Kwema lakini Watanzania wenzangu na msio watanzania ila naamini mko salama.
Aiseee toka sheria mpya ya vifurushi kupitishwa kumefanya maisha kuwa magumu zaidi kwa wenzetu wanaoishi kwa kutegemea biashara zao zilizopo huko mitandao ya Kijamii. Hebu tuweke ushabiki pembeni..! Mambo yamekuwa magumu kiasi fulani asee...! Yaani imekuwa either uamue kuwa online au ununue mboga [emoji22][emoji22].
Siku ya Juzi, TCRA waliagiza kusitishwa kwa gharama hizo mara moja na kuahidi kutoa utaratibu mpya hapo baadae. Sasa Vodacom walivyo jeuri hadi sasa vifurushi vyao gharama zao zipo juu hebu tizama screenshot hapo chini
View attachment 1742949
Hivi kweliii kwa hali hii tutoboa kweli sisi Freelancers ?? Wengine ambao kuwa online sio lazima sana wanaweza kuzima data na maisha yao yakaenda vizuri tu.
TCRA hebu wachukulieni hatua hawa Jamaa, Vodacom umekuwa mtandao wenye jeuri sana hapa Nchini. Sijui kuna shida gani hapo TCRA kuhusu kulichukulia hatua hili kampuni kwa kuwanyonya wananchi kiasi hicho.!
TCRA kuleni kichwa huyo