Tanzania ya enzi hizo katika picha
inasikitisha sana, maana naona kama zamani tulikuwa na akili, busara nyingi zaidi kuliko sasa, mazingira yalikuwa masafi sana, sababu ni nini? ongezeko la watu au kuondoka kwa mzungu?
 
Tanzania ambayo haikuwa na mafisadi.

 
Last edited by a moderator:
Kitabu kilichoandikwa na mwandishi wa habari na mwana-sanaa Freddy Macha. Kilitoka mwaka 1984.

covermachafreddy1.jpg
 
shule enzi hizo zilikuwa zinaruhusu vimini na afro? naona wadada wa kisutu walivyotokelezea

hilo jengo seaview, mawingu house lipo hadi leo. niliwahi kuishi maeneo hayo, tulikuwa tunaliita air india, tulikuwa tunaenda kuchezea lift tulipokuwa wtt
 
Hiyo style ya vidole viwili kama wanavyoonyesha wasichana wa Kisutu iliitwa LOVE and PEACE
 
USAFIRI DAR-ES-SALAAM
attachment.php

Hii ni Isuzu ELF 250. Hivi vibasi vilikuwa ni roho ya paka, sio hizi Eicher, aka maboksi,wanazotuletea sasa. Halafu dereva ndiye huyohuyo aliyekuwa kondakta. Watu walikuwa na nidhamu, wanapanda, wanalipa nauli, ndio wanakaa au kusimama.
 
Hii ni Isuzu ELF 250. Hivi vibasi vilikuwa ni roho ya paka, sio hizi Eicher, aka maboksi,wanazotuletea sasa. Halafu dereva ndiye huyohuyo aliyekuwa kondakta. Watu walikuwa na nidhamu, wanapanda, wanalipa nauli, ndio wanakaa au kusimama.

Hapa ni posta ya zamani dsm, nimeogelea hapa miaka ya 80 mwanzoni. Sasa ni aibu tupu!
Mkùu ni bora siku hizi kuliko enzi za awamu ya tatu siku hizi maendeleo yanaonekana barabara zinajengwa tena za lami na njia za mabasi yaendayo kwa kasi. Hongera Tanzania. Mola ibariki nchi yetu.
 
Musoma ndo haibadilikikabisa labda tofauti ni kwamba hiyo barabara now in lami ila majengo yako hivyohivyo japo yote yana nembo ya shirika la nyumba la taifa
 
Back
Top Bottom