Tanzania tuachane mfumo wa kupandishia watu mishahara bila kuwa na vigezo vya utendaji (performance)

Hii
Hii ni canada ulipoishi au ni nchi ya mnyazimungu. Sorry namaanisha kwa wakristo au kwa mwamedi.
 
Mimi sio mtumishi wa umma ila hili wazo lingeanza na katiba mpya itakayokiondoa chama chochote madarakani kitakachoharibu. Tusianze na watumishi wa umma tuanze na katiba mpya itakayo waondoa wasimamizi wa sera na watunga sheria.
Katiba mpya au ya zamani haijalishi. Kuna nchi hazina katiba na zinafanya vizuri. Ni kujipanga tu.

Unategemea katiba mpya ikupe lipi jipya? Nani wa kuitunga hiyo katiba mpya? Au tu "copy amd paste" katiba ipi duniani?
 
Hizo fomu anaezijaza ni mwajiriwa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787], unaandika vitu ulivyofanya kwa muda fulani
 
Nchi za nje zimepiga hatua sana kimaendeleo na kimikakati, binafsi nimeupenda huo utaratibu sana
 
Katiba mpya au ya zamani haijalishi. Kuna nchi hazina katiba na zinafanya vizuri. Ni kujipanga tu.

Unategemea katiba mpya ikupe lipi jipya? Nani wa kuitunga hiyo katiba mpya? Au tu "copy amd paste" katiba ipi duniani?
Hili ni swala la checks and balances tuanzie na wanasiasa !
 
Mbunge hapafom tunapiga chini chama hakipafom tunapiga chini ndio uje kwa watumishi (sera iwe uongozi kwa mfano)
 
Unalosema linaweza kuwa kweli na linaweza kuwa si kweli. Umetumia kipimo kipi kumuona kuwa Rais ni mzembe.

Niuonavyo mfumo wa Urais Tanzani na madaraka aliyonayo Rais, hawezi kabisa kuwa mzembe, huo muda wa uzembe atautoa wapi? Sema wale wenye kumsaidia Rais ndio wanakuwa wazembe namba moja, hususan mawaziri na wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa tasisi na mashirikaya kiserikali/ Duh. Mlolongo ni mrefu sana.
 
Katiba wapi imekataza kuwekwa vigezo vya kupandishwa mshahara?
Soma ibara ya 23 utapata jibu. Acha ujuaji usio kuwa na tija. Kima cha chini hakina sababu ya kuwepo na vigezo ni suala la kuwa na mshahara unaokidhi mahitaji kwa watumishi. Katiba ipo wazi ni kuwa na just renumeration.
 
Ndiyo hivyo meku, hata mimi nimeupenda sana huu uzi na kwa kuwa mleta mada FaizaFoxy ni ameshapata uzoefu nje ya nchi haya mambo alioyainisha yana misingi mikubwa sana kukuza uchumi wetu,

Leo katika pitapita yangu mitandaoni nimegundua GDP 2022/2023 ya kenya na Tanzania ya kenya ipo vizuri sana na inaendelea kufanya vizuri tangu 2021 sasa kama uchumi haupandishwi na wafanyakazi hizo hela za kuweka nyongeza ya mishahara inatoka wapi
 
Lichama linaiba kura miaka nenda rudi halileti maendeleo vs rasilimali mkilichalenji linauwa na kuteka watu kwanini msianze kuliondoa lichama la hivi kabla hamjaenda kwa walimu na watumishi wanyonge?
 
Unahitaji maombi ya Mwamposa
 
Lichama linaiba kura miaka nenda rudi halileti maendeleo vs rasilimali mkilichalenji linauwa na kuteka watu kwanini msianze kuliondoa lichama la hivi kabla hamjaenda kwa walimu na watumishi wanyonge?
Hapo wapiga kura wanajiuliza, mbadala wa "lichama" hili, kuna "lichama" lipi lengine lenye maana?

Chama kipi Tanzania amabacho kina hati safi kwa ukaguzi wa "portion" tu ya "administration" unaofanywa na CAG?

Hapa tunaongelea "performance" hatuongelei siasa, kwa sababu naamini Tanzania wana siasa wenye nia hasa ya kuleta mabadiliko kwa wananchi ni wachache sana, 90% wa ya wanasiasa wapo kwenye siasa kwa kuwa ni njia ya mkato ya kujineemesha, hususan bunge.
 
Iendane na facilitation,anapanga bajeti yake kama mtumishi,inaletwa kama ilivyo kama huko private,tuone kama atashindwa kuperform
Tatizo sio budget, tatizo hao wafanyakazi hata "fundamentals" za budget hawaelewi namna kuzipanga.

Elimu kazini hakuna, Ikipangwa semina ya kuelimishana uelewe imepangwa ili watu wajipatie ulaji na "kula bata". Hilo ni dhahiri kabisa.
 
Rais amehoji, mbona hakuna bango linaloonyesha jitihada za wafanyakazi katika kuboresha uchumi wa nchi ila kila bango ni kuhusu mishahara tuu.
Kodi wanayo katwa haiboreshi uchumi? Kazi wanazo fanya haziboreshi uchumi?
 
Rais kwa nafasi yake ni Mwajiriwa nambari moja.

Yeye ni Boss.

Yeye ni Msemaji wa mwisho katika Masuala mengi na mbalimbali ya Kiserikali, Kisheria na mengineyo.

Yeye anatazamiwa au naweza kusema tunamtizama matendo, mienendo na hasa utendaji kazi wake ili na sisi tujipimie kama ni kutembea au kukimbia.

Anaposhindwa au hao wanaomzunguka wanaposhindwa pamoja nae kuhusu jambo fulani katika uchangamoto wake na Suluhu kwa macho ya wazi bila kupepesa inaonesha jambo lenyewe linawezekana basi hatuna budi kumuona Mzembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…