshindwa kuona hili kwa jicho pevu tu, kuna watu wanaabeti na wanakatwa 20% ya kile wanachoshinda. Kuna watu ni Youtubers wanalipia leseni< than 5M kwa mwaka, kuna watu wanalipia sponsored ads instagram. Kuna watu kula yao ni kupitia kupost matangazo Facebook na Instagram na ndio platform rahisi na ya pekee kuibua talents!

Kwa roho mbaya na chuki binafsi upandishe gharama ili watu washindwe kumudu kutumia mitandao. Toeni hizo ajira basi na mlipe watu mishahara stahiki ili tuwaone mna hata maana. Sio kukalia siasa na kugandamiza watu wasio na hatia.

You nailed it bro.

The world is shifting to digital world.

Gharama za maisha mtandaoni zinatakiwa kuwa nafuu kuliko wakati wowote ule ili watu waweze kumudu kuishi kwenye huu ulimwengu.

Serikal inabidi ielewe the world is now competing for digital Economy.
 
Mwezi uliopita alikuwa na followers 300K.

Mwezi huu kashafikisha 400K.

Mwezi ujao atakuwa kwenye 500K.

Nachosema hapa ni kwamba kamwe usidhani hili litawakosesha watu kuingia mtandaoni.
 
Hawajui kuwa kupunguza gharama za vifurushi kunachochea kukua kwa uchumi biashara nyingi zitafanyika mtandaoni bila kujali ukubwa wa faili hiyo multiplier effect wao wanataka faida moja kwa moja na hao tcra watoke kwenye mfumo wa kupeleka gawio la kuvunja record wanawanyonya wananchi wao wapo kwa ajili ya kusimamia huduma za mawasiliano wakiweka faida mbele wanaiua Tanzania kwenda na kasi ya maendeleo ya Dunia bila kujua sijui wanakua na matatizo gani mama angefumua huko kuna uozo sana..
Mama amewaambia watumie akili na maarifa kupata kodi. Hii ni nguvu inatumika.
 
Back
Top Bottom