Tanzania visiwani waomba msaada wa walimu toka Nigeria, wakati Bara kuna walimu hawana ajira

Tanzania visiwani waomba msaada wa walimu toka Nigeria, wakati Bara kuna walimu hawana ajira

Hapo kuna tatizo kweli. Hata ukitoa siasa, kuna haja gani ya kumwajiri mwalimu kutoka Nigeria? Ikiwa Tanganyika hamna walimu wa kutosha, mbona wasikaajiri kutoka Uganda au Kenya? Kiingereza cha Nigeria hakieleweki kamwe.
Zanzibar inatakiwa ipige hatua moja mbele zaidi,hii ya kuagiza walimu kutoka Nigeria isimalizikie hapo,Zanzibar irudushe mfumo wake wa elimu ifate "syllabus" ya Oxford kama ilivyokuwa ikifata hapa nyuma,waachane kabisa na mfumo wa elimu wa Tanganyika,Kufata "syllabus" ya Tanganyika ni moja katika ukoloni mamboleo
 
Wamefanya uamuzi wa busara kwa manufaa ya wazanzibari. Kuna ombwe kubwa katika ufundishaji wa masomo ya sayanzi na hesabu nchini.
 
Habari nzuri
Ndio walimu wa Tanzania wajue inabidi wajiongeze..
Hahahaa......Zanzibar inahitaji waalimu wanaojua Kiingereza, siyo hawa wa kwetu. Hapa Bongo notes tuu ndiyo huandikwa kwa Kiingereza lakini ufundishaji ni kwa Kiswahili. Mwalimu gani hawezi kunyoosha sentensi fasaha mwanzo mwisho? Janga la nchi hili!
 
Hao wanafunzi wajipange tu
maana hicho kingereza chao usipokuwa makini hatari.
nawakumbuka marafki zangu wa TATCOT hatari
 
Haya hebu niambie ni mambo gani ya kitoto ambayo yanafanywa na Wazanzibari ???
Mkuu unaongea kana kwamba matatizo yote ya Muungano yanasababishwa na Wazanzibari peke yao.
Ndio hivyo Mkuu,Ninavyoiona Zanzibar na "opportunities" walizokuwa nazo kama nchi, ilikuwa haina haja ya wao kuinyeyekea Tanganyika...

Zanzibar na Tanganyika ni nchi huru mbili zilizoungana na kuunda Tanzania,Zanzibar ina katiba yake ina Bendera yake,ina wimbo ya Taifa,ina jeshi lake,ni nchi iliyokamilika,Cha kushangaza Wazanzibari wanapokwenda kwa mshirika wake katika Mungano yaani Tanganyika wanakwenda kimakundi badala yakwenda kama Nchi..

Si unakumbuka mchakato wa rasimu ya katiba mpya katika bunge la JMT ,Wanajibagua wenyewe ili wapate kutawaliwa "divide and rule",na ndio maana nimesema usiwalaumu viongozi wa Tanganyika walaumu wazanzibar kwani wanajitakia wenyewe,watawala wa Zanzibar, CCM Zanzibar ndio janga la Zanzibar
 
Hao wanafunzi wajipange tu
maana hicho kingereza chao usipokuwa makini hatari.
nawakumbuka marafki zangu wa TATCOT hatari
Umeshasikia kuwa sio mara ya kwanza kwa walimu wa Nigeria kufundisha Zanzibar,...kwahiyo Zanzibar ina uzoefu na hawa walimu...,mtamaliza kuongea yote lakini Wanzanzibari ndio wameshaamua,naona hili limekukereni sana
 
hivi vijana wa bara hawaruhusiwi kuomba ajira visiwani...?
 
Hawa wakatiwe umumu shenzy zao
Umumu = Umeme..,ndio maana wazanzibari hawawataki walimu kutoka Tanganyika,kiswahili ndio kama hivyo sasa "Umumu" ndio nini!!,sio mtawafelisha hata hiyo lugha yao ya kiswahili...
 
hivi vijana wa bara hawaruhusiwi kuomba ajira visiwani...?
Hawaruhusiwi,unakumbuka kuwa vijana wa Tanganyika walikuwa wanaingia kwa Passport Zanzibar!,Salim Amour aliekuwa raisa wa Zanzibar ndio kaja kuiondosha hiyo,...
 
Hawaruhusiwi,unakumbuka kuwa vijana wa Tanganyika walikuwa wanaingia kwa Passport Zanzibar!,Salim Amour aliekuwa raisa wa Zanzibar ndio kaja kuiondosha hiyo,...
wanaruhusiwa, sema hawajui inakuwaje...?
wajua kuna vijana madakitari wengi tu unguja na pemba....
 
Umeshasikia kuwa sio mara ya kwanza kwa walimu wa Nigeria kufundisha Zanzibar,...kwahiyo Zanzibar ina uzoefu na hawa walimu...,mtamaliza kuongea yote lakini Wanzanzibari ndio wameshaamua,naona hili limekukereni sana
Nikereke nini sasa kwa vitu vidogo kama hivyo ambvyo havina faida yoyote kwenye kazi zangu na kwa shule yangu.
pambaneni na shida zenu
 
Hapo kuna mambo lukuki yamezingatiwa. Inawezekana
1. Udini
2. Fitna ya suala la sukari
3. Kuonesha kwamba wanaweza ku-survive nje ya kutegemea Muungano huu
 
Bara kuna jamaa wanasota kitaa hawana Ajira lakini Zanzibar wanaagiza Nigeria.Naona ni kama Sukari tu
 
Zanzibar inatakiwa ipige hatua moja mbele zaidi,hii ya kuagiza walimu kutoka Nigeria isimalizikie hapo,Zanzibar irudushe mfumo wake wa elimu ifate "syllabus" ya Oxford kama ilivyokuwa ikifata hapa nyuma,waachane kabisa na mfumo wa elimu wa Tanganyika,Kufata "syllabus" ya Tanganyika ni moja katika ukoloni mamboleo

Waafrika tuna shida nyingi sana. Sasa kufuata syllabus ya Tanganyika ni ukoloni mamboleo na kufuata ya Oxford je? Mbona wasifuate tu yao waliyotengeneza wenyewe? Kwani hawajiamini?
 
Waafrika tuna shida nyingi sana. Sasa kufuata syllabus ya Tanganyika ni ukoloni mamboleo na kufuata ya Oxford je? Mbona wasifuate tu yao waliyotengeneza wenyewe? Kwani hawajiamini?
Elimu ya Zanzibar imeshuka kwasababu ya kufata mfumo wa Elimu wa Tanganyika,bora ukoloni mambo leo ya taifa lilioendelea kuliko ukoloni mambo leo wa Taifa lisilojijua
 
Back
Top Bottom