Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Mkuu hapa tunazungumzia upande wa Mb tu ila hata Dakika za maongezi nako hawajaacha salama pia.
 
Toka wamerekebisha virufushi Halotel yamekua yakiibia wananchi ukijiunga kifurushi cha Tsh 2000 ili upate MB 900 yanaiba yanakupa MB 400 tu ambayo ni sawa na Tshs 1000. Muda si mrefu natupa line yenu.
Kile cha buku kwa wiki 1GB ilikuwa lazima baada ya siku tatu kiishe hakidumu zaidi ya hapo hata ujibane vp.
 
Hii kitu waiache kwa kampuni za mawasiliano zishindane zenyewe...

Hapo kabla tulikuwa vizuri tu. Kulikuwa na kasoro za hapa na pale, hizo ndizo zilizopaswa kurekebishwa..

Lakini kwa marekebisho haya ndiyo wameharibu na kuliongeza tatizo kuwa kubwa zaidi...
 
It's a matter of time tu
 
Wananchi tuna haki ya kujulishwa na kupewa ufafanuzi sahihi kusudi tusijekuwa tunaibiwa.

Kazi mojawapo ya serikali ni pamoja na kulinda wananchi wake kwa namna nyingi, chakula, mipakani, usalama wa raia n.k

Ndungulile uje utujulishe kwa ufasaha itisha press conference mara moja utuambie !
 
Kodi gani ambayo inasemekana kuongezwa?

Kodi siyo sehemu ya gharama za mauzo (COGS) au uzalishaji kiasi cha kuweza kuathiri bei ya bidhaa au huduma,

Werevu watakubaliana nami kuwa Tax has nothing do with pricing of a commodity!
 
Usitoke, tulia huko huko.
Ngoja nije huko angalau naona kuna unafuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…