Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Fanya hesabu mara 500 huoni ni faida kwako now ni 0.7mb/1tsh
Faida kiaje umeelewa vizur hapo?
Yan 1mb had 1.5mb iliuzwa kwa Tsh 1 kwaiyo hapa ni sawa na kusema kwa sh 500 ulikuwa unapata 300-500mb ambayo kwa sasa upati hvyo.

Faida hiyo ipo wap hapo kwa vifurishi hiv vipya
 
Nchi hii wapinzani ni sehemu ya tatizo maana wao kutwa wapo mitandaoni tu ndio wanapolalamika na hivyo malalamiko yao yanaishia kuonekana kuwa kama umbeya tu wa mitandaoni ndio maana hata Rais mama samia akasema wenye kununa na wanune huko instar.
Huko insta ulienda kufanya nini?
 
Ubongo wako ulimkabidhi mwenyekiti, washamzika nao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni majanga huku TTCL sijui kwengine.
Hapo tarehe 14/03 wala sikuongeza salio lolote cha ajabu nikapata huo ujumbe.
 
Hayupo sasa.

Waliobaki wameshindwa nini?
Mh RAIS alianza na taasisi za kutoa haki pccb, DPP waondoe kesi zisizo na ushahidi na Wasibambike kesi,TRA waache kuongea watu kupita fedha za wafanyabiashara.

Ujumbe huu ulipaswa umfikie Ndungulile abadilike mpango wa kumshusha malaika kufunga mitandao ulikuwa wa mwendazake.hii awamu ya sita .
 
Jamani wengine hatuna pesa tunaungaunga tu. Ndugulile ulipokaa na hayo makampuni na huu utopolo mpya wa vifurushi ni ujinga mtupu hakuna ahueni yoyote mliyotupatia sisi kina kajamba nani kama buku kwako sio pesa kwetu ni ya thamani sana yaani 600 eti mb 80 hiyo ni Voda sasa.

kwl pesa yetu ndiyo imeshuka hadhi kiasi hiki? Mama huyu alinyanyua mabega enda naye baraka zetu unazo mama...walitudanganya ukiunga kifurushi ukipewa dk Hata 50 zitakuwa zinaisha pale utakapozimaliza iwe mwaka siku,ni wewe na matumizi yako sijui ni utopolo gani huu wameleta gharama zimepanda Mara dufu za vifurushi kama VP turudishieni bando za zamani...again mama tumbua hii Ndugulile jipu Lina usaha kabisa tena wenye harufu...
 
Hii ilikuwa sera ya marehemu angekuwepo mngeambiwa asiyetaka aache

lakini Ndungulile siyo mtendaji mzuri kwa kuwa upepo umeshabadilika angejadiliana na wakubwa zake kuhusu hili suala wahairishe kwanza au wapeleke mbele wakiwa wanatafuta muafaka wa kuliopotezea hili suala

Ndungu anashindwa kwenda na upepo
Mzembe sana wenzie sasa hivi ukiwaangalia huwezi kujua kwamba ndiyo wale wa enzi za Magufuli wameshabadili gia
 
Aisee nilikuwa bado sijagundua kitu hiki, ndo maana nashangaa Internet kila wakati inakata kumbe napigwa halafu hadi sasa hivi bado hali ni ile ile sasa sijui tangazo la serikali limefikia wapi au ndo mambo ya zamani yanataka kurudi ya kwamba MTU MWENYE PESA ANAWEZA FANYA CHOCHOTE MAANA SERIKALI YOTE IKO MFUKONI MWAKE?
 
Faida kiaje umeelewa vizur hapo?
Yan 1mb had 1.5mb iliuzwa kwa Tsh 1 kwaiyo hapa ni sawa na kusema kwa sh 500 ulikuwa unapata 300-500mb ambayo kwa sasa upati hvyo.

Faida hiyo ipo wap hapo kwa vifurishi hiv vipya

I mean mitandao ndo inapata faida ilihali wengne tunateketea.

Kwani hamna mtu mwenye no za Rais?
 
I mean mitandao ndo inapata faida ilihali wengne tunateketea.

Kwani hamna mtu mwenye no za Rais?
hapo ndio ule msemo wa "aliyenacho ataongezewa asiyenacho atanyang'anywa ata kile kidogo alicho nacho" unataka kutimia
 
Kwema lakini Watanzania wenzangu na msio watanzania ila naamini mko salama.
Aiseee toka sheria mpya ya vifurushi kupitishwa kumefanya maisha kuwa magumu zaidi kwa wenzetu wanaoishi kwa kutegemea biashara zao zilizopo huko mitandao ya Kijamii. Hebu tuweke ushabiki pembeni..! Mambo yamekuwa magumu kiasi fulani asee...! Yaani imekuwa either uamue kuwa online au ununue mboga [emoji22][emoji22].
Siku ya Juzi, TCRA waliagiza kusitishwa kwa gharama hizo mara moja na kuahidi kutoa utaratibu mpya hapo baadae. Sasa Vodacom walivyo jeuri hadi sasa vifurushi vyao gharama zao zipo juu hebu tizama screenshot hapo chini

Hivi kweliii kwa hali hii tutoboa kweli sisi Freelancers ?? Wengine ambao kuwa online sio lazima sana wanaweza kuzima data na maisha yao yakaenda vizuri tu.
TCRA hebu wachukulieni hatua hawa Jamaa, Vodacom umekuwa mtandao wenye jeuri sana hapa Nchini. Sijui kuna shida gani hapo TCRA kuhusu kulichukulia hatua hili kampuni kwa kuwanyonya wananchi kiasi hicho.!
TCRA kuleni kichwa huyo
 
Zantel tumerudishwa kama mwanzo. Tupo vyema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…