unafikiri gharama ya bilioni 200 ni realistic kufanya hayo yote?
Siwezi kusema kama ni realistic ama sio kwasababu sipo kwenye mchakato wa kupata supplier wa mradi huo na wala sijui bei ya miradi kama hiyo. Inawezekana figure ikawa realistic bila kuwa justifiable.
Nataka kuamini unazungumzia kama pesa hizo ni justifiable. Kama hilo ndilo swali lako, naweza kusema "
Yes" endapo tu mradi utasimamiwa vizuri kuanzia kwenye tender, utendaji n.k. Na kuhakikisha kuwa pesa hizo zinatosha kufanya yote yanayotarajiwa kuanzia mitambo, card zenyewe, data input na distribution. Vinginevyo, haiwezi kuwa justifiable kutumia pesa zote hizo. Naweza pia kusema "No" kama mradi unakusudia kufanya machache zaidi ya hayo hapo juu.
Mbona vitambulisho hivyo vipo tayari, vinaitwa Passport na tumekuwa tukivitoa tayari na hivi karibuni tuliweka vya kisasa zaidi. Kwanini tusitumie passport ambazo tayari zina unique number, features, na tayari vinatutambulisha. Kwanini kwa mfano, tusiwe na utaratibu wa dual ID... moja ni Pass cha pili ni kitambulisho cha mkazi kinachotolewa kila mkoa?
Mkuu passport ni hati ya kusafiria. Sisi masikini hapa kwetu tunaitumia kwakuwa ndio document inayoaminika zaidi kuliko nyingine zozote tulizonazo. Passport Mkuu, haitolewi kwa kila mtu (si kila mtu ni msafiri wa kwenda nje ya nchi. Hivyo si kila mtu anaeweza kupewa Passport). Na hata kila mtu akipewa, gharama yake itakuwa kubwa kuliko mradi tunaouzungumzia hapa Siwezi kusema zaidi ya hapo kwa maana unaelewa vizuri tu.
Document nyingine ambayo nayo imeanza kutumika sana ni Kitambulisho cha mpiga kura (Voters ID). Hiki hakigawiwi kwa kila mtu. Kinatolewa kwa watu waliotimiza masharti ya kupiga kura tu. Na pia hakina feature yoyote zaidi ya maelezo yaliyopo kwenye daftari la kupigia kura.
Kuhusu swali lako la dual ID, nadhani itakuwa no kuongeza wingi wa documents tu. Labda unieleze mantiki yake hasa ukiilinganisha na Kitambulisho cha Utaifa.
[QOUTE]Nadhani hili linahusiana zaidi na utendaji na ufuatiliaji wa taratibu ambazo tayari tunazo kuliko kukosekana kwa vitambulisho.
Fikiria: Kila mtoto anayezaliwa anapewa cheti cha kuzaliwa! Cheti hicho kinasema huyo ni mtoto ni wa jinsi gani, wazazi wake ni nani, alizaliwa lini na wapi. kwanini Cheti hicho kisiwe ndiyo msingi wa utambulisho wa uraia? Kinachofanyika ni kutengeneza database inayounganisha taasisi zote za serikali na ofisi ya msajili wa uzazi na vifo? [/QUOTE]
Nadhani vyeti vya kuzaliwa vinatakiwa kusomeka kwenye kitambulisho hiki (Smart ID) ili kuwa na maana zaidi. Inawezekana kabisa. Kuhusu kutambulika kwa mtanzania kupitia cheti cha kuzaliwa, naona kama haijakaa vizuri. Haijakaa vizuri kwa maana ukilisema kwa sauti mafisadi wakasikia, watataka kubadili vyeti vyote vifae kuwa vitambulisho (Gharama yake nayo ni sawa ama kubwa zaidi ya hii 220Bil).
Mkuu hakuna cheti cha kuzaliwa chenye picha hata kimoja. Hivyo havifai kumtambulisha mtu. Vile vile, si kila mtanzania amezaliwa Tanzania. Kuna waliozaliwa nchi nyingine na kupewa vyeti huko huko. Sijui hawa wanafanywaje katika utaratibu wa kupewa vyeti vya kuzaliwa (wenye kujua wanaweza kusaidia hapa). Ila naamini utekelezaji wa kuwapa hao vyeti unaweza kuwa mgumu sana. Maana Ofisi ya Kabidhi wasii nadhani haina kumbukumbu zao za kutosha.
Ninachoona na ambacho tunakifanya vizuri ni duplication of services! Je tukiwa na Smart ID, tutaendelea kuwa na Passport?
Ndio Mkuu, tutaendelea kuwa na Passport kwa wale wasafirio kwenda nje ya nchi. Wale wasiohitaji kusafiri, hawana haja ya Passport, ila wanayo haja ya kutambuliwa. Hili ni jukumu la Kikatiba zaidi ya yote.
Asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini, zaidi ya kufungua akaunti na kupata mikopo hizo kadi atazitumia wapi zaidi.
Mkuu, kitambulisho cha utaifa kitasaidia sana kumtambua mtu sehemu yoyote atakayokuwa. Itasaidia pia kuhakikisha mtu huyo anapata haki stahili. Kwa mfano, mtu amenyimwa haki ya kupiga kura kwa kuwa hakuwahi kuwa na kadi kwa ajili hiyo (labda ndio amefikasha umri au hakukaa nchini miaka mingi). Mtu huyo ni lazima athibitishe kuwa hakuwahi kuwa na kadi kweli au ilipotea na kuwa jina analodai kujiandikisha ni lake na mambo mengine chungu mzima. Mtu huyo akiwa na ID kama hiyo, maongezi yanakuwa machache zaidi na utendaji wa kupewa kadi unakuwa rahisi.
Sasa hivi, nguvu nyingi sana ya serikali inatumika bila tija kubwa. Urasimu unakuwa mkubwa kwa kutokuaminiana n.k. Vitambulisho hivi nategemea vitaweza kutatua baadhi ya matatizo haya.
Kuna suala la faragha hapa ambalo ni kubwa zaidi. Sitaki mtu mmoja awe na uwezo wa kujua benki yangu, taarifa zangu za afya, kazi yangu, n.k kwenye kikadi kimoja!
Nadhani hofu yako Mkuu ni ya haki kabisa. Ila nina uhakika wanaoshughulikia hili wataangalia jinsi ya kulinda faragha za watu. Ila kuna taarifa ambazo ni lazima ziwe wazi kwa baadhi ya taasisi. Taarifa kuwa una account katika Bank zipi, Unafanya kazi gani, Una elimu gani, umewahi kushitakiwa kwa makosa gani, umewahi kutembelea nchi gani n.k. Ni muhimu kuwa kwenye kadi hiyo si kwa manufaa yako tu, bali kwa manufaa ya wengine pia ambao wanakusudia kushirikiana na wewe katika mambo mbalimbali ya kijamii, kiuchumi n.k.
Mkuu faidi za mradi huu zinaweza kuwa nyingi sana kama utafanywa vizuri inavyotakiwa.
Sijui umepata wapi figure hiyo, lakini let me assume for a second kwamba ni sahihi. Hii ina maana kuwa ni Tsh bilioni 220. Je gharama ya kuleta mitambo ya kusomea kadi hizo, kuandaa database, kuajiri wafanyakazi, kufanyia matengenezo, n.k inafikia kiasi gani?
Figure hiyo nimeifanyia mahesabu ya haraka haraka tu (assumption 40mil people).
Naamini kuwa mchakato mzima wa Vitambulisho hivi unashughulikia zaidi technology na hasa mitambo ya uzalishaji wa vitambulisho pamoja na mengine yote. Ila gharama hizi zinatakiwa ziweze kukidhi mahitaji ya kuchapisha cards zote, na kusambaza. Sijui scope ya supplier anaetakiwa.
Tatizo ni kuwa, twaweza kuwa na vitambulisho vizuri vya raia bila kuwa ni lazima viwe hivi vya Smart Cards. Hivi kweli unaamini njia pekee na bora ni hiyo ya smart card? l
Nadhani vitambulisho vizuri ni vyenye security kubwa iwezekanavyo (ili isiwe rahisi ku-fodge na kufanya maradi mzima kuwa hauna maana), viwe na uwezo wa kuweka kumbukumbu nyingi iwezekanavyo kwa kila mmiliki, visomeke tu kwa wenye mamlaka ya kivisoma na kwa ujumla vitosheleze mahitaji.