Typist au mchapaji anatakiwa abadirishe namna ya kubonyeza keyboard?
Mwl anatakiwa abadili namna ya kufundisha kila baada ya miaka mitano?
Jitazame wewe ulivyoandika "adadirishe" badala ya abadilishe. Kiswahili hicho kama alikufundisha Mwalimu wako, basi huyo Mwalimu alikuwa hafai, ni mjinga, na huo ujinga akakufundisha wewe, sasa unauendeleza.
Hizo ndizo shule za kufundisha ujinga.
Hata "arguments" zako ni finyu kiasi huelewi kuwa vipimo vya utendaji vikiwekwa na kutekelezwa kwa ufanisi ndivyo vinapelekea wafanyakazi kupewa mafunzo ya ziada ya kazi pale wasipopaweza kiubora.
Ukipitia vizuri huu uzi, nimeandika juu huko, kipimo cha ubora wa kazi kitapelekea au Mwalimu apandishe mshahara au apelekwe tena mafunzo kazini ili afikie kiwango kinachohitajika palae ambapo ataonekana hana kiwango bora. Au akishindwa kabisa itabidi ahamishwe hiyo kazi atafutiwe kwengine anapopaweza.
Licha ya kuwa si lazima kila Mwaalimu apandishwe daraja na kulipwa zaidi wakati hana kiwango, pia si lazima kila Mwalimu abaki kuwa Mwalimu hata asipoweza kufundisha. Vipimo vya uwezo wa kazi vya mara kwa mara ndivyo vitatoa majibu.
Narudia, huku kwa Walimu ndipo haswa zoezi hilo lianzie na lifanywe kwa nguvu na uadilifu mkubwa bila kuwa na huruma.
Mtu kama hawezi kufundisha akapike mandazi auze, badala ya kuleta mandazi wanafunzi wawe ndio wawe wateja wake wa mandazi. Ni ujinga tu.
Tukianzia kwa kuwa na Walimu bora basi ndani ya miaka michache tutakuwa na wafanyakazi bora kabisa, wafanyakazi wakifundishwa maadili mema, uchapa kazi, nidhamu kuanzia mashuleni, makazini itakuwa hakuna haja ya kupoteza muda kuanza tena kuwafundisha hao.
Shule zetu zinazalisha wafanya kazi wabovu kabisa. "No excuse".