Nina uhakika bila Ujio wake Kaka wa Twita ambao umekuwa ni wa Tija zaidi Kwetu Kitaarifa ( tena zile Nyeti kabisa ) pamoja na Yule Dada wa Instagram Mabadiliko haya ' Kandamizi ' ya Vifurushi vya Simu yasingefanyika.
Vifurushi vyote mmebadilisha, vile vya Chuo ( University Offer ) mmeondoa vyote ( hasa Airtel ) na Kupandisha Gharama maradufu ili Kutukomoa Wanyonge ( Masikini ) akina All - Rounder and the likes nchini.
Najua wapo Wapumbavu na Wanafiki watakaofurahia ila nina uhakika Wao na hasa hasa haya Makampuni ya Simu hayakuangalia kwa umakini Madhara makubwa Kwao Kibiashara ( Kimapato ) na wameogopa Kusimama imara kwa Serikali na Kukubaliana Kwao kutumaliza Sisi Wateja wao kama hivi.
Hatua hii itapelekea Watanzania wengi Wanyonge ( Masikini ) kuacha hata Kutumia Simu hali itakayoshusha Mapato kwa Kampuni husika na hatimaye katika Kujilinda Sokoni nao wakaamua Kupunguza Wafanyakazi hivyo kupelekea hali kuwa mbaya zaidi.
Ni Serikali isiyojielewa tu popote duniani inaweza kutumia Nguvu nyingi Kupambana na Adui yao Mmoja kwa Gharama za Kuwatesa ( Kuwaumiza ) walio wengi ambao ni Wanyonge wakijidanganya kuwa hapo wanamuweza na watatuweza hadi Sisi Wafuasi ( Followers ) wake.
Hivi Serikali husika ingekuwa inafanya ( inatenda ) mema na kwa haki huyo Adui yenu wa Twita ( Kaka ) na Yule mwingine wa Instagram ( Dada ) wangeweza Kuibuka na Kuwaumbueni na Uongozi wenu wa hovyo hovyo uliojaa Hila nyingi kiasi kwamba hadi wengine Mwenyezi Mungu kaamua Kuwatwaa ghafla ili Watanzania tuliobaki tuendelee kuwa na Amani na Furaha?
Halafu mlivyo Majuha ( Wapumbavu ) mmesahau kuwa ' Tozo Kandamizi ' na ' Tozo Komoa ' hizi mlizokuja nazo zitapunguza sana tu pia Mapato yenu kama Serikali na hatimaye mtarudi tena kule kule kuomba Misaada kwa Wakubwa akina WB, IMF, Uingereza, Marekani, Sweden, Ufaransa, Norway, China na Finland bila kusahau na zile nchi zilizopo Arab League pamoja na Waafrika Wenzetu waliotuacha Kimaendeleo Kitambo Egypt na South Africa.
Aliyewaambieni kuwa Watanzania wote watumiaji Mitandao huwa wako 24/7 kuwasoma tu hao Maadui zenu Kaka wa Twita na Dada wa Instagram pekee ni nani? Wengine kuwepo tu mfano hapa Mtandaoni JamiiForums kumetusaidia Kuongeza Maarifa yetu, Ufahamu mkubwa lakini pia tunapata Faraja ya Akili na Afya ya Moyo kwa burudani za Kimawazo ( Kiuwasilishaji ) za hapa Jamvini.
Wengine uwepo wa hii Mitandao ilisaudia tutulie na tuachane na Mawazo ya Kukaba Watu, Kubaka hovyo, Kupiga Punyeto hadi Mikono pamoja na Vidole Kuvimba, Kukaa Vijiweni na Kunywa sana Gongo bila kusahau Kuvuta Udi Karaha ( Bangi ) hivyo basi huenda kwa hatua yenu hii ya Kipumbavu na iliyojaa Chuki na Ukatili Kwetu Watanzania wengi basi tukaanza Kurejea katika Uovu tuliouacha Siku nyingi tu.
Msiponiona tena hapa JF jueni nami All - Rounder ni Mhanga Mwandamizi ( Mkomavu ) wa hatua hii hivyo kutokana na Ufukara wangu mkubwa sina uhakika kama nitaviweza hivi Vifurushi vipya vya Waziri Faustine Ndugulile.
Na wale Matajiri wa Kununua Vocha na Kuweka Mabando ya kutosha nawatakieni tu kila la kheri. Nimesikitika na Kuumia mno ila hukumu Kamili kwa Waziri Ndugulile na Makampuni yote ya Simu yaliyokubaliana nae pamoja na Yule aliyeshika Usukani sasa wa Kikatiba Serikalini namuachia Mola ( Maulana ) na najua atanijibia na atatujibia tu kama ambavyo alitujibia pia ghafla Wiki chache zilizopita.