Mama aanze kuweka plan ya kubana matumizi yaa serikali ikiwemo kupunguza safari za nje sasa, yeye na watu wake.
Serikali iwe serious Sasa kudhibiti wizi na majizi waliojazana Kila Kona hivi Sasa na wengi wao hizo hela wanaficha nje na kununua vitu vya anasa kama magari ambavyo vingi hutoka nje
Tuanze kuacha kununua vitu visivyo na ulazima nje, kama furnitures, magari na matumizi mengine ya serikali na taasisi zake.
Tuache sasa kununua midege baadala yake tujikite kuongeza ufanisi kwa hizi zilizopo hasa kuzitafutia route nyingi za nje.
Serikali ianze Sasa kuwa serious kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa na kuwawezesha wakulima vitendea kazi na kutafutia mazao yetu masoko serious.
Serikali ifikiri namna ya kuhakikisha viwanda vya nguo vya ndani vinafanya production ya kutosha na nguo quality ili tuache utegemezi wa kuagiza mitumba na nguo kutoka china.
Serikali iache kujenga jenga hovyo Kwa kutumia wakandarasi wa nje, baadala yake ijikite kutumia na kuwawezesha wakandarasi wa ndani, ujenzi ufanyike tu pale kwenye ulazima na sio Kila siku tunajengajenga tu hovyohovyo.
Mambo ni mengi sana,wengine wanaweza kuongeza hapo.