Lakini wale ambao ni vizazi vya watawala hawaoni shida ya gharama kuwa ni kubwa, kwa sababu gharama wanaimudu vizuri.
Upande mwingine, wale waliokuwa vizazi vya wakuu wastaafu wa majeshi ya MAGEREZA, ZIMAMOTO na kidogo POLISI walikuwa wanatumia nafasi za ubalozi katika ile namna ya kupeleka watoto wao kwenda kushiriki katika michezo mbalimbali.
Pia walikuwa wanapata fursa ndogo kutoka ubalozini, ili wapate namna ya kuishi kwa kupata kipato kidogo kutoka ubalozini.
Kazi waliyokuwa wakifanya kama
"PARTY TIME JOB" ilikuwa ni kukagua na kuhakiki miradi ya serikali kupitia ofisi ya kibalozi katika mataifa mbalimbali walipokuwa wakiishi.
Kile kitendo kiliwashitua watu wengi wa kipindi kile cha miaka ya tisini [1990's], maana kukagua na kuhakiki miradi ya serikali inatakiwa kufanyika na taasisi, siyo watoto wa wastaafu wakuu wa majeshi!
Zamani, kipindi cha HAYATI MWALIMU kazi ya kukagua na kuhakiki miradi ya serikali kwa upande wa nje ya nchi ilikuwa inafanyika na wenyeji wa asili wa KIJIJI CHA NINDO tu!
Lakini baada ya 1975, kazi ya kuhakiki na kukagua miradi ya serikali kwa upande wa nje ya nchi ilikuwa inafanyika na watoto wa wakuu wastaafu wa majeshi, kitu ambacho kiliitia dosari serikali ya MZEE RUKSA na ilileta mpasuko mkubwa ndani ya MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA [1985-1995].
Wao walikuwa wanasema
"watoto wa nyoka ni nyoka" na waliona ni sawa kwa watoto wa wakuu wa majeshi kukagua na kuhakiki miradi ya serikali kwa upande wa nje ya nchi na waliendelea kufanya hivyo, hata baada ya UTAWALA WA AWAMU YA TATU [1995-2005] ulivyoingia madarakani.
Tunaambiwa hata hiyo kampuni ya AXA ni kampuni inayomilikiwa na serikali kupitia ubalozi wa TANZANIA unaopatikana nchini UINGEREZA na walikuja kufanikiwa kufungua kiwanda cha kutengeneza dawa za kutibu binadamu [DINOPAT] kinachopatikana nchini INDIA. Hiyo kampuni ilikuwa inaitwa AXA PARENTERALS LIMITED..
Kwahiyo kwa kipindi chote hicho, wale watoto wa wakuu wastaafu wa majeshi walikuwa wanaishi kwa namna hiyo na waliamini wao ndiyo wenye SERIKALI YA TANZANIA kutokana na kufanya shughuli ya kukagua na kuhakiki miradi yote ya serikali inayopatikana nje ya nchi.
Watoto wao walikuwa wanaishi kwa namna hiyo na ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya wale wakuu wastaafu wa majeshi kupeleka watoto wao nje ya nchi kutokana na kazi ya kukagua na kusimamia miradi ya serikali inayopatikana nje ya nchi. Ijapokuwa walikuwa hawana vigezo!