Tanzania visiwani waomba msaada wa walimu toka Nigeria, wakati Bara kuna walimu hawana ajira

Tanzania visiwani waomba msaada wa walimu toka Nigeria, wakati Bara kuna walimu hawana ajira

Mbona kuna waalimu ngazi ya degree (science) mtaani huku bara?? Wanatumia gharama kubwa wakati Tanganyika wapo imekuaje! Sijafanya utafiti wa kutosha ila mtaani kwangu wapo waalimu wanaotafuta kazi
 
Umeandika wazanzibari hawajitambui. siamini hivyo mimi hata kidgo. kuna sababu ya haya yanayotokea. Kikwazo kikubwa kinatokana na uendeshaji wa muungano huu kwa kudhibiti kila kitu mojawapo ni hiyo issue ya mafuta na masuala mengine. Nishati ya mafuta mpk leo hii ni suala lililoingizwa ktk orodha ya mambo ya muungano kinyemela kinyume na ridhaa ya wazanzibari.

Sasa unataka tujitambue vipi kwa kuwa Znz haiwezi ukafanya hata utafiti wa kuangalia mafuta kama yapo mpaka ipate kibali kutoka kwa mkoloni Tanganyika seuze kuyachimba? Zaidi ya hayo, issue za maamuzi ya kimkakati ambayo labda yangeitoa znz ktk umasikini yanadhibitiwa na mkoloni, yaani kitu rahc hakifanyiki mpaka mkoloni T/ bara atoe kibali hata cha kukohoa au kujamba ushuzi unaonuka. Znz inakwazwa kwa kutokuwa na nguvu na uwezo wa maamuzi ( legitimacy ya kufanya maamuzi na nchi / taasisi nyengine za kimataifa), kwa mfano, inapotaka kuomba msaada ama wa fedha/ kifundi ikiwemo kukopa, kuomba msaada, lazima ipitie kwa Wizara ya mambo ya nje / Wizara ya fedha ya T/ Bara kwa vitu vidogo tu na pengine na hapo nasikia huwa kuna vikwazo kedekede. Ni ukoloni ktk uhalisia wake.
Nafikiri solution ya matatizo haya ili Zanzibar tujitambue ni kuijtoa ktk muungano kwa minajili ya kuwa na mamlaka kamili bila ya kupitia kwa mtu wa kati ( middle man- T/ Bara ). Vyenginevyo, tutaendeleza business as usual bila ya natija yoyote.
Mkuu naona kama umejichanganya,hii comments yako ndio inaonyesha kabisa kama hamjitambui...Kwanini mnawachia Watanganyika wakuamulieni!,kwanini pale watu wenye mawazo ya kuiondoa Zanzibar kweye mashaka mnawabeza,mfano aliekuwa Mwanashria mkuu wa Zanzibar,huyu jamaa anaigombania sana Zanzibar lakini matokeo yake anapuuzwa tu na wazanzibar,hawamuungi mkono..

Zanzibar ina katiba yake kwanini,hamtumii katiba yenu kujitoa kwenye huu Mungano,Mungano ambao nchi mbili haziwezi kuuziana Sukari.,Haya mambo yote yanayofanywa na Watanganyika kuhusu Zanzibar ni wazanzibari wenyewe wanaruhusu wafanyiwe...,

Kijani, hapo ndio solution..itakuwa sio Mungano wa kwanza Afrika kuvunjika.Senegambia,Muungano wa Senegali na Gambia umevunjinga,Carpe Vade na Guinea umevunjika,sembuse UK imejitoa katika Muungano wa Ulaya..

Kama hakuna maslahi ya nchi na wananchi, Mungano wa nini!???..Mbona Sultani aliweza kuiweka Zanzibar juu,kulikuwa na msemo unaosema" ngoma ikipigwa Zanzibar husikika Afrika nzima",huo ndio ulikuwa umuhimu wa Zanzibar,chochote kilichofanyika Zanzibar kilikuwa muhimu kwa Afrika nzima
 
Mbona kuna waalimu ngazi ya degree (science) mtaani huku bara?? Wanatumia gharama kubwa wakati Tanganyika wapo imekuaje! Sijafanya utafiti wa kutosha ila mtaani kwangu wapo waalimu wanaotafuta kazi
Kwanini mnatumia gharama kubwa kuagiza Sukari kutoka Brazil wakati Zanzibar ipo..
 
Si mara ya kwanza kwa walimu wa masomo ya sayansi kutoka Nigeria, Zanzibar na Nigeria wana urafiki unaowafanya walimu kwenda kujitolea kufundisha. kuna watu wameanza kupotosha kuwa kwanini hawajaomba bara wapeleke walimu , bara yenyewe hakuna waalimu wa kutosha. Mi naona ni sahihi tu kwa kuwachukua hao wanigeria na cha maana ni kuwahamasisha Wanafunzi wachukue masomo ya Sayansi ili mwisho wa siku tupate walimu wakudumu wakufundisha ktk shule zetu.
 
Acheni kuingilia mambo ya Nchi huru..
 
Hongera Zanzibar mwanzo mzuri.
Safi sana na pia waalimu wa Kiingereza waajiriwe ktk shule za serikali toka nchi jirani za Malawi, Zambia, Zimbabwe ili changamoto ya lugha hii ya Kimataifa huku Tanganyika na Zanzibar iishe. Tuna wachezaji soka toka nchi hizo Tanzania vipi tuweke vikwazo ktk elimu?

Baada ya muda wa mpito kuajiri wageni kupita, pia waalimu wa Kiingereza, masomo ya sayansi na hisabati watapatikana toka humu humu Tanganyika na Zanzibar.
 
Hivi hawa wazanzibari hawana washauri kweli? Kuna walimu gani Nigeria? Wanigeria hawazungumzi kiingereza vizuri na hata kama watazungumza hawaeleweki wanaongea nini. Hiki ni kichekesho kingine kwa serikali ya Zanzibar.
hujasoma sayansi wewe na nyie mnahangaika na kiingereza cha kwenye filam in Nigeria .Soyinka nina mwelewa vizuri kiingereza chake spoken and written msioongee mambo ya kwenye maigizo mkayaleta hapa!intelectual yupi wa nigeria unayeweza kumtolea mifano zaidi ya wasanii wa kinigeria tu katika ufasaha wa kiingereza?
Waacheni wazanzibari wajinusuru kieleimu nyie endeleeni kufanya kampeni wtoto wetu wa liopitia private hakuna kuingia chui
 
Majority ya Nigerians hawajuwi kiingereza kivile, usibabaike na baadhi yao waliowahi kuishi nje. Walimu wao huko kwao ni majanga, watazungumza kiingereza ila hawaeleweki. Shauri yenu.
 
Serikali ya Zanzibar imeagiza zaidi ya waalimu 300 wa masomo ya Sayansi kutoka nchini Nigeria ambao tayari wameanza kuwasili visiwani humo.

Kwa mujibu wa serikali ya Zanzibar, waalimu hao wanaoingia kwa awamu, na wanatarajiwa kuziba pengo la uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 wa masomo hayo.

Katika mahojiano maalum na BBC naibu waziri wa Elimu Zanzibar Mmanga Mjengo amesema ujio huo utasaidia kuamsha pia morali ya waalimu wengine wa masomo ya sayansi visiwani humo

Mimi kama Britannica sioni mantiki.

======

Katika mahojiano maalum na BBC naibu waziri wa Elimu Zanzibar Mmanga Mjengo amesema ujio huo utasaidia kuamsha pia morali ya waalimu wengine wa masomo ya sayansi visiwani humo.

Ameongeza pia wameamua kwenda mchini Nigeria kwa sababu kuna wingi wa waalimu na wenye ubora na haikuwa rahisi kuchukua kutoka nchi za karibu kwa sababu na wao pia wana tatizo la uhaba wa waalimu.

''Mchakato wa upatikanaji wa waalimu hawa hufanywa kwa kutegemea uwezo wao katika ufundishaji na pia ubora wa kazi zao.'' alisema waziri Mjengo.

Serikali ya Zanzibar imesisitiza kuwa sio mara ya kwanza kwa ujio kama huu kwani katika miaka ya nyuma waalimu hawa wamekua wakija kwa kujitolea.

Ujio wa waalimu hawa ambao watakuwepo kwa kipindi cha miaka miwili unatajwa kupunguza uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 visiwani humo.

Zanzibar yaagiza waalimu wa sayansi kutoka Nigeria
Tuwe wakweli jamani,mfumo wetu wa elimu ni duni sana,una tengeneza wahitimu vihiyo mno,hata ningekuwa mimi nisingewachukua.
Halafuu, mmesahau kwamba mmekataa kununua sukari yao?Wale ni wazee wa jicho kwa jicho bwana.
 
Wanageria walivyo tapeli katika hao 300 sidhani kama kuna hata mmoja aliyefika high school.
 
Hivi hawa wazanzibari hawana washauri kweli? Kuna walimu gani Nigeria? Wanigeria hawazungumzi kiingereza vizuri na hata kama watazungumza hawaeleweki wanaongea nini. Hiki ni kichekesho kingine kwa serikali ya Zanzibar.
Maguful kasema kusoma sio lazima ujue kiengereza
 
Serikali ya Zanzibar imeagiza zaidi ya waalimu 300 wa masomo ya Sayansi kutoka nchini Nigeria ambao tayari wameanza kuwasili visiwani humo.

Kwa mujibu wa serikali ya Zanzibar, waalimu hao wanaoingia kwa awamu, na wanatarajiwa kuziba pengo la uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 wa masomo hayo.

Katika mahojiano maalum na BBC naibu waziri wa Elimu Zanzibar Mmanga Mjengo amesema ujio huo utasaidia kuamsha pia morali ya waalimu wengine wa masomo ya sayansi visiwani humo

Mimi kama Britannica sioni mantiki.

======

Serikali ya Zanzibar imeagiza zaidi ya waalimu 300 wa masomo ya Sayansi kutoka nchini Nigeria ambao tayari wameanza kuwasili visiwani humo.

Kwa mujibu wa serikali ya Zanzibar, waalimu hao wanaoingia kwa awamu, na wanatarajiwa kuziba pengo la uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 wa masomo hayo.

Katika mahojiano maalum na BBC naibu waziri wa Elimu Zanzibar Mmanga Mjengo amesema ujio huo utasaidia kuamsha pia morali ya waalimu wengine wa masomo ya sayansi visiwani humo.

Ameongeza pia wameamua kwenda mchini Nigeria kwa sababu kuna wingi wa waalimu na wenye ubora na haikuwa rahisi kuchukua kutoka nchi za karibu kwa sababu na wao pia wana tatizo la uhaba wa waalimu.

''Mchakato wa upatikanaji wa waalimu hawa hufanywa kwa kutegemea uwezo wao katika ufundishaji na pia ubora wa kazi zao.'' alisema waziri Mjengo.

Serikali ya Zanzibar imesisitiza kuwa sio mara ya kwanza kwa ujio kama huu kwani katika miaka ya nyuma waalimu hawa wamekua wakija kwa kujitolea.

Ujio wa waalimu hawa ambao watakuwepo kwa kipindi cha miaka miwili unatajwa kupunguza uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 visiwani humo.

Zanzibar yaagiza waalimu wa sayansi kutoka Nigeria

Nimewaelewa kuwa hawana uwezo wa kuajiri wazawa kwa kuwa watahitaji mikataba ya muda mrefu. Lakini si watangaze tu kuwa kazi ni ya mkataba waone kama hawatapata walimu wenye sifa?
 
Mimi ni mwalimu, nimejitahidi kuajiri na kutafutia baadhi ya walimu kazi, kwakweli inatia huruma Tasnia hii ya Elimu kuwa na graduates wengi sana. Au Ualimu ni chaka? kwamba umeshindwa fani zingine au ulikuwa kilaza kwahyo unakimbilia ualimu?

Nashauri watoto wenu mnaowasomesha waamulieni Taaluma zenye maslahi, sio kwasababu anapenda ualimu basi umlipie Chuo asome ualimu halafu aje kukosa kazi na kutangatanga. Kuna fani nyingi sana. Supply ikiwa kubwa Demand inapungua, ndio maana hata Serikali inaelemewa imuajiri nani imuache nani.
 
Akutukane tu wewe kwa upumbavu wako. Je ni uvivu wa kufuatilia mambo ama ni uwezo duni wa kuelewa? Serikali ilinunua Sukari Brazil kwa sababu ya ndani haitoshi kama ilivyo ya Zanzibar kutotosheleza mahitaji yao.
Hata hivyo, Serikali ilipozuia sukari ya nje, Wazanzibar wenyewe waliendelea kununua ya Brazil ya bei ya chee ambayo ikifika Zanzibar inauzwa haraka kuliko ya kwao inayotengenezwa Mahonda, Unguja Kaskazini. Hali hiyo imepelekea sukari ya Makonda kutonunulika visiwani humo na hivyo kutaka kuuza huku Bara.
Sasa, kama wao Wazanzibar hawalindi Kiwanda chao, wanaingiza Sukarno ya nje bila mipango maalum, unataka nani awalindie. Wao walitegemea kufanya biashara ya magendo watuuzie huku Bara sukari nyingi wanayonunua toka Brazil huku wakitudanganya kuwa ni ya Zanzibar.
Weye kwani shida yako nini kununua sukari bei chee, kumuunga mkono magufuli wa viwanda na kufa njaa . Hebu fikiri sukari inatoke brazil inalipiawa ushuru na bado rahisi kuliko hio ya magufuli . Sasa hujionei huruma
 
Hiyo inaitwa piga nikupige ukitaka huu wenzio wanataka ulee,tushirikiane kwenye mambo ya vifaru tu ukisikia zanzibar kuna chokochoko pelekeni vifaru na magari ya deraya mambo mengine hapana,lakini la pili,kwani hao waalimu wenu wanajua lugha iliyokuja na hayo masomo???si mnafundishia kiswahili??teh,teh,teh,teh zanzibar haijapenda.....
 
Back
Top Bottom