Tanzania sihami, Matokeo ya Sensa yakioneshwa kwa Helkopita

Tanzania sihami, Matokeo ya Sensa yakioneshwa kwa Helkopita

Uwezo wa MTu flan kufikiri na kuamua..
watu hawana maji salama
images.jpg
 
Nchi ina pesa za kuchezea wakati ikiwa na matatizo msululu.

Ama kweli, ni aheri unyimwe vyote, upate akili ya kutambua uwezo wako, kutambua kuwa mbwembwe hufanywa baada ya kukamilisha yote yaliyo ya muhimu, badala ya kuanza na anasa, mambo ya muhimu inakuwa ziada.
 
Msilaumu msije kulaumiwa.
Ukweli hiki ambacho kinafanyika now ni kuwananga waliokuwepo wakati wa jeshi la mtu mmoja, sidhani kama kuna la ziada.

Na sisi wananchi tuache lawama zisizo na maana, mlikuwa mnalialia sana hali ngumu, pesa hakuna leo mbuzi kakata kamba mnalalamika, mfanyiwe nini asee watz..?

Hali bado ni tete mkuu au wew ulipo unanyonya maziwa na asali ndo maana unaropoka hivyo
 
Nimeandika nimefuta mara tatu.

Magufuli pamoja na kumsema alikuwa mbaya alijitahidi kubana matumizi Ili Hela ionekane. .
Kwangu mimi, Magufuli pakubwa aliponikwaza ni kupoteza watu, kuteka watu na kubambikia watu kesi za uhujumu uchumi, na kutoheshimu misingi ya demokrasia na haki za watu.

Ukiacha zile 1.5 trillion na zile pesa walizotoa waliobambikiwa kesi za uhujumu uchumi ambazo hazieleweki ziliishia wapi, kwenye kudhibiti matumizi ya hovyo kama hizi sherehe zisizo na vichwa wala miguu, Magufuli alimudu vizuri.

Serikali inachezea pesa ilihali hao wanaotoa hizo pesa wapo hoi bin taabani.
 
Tunashule za sekondari elfu tano nchi nzima badala tujitafakari, umeme/maji/chakula shida badala tutafakari tunaalikwa tukashangilie helkopta.

Mimi nilimjibu niletee maji nioge ndio nije maana hamna maji huku kwetu! sijui aliisoma?
 
Tuendelee kushabikia kabumbu tuu,na ikiwezakana wenye kubeti mbeti kweri kweri.
 
Helkopta ikionesha idadi ya Watanzania kutoka matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022.

Tuko 61,741,120. - Gerson Msigwa
================
Mheshimiwa hizi helkopita zingeenda kusaidia kuzima moto mt. Kilimanjaro huoni mngetumia busara.



Hivi hii idadi inajumuisha na yule katibu wa Mzee wa Kukandamiza.
 
Nilitarajia rais angekaa zake ikulu na kulihutubia taifa kwa dakika 5 na kutangaza hayo matokeo. Lakini kitendo cha kufanya gafla kubwa namna ile kwa jambo dogo hili, hakika ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
Hivi hii helkopta imetembea nchi nzima?

Na hata hapo ilipoonyeshwa, ni watu wangapi wameona maandishi hayo?

Kwanza 'design' yenyewe ni mbovu, haivutii na haisomeki kiurahisi. Hawa waliobuni njia hii itakuwa ni vihiyo, hawajawahi kujua njia nzuri za kutangaza kwa njia hiyo.
 
Back
Top Bottom