Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Wanaendesha wanavyotaka wao kwa sababu tumekuwa wavivu kupaza sauti physically tuna kalia kupaza sauti mitandaoni ambapo wanapita na kuzipuuza kama vile hawazioni.
Kupaza sauti physically kunataka ujasiri sana especially kuvumilia virungu vya ugoko na mabomu ya machozi wakati wenzenu wametulia majumbani kwao wanawacheki kama sinema😁😁😁
 
Ni upuuzi wa hali ya juu kutosikiliza malalamiko ya watu wengi kama ilivyokuwa kwa jiwe .Mwisho wake ndio kama tulivyoona mtu anapatwa na matatizo watu wanasherehekea.Viongozi mjifunze kutusikiliza wananchi wenu.Hizo nafasi hamtakuwa nazo milele
 
Wakuu,

Kama kweli tunaamini katika uhuru wa mawazo kama haki ya kikatiba, na kama kweli tunaamini katika uwajibikaji wa viongozi, basi naomba huyu waziri Ndugulile asome ninayoandika kama jinsi yalivyo...
Ujumbe mzuri huu kwa ndugu-lile, mwenye I'd yake atusaidie kumuita hapa, please.

Ombi langu kwa mheshimiwa mama yetu mpendwa rais SSH, atusaidie kutumbua huyu mtu tafadhali
 
Wanaendesha wanavyotaka wao kwa sababu tumekuwa wavivu kupaza sauti physically tuna kalia kupaza sauti mitandaoni ambapo wanapita na kuzipuuza kama vile hawazioni.
Sasa tufanyeje mkuu? Onyesha njia
 
Mimi ninavyojua offer hutolewa kwa wateja kama motisha. Maana wanakuwa wamekuchangia na umepata faida

Kulikuwa na ofa ya kwako tu au zile za kikanda ambazo mtu uliweza kupata Mb 500, na hamsini. Sasa wamefuta. Ina maana walitoa ofa sababu waliibia wateja?
CC: MATAGA wote
 
Mkuu, sio basic need kivipi?🙄

Kuna watu wanatumia mitandao kwa masomo, utafiti, biashara, ajira, kazi, nk nk..

Mtu anaweza kuwa Katavi huko, akawa anafanya kazi kwenye kampuni moja au kadhaa US au Europe na anaendesha maisha vizuri tu.

So, kwa sasa internet ni zaidi ya basic need kwa baadhi ya watu, tena wengi. Ukiminya hiko unakuwa unanyonga watu kabisa

Thanks, for your kind reply,

Umenena vema sana, tena sana...!

Lengo la komenti yangu si kusema kwamba mawasiliano sio basic need, that is why nimetumia neno "huenda".

Huenda ni two side statement.

Walaji tunategemea gharama ya vifurushi iendelee kushuka ikibidi hata kwa serikali kutoa ruzuku.

Sasa pale gharama mlizotegemea zishuke then zinapanda, unaitafsiri vipi Serikali? Ndio nikasema Huenda imeona huu uhitaji hauna msingi.

Je ni sahihi hauna msingi? Naiomba Serikali iangalie haya maoni yako.
 
Mchakato ulikuwepo lakini hawakuthubutu kuchukua hatua ya ghafla ya kupandisha gharama kiasi hiki.Kwa kifupi ni kama walikuwa wanasubiri mwendazake apite na sasa hawana woga wowote.Inasikitisha
mwendazake aliwaambia tigo, airtel na zantel mwaka 2016 wasipoingia soko la hisa anazifuta, mpaka leo hajafuta tu
 
Mnapenda kuitwa wanyonge
Ulishaona wapi mnyonge kahurumiwa
 
Nchi hii wapinzani ni sehemu ya tatizo maana wao kutwa wapo mitandaoni tu ndio wanapolalamika na hivyo malalamiko yao yanaishia kuonekana kuwa kama umbeya tu wa mitandaoni ndio maana hata Rais mama samia akasema wenye kununa na wanune huko instar.
 
Hii ndio ilikuwa sera ya Magufuli katika akuhakikisha mitandao ya kijamii watu washindwe kuitumia, maana alishasema anatamani malaika washuke wafungie mitandao.
Akili za kishenzi tu, katika mambo ambayo hayati alichemsha ni hili. kuna makundi mengi mtandaoni wengine wanafanyia biashara wengine recreation. Sasa kuhukumu watu wote sababu kuna cyber protestants ambalo ni kundi dogo miongoni mwa watumiaji ni makosa makubwa sana.
 
Leo tarehe 1/4/2021 makampuni ya simu yamefanya mabadiliko makubwa katika vifurushi vyao.

Wamepunguza vifurushi kwa kiasi kikubwa hasa vifurushi vya data, sitaweka hapa kifurushi kimoja baada ya kingine lkn kwenye mitandao yetu hilo lipo.

Nenda kwenye menu tu nadhani utakutana na upuuzi wote

Nini nataka kusema?
Wakati dunia inakimbia kwa kasi kwenye technolojia sisi tunajirudisha nyuma tena kwa kasi kubwa na wala hapa siyalaumu haya makampuni ya simu kwani yenyewe yanapokea tu order toka Serikalini.

Kama wananchi wa kawaida kabisa tunaiomba Serikali iweze badilisha hiv vifurushi haraka sana maana wanachokifanya ni kurudisha juhudi za maendeleo ya kisayansi nyuma.

Na kwa vile tuna Serikali mpya nina hakika watashughulikia hili haraka sana na wala hawatasubiri hadi mwezi upite maana kilichofanyika ni zaidi ya upuuzi wa hali ya juu.

Kama Serikali itashindwa rekebisha hili basi tutajua hamna mpango na wananchi wa kawaida na mengi mnayoyaongea ni porojo tu

Naomba kuwasilisha.
Huwa najiulza sana eti ndy wanasema gharama za vifurushi zimeshuka hali hii, mwanzo Halotel Sh.1000 unapata GB 1 kwa wiki plus sms na dakika.

Lakini jinsi walivyobadili kwa sasa ni full Majanga tu hakuna nafuu yeyote..
 
Nyie ndiyo mnaturudisha nyuma enzi za ujima.
Matumizi ya Internet ni sehemu ya kujipatia kipato mtandaoni.
Wazee wenye fikra km zako ndiyo wamejaa BOT hata kutoruhusu PayPal. Kenya wameruhusu lkn mewazidi nin kiuchumi? Mezoea shida na umasikini
Kabisa mkuu, wapumbavu sana watu wa hii sampuli.
 
Mimi ninavyojua offer hutolewa kwa wateja kama motisha. Maana wanakuwa wamekuchangia na umepata faida

Kulikuwa na ofa ya kwako tu au zile za kikanda ambazo mtu uliweza kupata Mb 500, na hamsini. Sasa wamefuta. Ina maana walitoa ofa sababu waliibia wateja?
Sasa hiv nafanya survey mitandao mingine nione kulikoni.maana voda wamenishinda
 
Back
Top Bottom