Tanzania ya sasa ni ile aliyoiona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Tanzania ya sasa ni ile aliyoiona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

WANAMICHEZO wengi wenye asili ya kiafrika huwa wanaenda kushiriki michezo katika MATAIFA YA MAGHARIBI kwa nia ya kupata uzoefu wa kuja kusaidia mataifa yao katika michuano ya kimataifa na kombe la dunia.

Kule MATAIFA YA MAGHARIBI kuna michuano mingi na presha ya mashabiki ipo juu kulinganisha na MATAIFA YA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA. Hivyo inasaidia kuwajengea uwezo wanamichezo kujiamini wanapokuwa uwanjani.
Wale wakuu wa majesh walikuwa wanawaiga marais na machifu wa kpindi kile, ijapokuwa hawakuwa na hela yoyote ya kupeleka watoto wao ulaya. Nindo ndo walikuwa wanapigia hela huko kwenye mirad ya nje.. 🙏🏽
 
Miaka ile kpindi Mrema yupo hot iliibuka hii skendo, wanamichezo walienda kukagua na kuhakiki kiwanda cha kutengeneza dawa za kutibu binadam..

Walienda India na walilipwa pesa ndefu, wakasepa hata hawakuwa wafamasia! Ila ndo huwa wanaish kwa namna hiyo huko Ulaya..

Ilikuwa ni skendo kubwa na wachezaji walioenda kule India walikuwa na majina makubwa katika soka la ulaya. Lakin walikuwa hawana hela..

Hadi watoto wa kike waliozaliwa kpindi hicho walipewa jina la AXA, ikiwa na maana ya kampun ya kutengeneza dawa za kutibu binadam inayopatikana India..

Saivi hawana ishu hao diaspora, kuna mataifa kama Rwanda, Burundi, Msumbiji na Malawi ambao wanaweza kufanya hyo kaz ya kukagua mirad ya serikali.. 🙏🏽
a5c3f8cb31c8821d0c3f1ad843b06824.jpg

​
Wenzenu walijaribu kuishi maisha na mtindo wa kimagharibi na walifanikiwa, ijapokuwa hawakuwa na fedha za kutosha ili kukamilisha masuala yao.

_20260423_200103.JPG

Tunaambiwa wale wastaafu wakuu wa majeshi walikuwa wanatumia gharama kubwa katika kufanikisha ndoto za watoto wao kuwa wasanii wa nyimbo na kucheza mpira wa miguu, ulaya!

Kumbe ulaya, idadi kubwa ya wanamichezo huwa wanatoka kwenye MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA na huwa wanaandaliwa na serikali kwa ajili ya kushiriki michuano ya kimataifa na kombe la dunia.

1709748f5d132b6fc2caf4c1cc39b6c9.jpg

Wale waliokuwa MAWAZIRI kipindi cha miaka ya tisini [1990's] waliamua kuvumilia na kujijenga kiuchumi. Sasa hivi wanamiliki timu za mpira wa miguu katika BARA LA ULAYA!

458668a1e0a10ad2ab14ca64e1068066.jpg

FC SCHALKE 04 imebakiza michezo miwili au mitatu kupanda LIGI KUU YA UJERUMANI, BUNDESLIGA na inamilikiwa na WATANZANIA.
 
Tangu nipo shule ya msingi tulikuwa tunaaminishwa kwamba Mwl Nyerere ndio "icon" pekee hapa nchini, tulikuwa tunaimba nyimbo nyingi ni za kumsifu, lakini hatukuwahi kuambiwa kuwa kuna watu wengine ambao bila wao mwalimu "asingetoboa" na pengine tusingemjua kabisa mwalimu Nyerere, au story yake ingekua "short lived". Mmoja wa hao watu ni OSCAR KAMBONA.

Nimezaliwa hapa Tanzania miaka ya 90 mpaka nimekua mtu mzima kila kitu ni Nyerere tu. Kambona nilimsikia baadae sana baada ya kusikia kisa cha huyu mtu nikawa interested sana kufuatilia stories zake.

kwa mujibu wa maandiko Kambona alikuwa bega kwa bega na mwalimu ktk kudai uhuru yaani ilikuwa akitoka mwalimu anaefuata ni Kambona lakini huwezi sikia hichi kitu kinasemwa waziwazi na pengine bila mawazo na support ya Kambona mwalimu "angefeli vibaya mno".

Kambona ndio mtu aliezima mapinduzi yalioilenga serikali ya Nyerere kutoka kwa askari waliotaka kuasi, yaani kwa ufupi ni kwamba Nyerere asingeendelea kuwa mtawala wa nchi hii kama sio Kambona.

Kambona aliona mbali kuliko mwalimu Tanzania ya sasa ndio aliyoiona Kambona lakini mwalimu alipinga, Kambona aliona ubepari ndio utafanya kazi lakini mwalimu aliona ujamaa ndio unafaa, mwalimu "failed miserably" akatupeleka chaka mpaka leo we still pay for his "grave mistake".

Mwalimu alikuwa mbishi na aliamini kwamba yeye ndio ana maono bora kuliko wengine, chochote kile ambacho kilikuwa hakiendani na sera zake alikipinga hata kama kilikuwa "viable".

Fikiria mtu mmoja tu kaenda Urusi akafurahishwa na mfumo wa ujamaa akaja kuufanyia "experiment" hapa nchini na ukafeli kwa sababu alikataa kusikiliza maoni ya watu wengine, kwa wakati huo mwalimu ndio alikuwa "kila kitu".

Kambona akatofautiana na mwalimu , yeye alitaka ubepari mwalimu alitaka ujamaa. Kutokana na ushawishi mwalimu alishinda japo Kambona ndie aliyekua sahihi lakini hawakumskiliza.

Baadae mwalimu alijua amekosea akaturudisha kwenye Ubepari na bado akaonekana ni "hero" . Kitu ambacho Oscar alikiona miaka kadhaa kabla wakati huo mwalimu alikuwa "blind" almost everyone was blind except the very few including Kambona.

Haya leo 2021, TZ hii ya leo ndio Kambona aliyoiona na tumechelewa sana, kwa mtazamo wangu bado tupo nyuma kwa miaka 15 kutokana na sera mbovu Mwalimu nyerere.

Wote ni marehemu wapumzike kwa amani lakini, mwisho wa siku Oscar Kambona ndio AMESHINDA!!!!! Kwangu mimi shujaa wa kweli nchi hii ni OSCAR KAMBONA na sio mwalimu! Na ndio mtu muhimu sana sawa na mwalimu lakini ndio aliesahaulikia kuliko wote nchi hii

Natamani Watanzania wengi tuliozaliwa miaka ya 90 tujue habari za huyu shujaa ambaye ni co-founder wa hii nchi kwangu mimi alichangia 50% ktk kutengeneza taifa hili sawasawa na mwalimu, yaani ni kama vile "stive wozniak na stive jobs", steve jobs alitumia akili za stive wozniak na credit akajiapa yeye mwenyewe

Aliyeweka Nyerere day kama public holiday alitumia vigezo gani ilihali si kweli kwamba Nyerere ndie mtu pekee aliepigania uhuru wa nchi hii

Ukiniambia nichague kati ya Nyerere na Kambona itakua ni Kambona always

UPDATE:
Watu wengi kwenye comments wanasema kwamba ujamaa ulituleta karibu, lakini ujamaa huohuo ndio uliotuletea umaskini, kwa hiyo logic yake ni kwamba mwalimu alichagua umaskini na umoja dhidi ya maendeleo ambayo hatuna uhakika kama yangetugawa, lakini kabla ya yote Kambona alimshauri kwamba kabla ya ku adopt ujamaa tuufanyie kwanza majaribio , tutengeneze vijiji vichache ambavyo vitaishi kijamaa ili tuone hii system itafanya kazi lakini mwalimu alikataa akaiingiza moja kwa moja bila kujua risks zake ni nini kitu ambacho kambona alishakiona

"Oscar Kambona was one of the best presidents Tanzania never had"
refence:

====

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!!

Christopher Makwaia

WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.10.jpeg

1. Usuli
Jioni ya Ijumaa ya tarehe 13.8.1925, huku mvua kubwà na radi kali zikirindima kijijini Kwambe, wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma, alizaliwa mtoto wa kiume akiwa buheri wa afya. Wazazi wa mtoto huyo, Rev. DAVID KAMBONA na Bi. MARIAM KAMBONA, wakampa mtoto huyo jina la OSCAR SATHIEL DAVID KAMBONA. Mvua na radi hiyo, kwa mujibu wa mila za kijijini hapo, "nyumbi hii, bombi hii", ilikuwa ni baraka na ishara kuwa mtoto huyo atakujakuwa wa kipekee.

2. Elimu Chini ya Mwembe
KAMBONA, tofauti na watoto wengine, hakusomea shuleni elimu ya awali bali alifundishwa na wazazi wake pamoja na mjomba wake ambao wote walikuwa walimu. Mafunzo hayo ya awali yalikuwa yakifanyika chini ya mwembe huku chai na mihogo vikiwa pembeni.

3. Elimu ya "Middle School"
Baadae KAMBONA alipelekwa shule ya Kati ya Mt. Barnabas, Liuli. Akiwa shuleni hapo, KAMBONA alikuwa kipanga na "aliwatimulia vumbi" wanafunzi wote kwa miaka yote alipokuwa shuleni hapo.

4. Alliance Sec. School
KAMBONA alifaulu vizuri mitihani yake na akachaguliwa kujiunga na "Alliance Sec. School", Idodomia ambayo baadae ikajaitwa Mazengo Sec. School. Almanusra KAMBONA asiendelee na masomo kwani baba yake hakuwa na uwezo wa kulipa £ 30 kwa mwaka. Uwezo wa KAMBONA "kutema yai" ndio uliomponya kwani alifanikiwa kumshawishi Askofu kumlipia ada hiyo baada ya kusali Sala ya Baba Yetu kwa Kiingereza!.

5. Tabora Boyz Sec. School
KAMBONA alisoma shule hii pamoja na J. Lusinde, E. Mzena, B. Ngwilulupi, A. Nsekela, A. Nyirenda na K. Chiume. Ni akiwa shuleni hapo ndipo kwa mara ya kwanza, KAMBONA alionana na NYERERE aliyekuwa akifundisha St. Marys, Tabora.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25281%2529.jpeg

6. Ualimu Alliance Sec. School
Baadae, KAMBONA alienda kufundisha shule hii na akakutana na J. Lusinde na K. Chiume na baadae akawa "Schoolmaster".

7. KAMBONA akutana na NYERERE tena
KAMBONA alikutana na NYERERE kwa mara ya 2 kwenye Mkutano wa taifa wa waalimu mwaka 1954.

8. KAMBONA Ajiunga TANU
Mwaka 1955, KAMBONA alijiunga na TANU iliyozaliwa tarehe 7.7.1954 na akaonesha bidii kubwa huku akifanya kazi kwa kujitolea kwani TANU haikuwa na fedha. Bidii yake ilipelekea kuwa Katibu Mkuu wa TANU.

9. KAMBONA Awaingiza TANU Watanganyika 100,000
KAMBONA alitembea nchi nzima kwa miezi 6 akionana na Machifu na wanavijiji na kufanikiwa kuingiza wanachama 10,000. Baadae akiendelea na harakati hizo na baada ya miezi 12 akawa ameingiza wanachama 100,000. Viongozi wenzake wa TANU walimpongeza sana kwani TANU ikawa inaenea kwa kasi sana.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25282%2529.jpeg

10. KAMBONA Afungua Akaunti ya Kwanza ya TANU
KAMBONA alikuwa na mawazo ya kimaendeleo kwani kutokana na michango ya wanachama aliweza kufungua akaunti ya kwanza ya TANU. Kwa hakika, hili lilikuwa ni jambo la kihistoria.

11. KAMBONA afuma "Governor's Scholarship" kusomea Sheria, UK
Mwaka 1957, KAMBONA alipata fursa ya kwenda UK kusomea LLB kwa miaka 3 na hivyo akaenda huko.

12. KAMBONA Awa Mtangazaji wa 1 wa Kiswahili BBC 1957
Tarehe 27.6.1957, KAMBONA aliweka historia kwa kutangaza Kiswahili BBC kwa mara ya 1 akisema-: "Hapa ni London, kwa mara ya kwanza BBC inawaletea habari kwa Kiswahili wananchi wa Afrika Mashariki. Asalaam Aleikhum".

13. KAMBONA awa Mwenyekiti wa TANU London
Kutokana na talanta yake kubwa ya uongozi, KAMBONA alichaguliwa kuwa Kiongozi wa wanafunzi chuoni na Mwenyekiti wa Tawi la TANU, London.

14. KAMBONA na NYERERE Washeachumba Chuoni London
Kati ya tarehe 26.6.1959 na 7.8.1959, NYERERE alikwenda UK kwa matayarisho ya uhuru wa Tanganyika na akalala chumba kimoja na KAMBONA ambaye walikuwa "wameshibana" sana. Katika "Press Conference" ya 1991 KAMBONA alisema- "TANU haikuwa na hela hivyo ili kubana matumizi, nikakaa na NYERERE room yangu chuoni na hii ilisaidia tuwe na muda mwingi wa majadiliano".

15. KAMBONA Amuoa MISS Tanganyika
Tarehe 19.11.1960, KAMBONA alimuoa Miss Tanganyika mrembo, Bi. FLORA MORIYO toka Kilimanjaro. Harusi hiyo ya kukata na shoka ilifanyika St. Paul Cathedral, London na kuhudhuriwa na wageni waalikwa 400. NYERERE alikuwa ndiye msimamizi aliyemsindikiza Bi. FLORA altareni. Ilikuwa ni harusi ya kwanza ya watu weusi kanisani hapo na ilitoka kwenye magazeti mbalimbali ya Ulaya.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.12.jpeg

16. KAMBONA Arejea Bongo
KAMBONA alirejea Bongo kuendelea na harakati za uhuru akihudumu kama Waziri wa Elimu na Katibu Mkuu wa TANU.

17. KAMBONA Awa Waziri wa 1 wa Mambo ya Nje
Katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Tanganyika, KAMBONA aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi.

18. KAMBONA Kipenzi cha 2 cha Wananchi baada ya NYERERE
KAMBONA alipendwa sana nchini kwani alikuwa msomi, mwanasiasa hodari, mtanashati na vijana wengi walimuiga staili yake ya nywele "KAMBONA Style". Kwa hakika, KAMBONA alipendwa sana.

19. KAMBONA- Kiongozi PEKEE Aliyewakabili Waasi, 1964
Usiku wa tarehe 19.1.1964, askari wa kambi ya Colito(Lugalo) waliasi wakidai marupurupu na nafasi za juu za vyeo kwa Waafrika. Rais NYERERE na Mh. RASHID MFAUME KAWAWA walitoroshwa na mlinzi wao, PETER BWIMBWO usiku wa manani hadi Kigamboni na kufichwa kwenye nyumbaya Mzee KIZWEZWE.

Mawaziri wote walibanisha makwao baada ya kupigiwa simu na Mh. J. LUSINDE, Waziri wa Mambo ya Ndani, kuhofia usalama wao. KAMBONA ndiye pekee aliyeingia "fronti" kwani si tu raia waliokuwa wakimpenda bali pia askari. Waasi walionekana kutulia baada ya mambo yao kuwekwa sawa lakini baada ya Rais NYERERE kuibukia Ikulu toka mafichoni baada ya siku 3, waasi "wakalianzisha" tena hivyo ikabidi maasi hayo yalizimwe kwa msaada wa Waingereza na baadae Wanaijeria.

20. KAMBONA Ashuhudia mchakato wa Muungano 1964
KAMBONA alikuwa ni mmoja wa mawaziri wachache sana waliokuwa wakijua mchakato wote wa muungano kwa undani na pia alishuhudia utiaji saini hati za muungano huko Zenji, tarehe 22.4.1964 kati ya Rais NYERERE na Rais wa Zanzibar, Mh. ABEID AMAN KARUME.

21. KAMBONA Atofautiana na NYERERE Mfumo wa Chama Kimoja
Baada ya ziara ya China 1965, NYERERE alivutiwa na "alikuwaameoza" kwa siasa za China na mfumo wao wa siasa hivyo akaunda Tume tarehe 28.1.1964 ili ipendekeze mfumo gani unaifaa nchi yetu. Tume hiyo ilikuwa chini ya Mh. KAWAWA ikapendekeza mfumo wa chama kimoja. KAMBONA, ambaye daima alikuwa hapepesi macho wala hayumbishwi, aliweka kunji na kutosaini ripoti hiyo na badala yake akatayarisha ripoti yake ya kutaka mfumo wa vyama vingi na NYERERE akahuzunishwa sana na msimamo huo wa KAMBONA.

Kipindi hiki NYERERE aliishamuondoa KAMBONA kwenye wizara zile nyeti.

22. NYERERE "Amchana" kiaina KAMBONA 77 ya 1966
Tarehe 7.7.1966, NYERERE, akihutubia Taifa katika sherehe za 77, NYERERE alitumia mafumbo "kumpa za uso" KAMBONA ambapo alisema viongozi wanaonekana kujipatia mali nyingi kiajabu hawafai hata kidogo.

23. KAMBONA Ajiuzulu u-Waziri na U-Katibu Mkuu TANU 1967
Tarehe 9.6.1967, KAMBONA alibwaga manyanga kwa kujiuzulu U-Katibu Mkuu wa TANU na Uwaziri wa Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini ambapo alitaja sababu za kiafya kuwa ndizo zilipelekea achukue uamuzi huo.

24. KAMBONA Atorokea Kenya, 1967 ki-James Bond
Kwakuwa KAMBONA alikuwa ni mtoto wa mjini, alitonywa kwamba kuna mpango wa kumkamata na kumsweka kizuizini. Hivyo, usiku wa kuamkia tarehe 26.7.1967, KAMBONA, mkewe, watoto wake 2 na msaidizi wa kazi walifunga virago na ku-drive hadi Kenya kwa staili ya "James Bond"! Watu wengi walipigwa butwaa ni kwq vipi aliweza kutoroka bila kubambwa!.

Usiku wa siku hiyo jijini Nairobi, KAMBONA na familia yake walikwea "pipa" East African Airways Flight 720 kwenda "Kwa Mama, huku, huku nyuma ikadaiwa alitoroka na mamilioni ya fedha!.

25. NYERERE Aelezea "Kusepa" kwa KAMBONA
Siku chache baada ya KAMBONA "kula kona", NYERERE, akiongea na viongozi wa TANU Morogoro, alisema : "Itachukua muda mrefu kufahamu sababu za Bw. KAMBONA kujiuzulu, lakini jambo moja ni dhahiri; KAMBONA amenidanganya mimi, TANU, TZ na Afrika".

26. KAMBONA Ajitetea UK
Baada ya kusikia vijineno kwamba amesepa na mamilioni, tarehe 6.9.1967, KAMBONA alikanusha vikali na kuitaka serikali ya Tanzania iwasiliane na ya Kenya kupata uthibitisho kitu ambacho serikali ya TZ hakikufanyika.

27. OTTIN na MATTIYA KAMBONA "Wasukumiziwa Ndani", 1967
Hawa wadogo zake KAMBONA walionja "joto ya jiwe" kwani walinyakwa usiku tarehe 30.12.1967 na kuwekwa kizuizini, Ukonga. Familia zao zikasambaratika vibaya sana kufuatia kukamatwa kwao. OTTIN alikuwa ni "Journalist" na MATTIYA alikuwa mfanyakazi Wizara ya Kilimo. OTTIN alikuwa amemuoa raia wa Martinique na walikuwa na watoto 2 wadogo na MATTIYA alikuwa amemuoa Mgambia wakiwa na mtoto wa miezi 3 tu. Wanawake hao walifukuziliwa mbali na kurudishwa makwao pamoja na watoto wao!.

28. KAWAWA "Amchana" KAMBONA Bungeni, 1968
Jumanne ya tarehe 23.1.1968, KAWAWA, 2nd VP, alilitaarifu Bunge:
"Wote mnajua kwamba Bw. KAMBONA aliikimbia nchi mwaka jana, 1967. Kabla hajaondoka, tarehe 6.12.1966, TZS 500.000/= ziliingizwa kwenye akaunti yake toka benki moja ya Uingereza. Uchunguzi wa BOT toka KAMBONA atoroke umeonesha kuwa tangu Juni 1965 na Desemba 1966, KAMBONA aliingiza katika akaunti yake jijini Dsm TZS 896,800/=. Kambona pia alikuwa anamiliki majumba mengi (Nyumba Magomeni-Plot No. 21,39 31), (Kunduchi bichi-Plot No.28), (Msasani bichi -Plot No. 92), (Morogoro-Plot No. 89) ns (Songea-Plot No.21)".

29. KAMBONA Amchana NYERERE nchini Nigeria, 1968
Baada ya TZ kuitambua Biafra, serikali ya Rais YAKUB GOWON ilikasirishwa sana hivyo ilimwalika KAMBONA aichafue TZ . Kwahakika, "jipu likawa limepata mkunaji" Hivyo, KAMBONA akaenda na kutoa muadhara Lagos tarehe 14.6.1968 ambapo "alimchana" vilivyo Rais NYERERE na kumwita dikteta. KAMBONA akaonesha kukosa uzalendo kwa taifa lake pale alipozomoka, bila ushahidi, kwamba TZ imepeleka vifaa vya kijeshi Biafra badala ya Zimbabwe!.

30. TANU "Yamfyekelea mbali" KAMBONA
NEC ya TANU iliyokuwa ikiketi Tanga, tarehe 19.10.1968, ilimvua uanachama KAMBONA pamoja na wabunge wengine 8 "Vichwa-maji" waliohoji uhalali wa TANU kuwa juu ya Bunge. Wabunge hao ni W. Mwakitwange, M. Choga, S. Kibuga, J. Bakampenja, E. Anangisye, G. Kaneno na Dr. F. Masha.

31. NYERERE "Amchana" tena KAMBONA, 1969
Tarehe 12.1.1969 kwenye sherehe za Mapinduzi Znz, NYERERE "alimuwakia" KAMBONA na kusema- "KAMBONA ni mwizi na mhuni kisiasa.

32. KAMBONA Akejeliwa Mashuleni na Majeshini
Nyimbo nyingi za kumkejeli KAMBONA zilitungwa majeshini na mashuleni lakini zilizokuwa maarufu ni hizi 2:
1. KAOMBONA Kaolewa wapi....? Kwa Wazungu...Kisa nini?...Tamaa ya Mali!

2. Alimselema ...alija, akija KAMBONA chinja... chinjilia mbali..!

33. KAMBONA Adaiwa ni _"Mastermind"_wa Uhaini, 1969
Mwaka 1969, KAMBONA alidaiwa kuwa "Mastermind" wa uhaini. Mashitaka yalikuwa kwamba washtakiwa 7 wakishirikiana na KAMBONA kati ya Machi 1968 na Octoba 1969, walitaka kumuua Rais NYERERE na kuipindua serikali. Washtakiwa hao 7 ni (Bibi Titi Mohamed , Michael Kamaliza, Gray Mattaka, John na Eliya Chipaka, Capt A. Milinga na W. Chacha).

Kesi ilianza kurindima Jumatatu tarehe 6.6.1970 na ilisikilizwa na Jaji Mkuu Georges na iliendeshwa na AG Mark Bomani. Wanafunzi wa Sekondari Tambaza(F.V Arts akiwepo Othman Chande, Jaji Mkuu wa 7) walikuwa wakijongo vipindi kwenda kortin kushuhudia kesi hii iliyokuwa na mvuto wa aina yake.

Washtakiwa wote walitiwa hatiani kasoro A. Milinga na KAMBONA ambaye hakuwepo. M. Kamaliza na mwenzake walipigwa "mvua" 10 na wengine walifungwa maisha na Bibi Titi akapata msamaha 1972.

34. OTTIN MATTIYA Waachiwa 1978
Tarehe 5.2.1978, katika kusheherekea mwaka 1 wa kuzaliwa CCM, NYERERE, akitumia ibaracya 45 ya Katiba, aliwaachia huru OTTIN na MATTIYA pamoja na JOSEPH KASELABANTU(Mwasisi wa TANU). OTTIN na MATTIYA, baada ya kugundua familia zao hazipo, wakaona Bongo hamna ishu nao wakaamua pia kusepa. Walivuka mpaka wa TZ na Kenya usiku Kininja kwani mpaka huo ulikuwa umefungwa kutokana na uhasama bainavya TZ na Kenya na wakaelekea UK.

35. NYERERE NA KAMBONA walikuwa majirani Msasani
Baada ya KAMBONA kuondoka nchini 1967, nyumba yake ikawa inakaliwa na Rais MILTON OBOTE kwa takribani miaka 10 baada ya kupinduliwa na Nduli IDD AMIN, 1971.

36. Vyama Vingi vyaanzishwa Bongo, KAMBONA ataka kurejea
Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, KAMBONA akiwa London alisema, ije mvua, lije jua, anarejea kwenye Taifa lake. Serikali ikamuonya kuwa asithubutu na akijifanya fyatu au kichwa-maji akatia pua yake tu Bongo, "hakuna rangi ataacha kuiona".

37. KAMBONA Aitunishia msuli serikali, Atinga Bongo
KAMBONA aliamua kuwa kama "Mbwai, mbwai tu" hivyo akaonesha "Shoo za kibabe" na kurejea nchini akisafiria nyaraka za Umoja wa Mataifa zilizotolewa na serikali ya UK. Aliporejea hakukamatwa na badala yake, tarehe 4.9.1992, serikali ilimpa miezi 3 aweke sawa uraia wake kwakuwa ni Mmalawi! Miezi hiyo iliisha tarehe 4.12.1992 na serikali "ikaufyata" kwani haikumfanya kitu chochote!.

38. KAMBONA aeleza sababu za kutoroka, 1967
Baada ya kurejea nchini, KAMBONA alikata kiu ya wote waliotaka kujua kilichopelekea asepe "Kwa Mama" ni nini ambapo alitiririka: "Mimi na NYERERE tumetoka mbali. Sisi ndio tuliokuwa Viongozi wakuu wa TANU; Yeye Mwenyekiti, mimi Katibu Mkuu. NYERERE aliporudi toka China 1965 alitaka kuleta sera za China na mfumo wa chama kimoja. Nikapingana nae.."

39. KAMBONA Aeleza alichokuwa akifanya UK

Wiki 2 baada ya kurejea nchini, KAMBONA alitiririka kitu alichokuwa akifanya nchini Uingereza kwa miaka 25 aliyoishi huko ambapo alisema- "I did business. I used to go to the Arab countries but this did not last. I then depended on income support from Britain. Every Tuesday You take your book to the Post office...

40. KAMBONA atishia "Kumwaga ugali na mboga" kuhusu NYERERE
Badala ya kushugulikia uraia, KAMBONA akaendeleza bifu lake na NYERERE ambapo alisema anataka kufanya mkutano mkubwa viwanja vya Jangwani ili aeleze ufisadi wa NYERERE. Mapadri na masheikh walimsihi sana lakini akashikilia msimamo wake.

41. KAMBONA Ambwelambwela Jangwani, 1992
Tarehe 21.11.1992, viwanja vya Jangwani viliweka rekodi kutokana na umati mkubwa wa "wapenda ubuyu" uliojitokeza toka mida ya mchana kulisikia Jabali hilo litaeleza nini kuhusu Baba wa Taifa, Mwalimu NYERERERE.

KAMBONA aliwaboa sana 90% ya waliohudhuria kwani alidai, bila ushahidi, kuwa NYERERE, AMIR JAMAL na KAWAWA wameficha mamilioni ya fedha mabenki ya Ulaya. KAMBONA akaenda mbali na kudai NYERERE ni Mtutsi, KAWAWA na MKAPA ni watu wa Msumbiji na MALECELA ni Mcongoman!. Ikaonekana ni hekaya za Abunuwasi na hadithi za Esopo tu!

42. NYERERE Amjibu KAMBONA
NYERERE, siku chache baadaye akiwa Msasani, aling'aka- "Mimi ni lofa. I dont have a single penny abroad, I can assure you. Kama RASHID na AMIR hawawekwi kundi la watu waaminifu duniani, labda neno uaminifu ni neno tu, halina maana. Hawa ni waaminifu sana. Pia, mimi sipendi kuhusishwa na mambo ya kijingajinga. Ni makosa kushindana na kundi la wapumbavu. Kambona alete ushahidi maana "any blessed fool could stand up there" na kusema chochote".

43. MAWAKILI wamchimba Mkwara-Mbuzi KAMBONA
Baada ya KAMBONA kutoa kashfa dhidi ya viongozi hao mashuhuri nchini, mawakili wa Viongozi hao walimpa siku 14 toka tarehe 8.12.1992 kuomba radhi au kutoa ushahidi.

KAMBONA aliwajibu kuwa _"Mtu mzima hatishiwi nyau"_na akachekesha watu pale alipodai _"Nondo" zake kuhusu "bank accounts" za viongozi hao amezisahau UK!.

44. KAMBONA Aunda TADEA
KAMBONA aliunda chama cha TADEA ambacho hakikuleta upinzani wowote wa maana.

45. KAMBONA afariki London, 1997
KAMBONA alifariki jijini London mwaka 1997 na mwili wake kuletwa nchini na kupokelewa na ndugu zake na kiongozi wa serikali, Mh. J.M. KIKWETE, Waziri wa Mambo ya Nje. Rafiki yake NYERERE hawakuwahi kuonana toka atoroke mwaka 1967 na wala hakwenda kwenye mazishi yake.

46. RAIS KIKWETE Akutana na Mke wa KAMBONA, 2007
Tarehe 28.6.2007 katika hotel ya Kilimanjaro Kempisk, Rais wa awamu ya nne, Mh. JK alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 50 ya BBC KISWAHILI. Mh. JK, akiwa na mcheshi na mwenye bashasha kama kawaida yake, alikutana na kusalimiana na Bi. FLORA KAMBONA ambaye alikuwa mgeni mahsusi kwani mmewe, KAMBONA ndiye aliyekuwa Mtangazaji wa 1 wa BBC Kiswahili, 1957.

46. MWISHO:
Huyu ndiye OSCAR SATIEL DAVID KAMBONA aliyekuwa chanda na pete na Mwalimu NYERERE lakini mwisho wakawa maadui wasio na mfanowe!.

Tafakuri Tunduizi:
ATIKALI HII YA KUKATA NA SHOKA ina Tafakuri Tunduizi 100!!!

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!! - MICHUZI BLOG (issamichuzi.blogspot.com)

Oscar Kambona - Wikipedia

View attachment 1983785
kizaz cha sasa kimekuwa kivivu sn kutafit kinanendeshwa na ubuyu

Kambona anavuma sn ila hata kujieleza haez , Kambona alikuwa baba wa ufisad

Kama tusingepotoka na tungebakia kweny misingi ya Nyerere tungekuwa superpower kweny huu ukanda mzima

Kwasas rushwa , ufisad , ukiukwaj wa haki za binadam na ujinga mwing sn unaendelea ambao unafanywa kwa makusud kbs
 
Waliishia kumpaka matope.

View attachment 1665493
Thibitisha kama kwel alipakwa matope ? Tuambie kwann Nyerere alifanya yote hayo ? Je Nyerere alilinda nin akiwa madarakan?
Tuepuke kuweka udini ( Uislam na Ukristu ni ushoga tu na mtu unaetumia hz dini kujadili watu bas ww ni ms3ng tu maana bado akil yako imefungwa minyororo)

Nyerere ndo rais pekee aliibadili nchi yake
1.Kaleta umoja ( 98% ya marais wa kizaz cha Nyerere waliyavunja mataifa yao kwa kupendelea watu wao badala ya kujenga nchi zao ziwe moja )

2.Nyerere alisuka mfumo bora kbs wa elimu ambao ulimwandaa mtu kuyamudu maisha sio elimu ya leo inazalisha mashog magaw vnyeo mama Mwija...ku , mim nmekuwa mwl naelewa mapungufu yaliyopi kule , elimu imekuwa biashara , Nyerere alizuia hili aliifanya elimu kuwa huduma ya kijamii

3.Usalama ulikuwa juu san kipind hiko

4.Uwajibikaj kwa watumishi ulikuwa juu

5.Alisimamia viwanda vingi na kuviendeleza ila waliomfuata waliua viwanda vyote ili wao wakanunue bidhaa nje waje kutuuzia

6.Krb kila shule ilikuwa na kitega uchumi hadi usafir ambao leo vyot vimekuwa historia

7.Hakuwa omba omba kama viongoz wenu wa leo hadi kujenga vyoo vya shule mpk waombe ulaya
 
Wale wakuu wa majesh walikuwa wanawaiga marais na machifu wa kpindi kile, ijapokuwa hawakuwa na hela yoyote ya kupeleka watoto wao ulaya. Nindo ndo walikuwa wanapigia hela huko kwenye mirad ya nje.. 🙏🏽
9d5fa7a2681511092413564bc5fd3b7b.jpg

​
Usicheze na WATAWALA! Wenzenu wapo mbali na walikuwa na mahusiano mazuri na UINGEREZA tangu kipindi cha UKOLONI.

65110a1322dee18e78246fffcf59a706.jpg

​
Hawa ni SHINYANGA VIJIJINI [NINDO actually] na walifanikiwa kujijenga kisiasa na kiuchumi tangu miaka ya sitini [1960's] hadi leo.

05ca420b802b44e2f5b36ae0b6662ada.jpg

​
Sasa hivi SHINYANGA VIJIJINI [NINDO actually] ndiyo wanaongoza SERIKALI YA SENEGAL! HAYATI MWALIMU alikuwa vizuri sana katika masuala binafsi, kwanza hata mke wake hajawahi kuonekana kwenye vituo vya televisheni na majukwaa ya siasa.

e5dce55763da4f52df8b9abaeabad9bd.jpg

​
Huyo ambaye huwa anaonekana kwenye vituo vya televisheni siyo mwenyewe na wajukuu zake unaweza ukawa nao sehemu moja na usiwatambue!

3fa9c6d26dbc1e9ba0942d2cf48424a7.jpg

Vizazi vya watawala wengi wanarudi AFRIKA, kwa sababu ulaya kila kitu lazima ulipie hata kama unafanyika msaada kwa timu kuwa bora zaidi, lazima ulipie! WAINGEREZA huwa wanasema "no money, no love" au "no money, no service" hata kama una kipaji, kama huna pesa unaweza kulala njaa..

b14066814ba09bf725d46560f34121af.jpg

Kwahiyo wenzenu wale bado wapo vizuri kiuchumi na kisiasa! Ile nafasi ya URAIS WA KWANZA WA TANZANIA bado inaendelea kwa vizazi vyao na wanatambulika serikalini, sema waliamua kuchepuka baada ya mwaka 1975 na sasa hivi wanaendelea kufanya mambo yao.
 
Wenzenu walijaribu kuishi maisha na mtindo wa kimagharibi na walifanikiwa, ijapokuwa hawakuwa na fedha za kutosha ili kukamilisha masuala yao.

Tunaambiwa wale wastaafu wakuu wa majeshi walikuwa wanatumia gharama kubwa katika kufanikisha ndoto za watoto wao kuwa wasanii wa nyimbo na kucheza mpira wa miguu, ulaya!

Kumbe ulaya, idadi kubwa ya wanamichezo huwa wanatoka kwenye MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA na huwa wanaandaliwa na serikali kwa ajili ya kushiriki michuano ya kimataifa na kombe la dunia.

Wale waliokuwa MAWAZIRI kipindi cha miaka ya tisini [1990's] waliamua kuvumilia na kujijenga kiuchumi. Sasa hivi wanamiliki timu za mpira wa miguu katika BARA LA ULAYA!

FC SCHALKE 04 imebakiza michezo miwili au mitatu kupanda LIGI KUU YA UJERUMANI, BUNDESLIGA na inamilikiwa na WATANZANIA.

Watoto wao ndo waliowamalizia hela hao wakuu wastaafu wa majesh. Saivi hawana chochote, wamebakza kupiga madili ya serikalin! Popote penye gepu utawakuta.. 🙏🏽
 
kizaz cha sasa kimekuwa kivivu sn kutafit kinanendeshwa na ubuyu

Kambona anavuma sn ila hata kujieleza haez , Kambona alikuwa baba wa ufisad

Kama tusingepotoka na tungebakia kweny misingi ya Nyerere tungekuwa superpower kweny huu ukanda mzima

Kwasas rushwa , ufisad , ukiukwaj wa haki za binadam na ujinga mwing sn unaendelea ambao unafanywa kwa makusud kbs
Baada ya 1975, walioingia kuongoza serikal walikuwa hawajui hata gharama za muungano wa Tanganyika na zanzibar. Walikuwa wanaenda enda tu, kama gar bovu.. 😂 Wakatujazia wakosovo na wakongo
 
Usicheze na WATAWALA! Wenzenu wapo mbali na walikuwa na mahusiano mazuri na UINGEREZA tangu kipindi cha UKOLONI.

Hawa ni SHINYANGA VIJIJINI [NINDO actually] na walifanikiwa kujijenga kisiasa na kiuchumi tangu miaka ya sitini [1960's] hadi leo.

Sasa hivi SHINYANGA VIJIJINI [NINDO actually] ndiyo wanaongoza SERIKALI YA SENEGAL! HAYATI MWALIMU alikuwa vizuri sana katika masuala binafsi, kwanza hata mke wake hajawahi kuonekana kwenye vituo vya televisheni na majukwaa ya siasa.

Huyo ambaye huwa anaonekana kwenye vituo vya televisheni siyo mwenyewe na wajukuu zake unaweza ukawa nao sehemu moja na usiwatambue!

Vizazi vya watawala wengi wanarudi AFRIKA, kwa sababu ulaya kila kitu lazima ulipie hata kama unafanyika msaada kwa timu kuwa bora zaidi, lazima ulipie! WAINGEREZA huwa wanasema "no money, no love" hata kama una kipaji, kama huna pesa unaweza kulala njaa..

Kwahiyo wenzenu wale bado wapo vizuri kiuchumi na kisiasa! Ile nafasi ya URAIS WA KWANZA WA TANZANIA bado inaendelea kwa vizazi vyao na wanatambulika serikalini, sema waliamua kuchepuka baada ya mwaka 1975 na sasa hivi wanaendelea kufanya mambo yao.
Kuna viongoz wa kitaifa wengine hawajawahi hata kuwaona wake wa Nyerere,achilia mbali hata kupeana salamu! Jamaa alikuwa na mke zaidi ya mmoja..

Saivi kila mtu ndo anaenda hivyo! Nchi zangu tatu zimekaa pale chin zinasubiri nikawekeze, sema hela sina..

Msumbiji, Malawi na Zambia ni very good countries. Kwa wale undergrounds kama mie, huko panafaa kuzaa na kulea watoto wengi..

Ila wale wenye hela za kulenga kwa manatii, inabidi wasubiri zamu yao itafika hata kama bado iko nyuma.. 😂
 
Ilikuwa inawauma sanaa! Walitaman kuona watoto wao ndo wanafanya vizur darasan. Hzo zawad wangekuwa wanabeba wao kwa mbwembwe na wangekuwa wanatangaza had kwenye TV..

Lakin saivi wanaupiga mwingi ili kujipatia mali kwa njia za udanganyifu..😂 Kweli bongo nyoso, bongo balaaa..

Mwaka 2010 ilikuwa ni kama miujiza, Sacp alipatikana kupitia Necta na watu wote walikaa kimya qumammamake..

Elimu ya Tanzania ni nzuri sanaa, inaweza kumuinua yoyote bila ya kutegemea mtu yoyote. Ni kujua kuandika na kusoma kwa bidii.. Mchezo kwishaa halaf huwa wanapewa kuongoza gereza kwa miezi mitano kabla ya kwenda depo..

Tena msikae nao, Endeleeni hivyo hivyo! Mazoezi mengi, depo hadi mwakani! Wasije wakawapa sumu, maana wamekua kama Wakongo.. 😂

Kwahiyo malengo yamefanikiwa, Mkapa alitengeneza viongozi wa kijesh ambao watakuja kuwa royal kwa serikal na walikuwa wanapewa nyumba za serikali.. 🙏🏽
Unajua BARAZA LA MITIHANI TANZANIA [NECTA] linaweza kutoa DEPUTY COMMISSIONER OF POLICE [DCP] au DEPUTY COMMISSIONER OF PRISONS [DCP] kwa upande wa JESHI LA POLISI na JESHI LA MAGEREZA, kama endapo mwanafunzi atafanikiwa kuongoza kitaifa kwa mara tano mfululizo kuanzia DARASA LA NNE [FTNA], DARASA LA SABA [PSLE], KIDATO CHA PILI [FTNA], KIDATO CHA NNE [CSEE] na KIDATO CHA SITA [ACSEE].

images.jpeg

​
Sema kwa mwaka 2010, BARAZA LA MITIHANI TANZANIA [NECTA] lilifanikiwa kutoa mwanafunzi ambaye ni SENIOR ASSISTANT COMMISSIONER OF POLICE [SACP] na SENIOR ASSISTANT COMMISSIONER OF PRISONS baada ya kufanikiwa kuwa mwanafunzi bora kwa mara nne mfululizo.

_20260417_005614.JPG

​
VIONGOZI WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA huwa wanapatikana kupitia BARAZA LA MITIHANI TANZANIA [NECTA], sema JESHI LA MAGEREZA huwa hakuna ushindani kama ilivyo kwa upande wa majeshi mengine kwa sababu JESHI LA MAGEREZA, mwenye ufaulu mzuri au ufaulu mkubwa kuliko askari wengine ndiyo huwa anafanyika kuwa kiongozi wa kijeshi.

_20260417_005642.JPG

​
VIONGOZI WA JESHI LA MAGEREZA ni lazima kuwa miongoni mwa WANAFUNZI TANO [5] BORA kwa upande wa masomo ya uraia [MAARIFA YA JAMII kwa upande wa DARASA LA SABA au CIVICS kwa upande wa KIDATO CHA PILI na KIDATO CHA NNE au DEVELOPMENT STUDIES [DS] kwa upande wa KIDATO CHA SITA].

IMG_20220629_094922_5.jpg

​
Sasa kwa mwaka 2010, kupitia MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA SITA kulipatikana mwanafunzi ambaye alifanikiwa kuongoza kitaifa kwa mara nne mfululizo na alifanikiwa kuongoza masomo yote ya uraia kuanzia DARASA LA SABA [2003] hadi KIDATO CHA SITA [2010].

IMG_20220629_094505_5.jpg

​
Huyo ndiyo anatazamiwa kuja kuwa kiongozi wa kijeshi [CGP] hata kabla ya kufikisha miaka arobaini na tano [45], sababu hakuna wa kufanana naye.

_20230722_165809.JPG

​
Pia alifanikiwa kushika nafasi ya tatu kitaifa kwa upande wa MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA NNE [2000] na kufanyika kuwa na sifa ya kuwa kiongozi wa kijeshi [CDF] kwa upande wa JESHI LA WANANCHI [JWTZ].

cd05c966aee81078b20c80d029682b3a.jpg

Kwahiyo miongoni mwa MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA yanayopatikana TANZANIA, JESHI LA MAGEREZA linakuwa halina ushindani kama majeshi mengine kutokana na kuzingatia vigezo vya kitaaluma zaidi - askari mwenye ufaulu mzuri wa darasani katika masomo ya uraia ndiyo kiongozi wa kijeshi kwa upande wa MAGEREZA.

f3654932b4b26ce3ffe0f62c173e7b96.jpg

​
Ikitokea mhusika yoyote hayupo KUMI [10] BORA inafaa kufanya RESITTING EXAMS kama PRIVATE CANDIDATE [PC] na akifanikiwa kuingia KUMI [10] BORA au hata TANO [5] BORA anafanyika kuwa na sifa ya kuwa kiongozi wa kijeshi.
 
Magereza mwenye kisu kikali ndo mla nyama, huko kwingine unaweza kuambiwa utoe ndugu yako mmoja ndo uwe kiongozi wa kijesh.. 😂
 
Hiyo buti cjawahi ona inavaliwa jeshin! Magereza ina kampuni nyingi za viatu. Wengine walipata vyeo wakachezea, saiv wanaish kwa aibu hata hela hawana! Imebakia kila mtu wa kulaumu, Watoto kila kona hata hela ya kuwalea hamna.. 🙏🏽 Ngoja tuwavue hivyo vyeo.. Hauwez kuwa mkuu wa gereza na jeneral mstaafu halafu unaendesha genge la kitapel.. 😂
 
Hiyo buti cjawahi ona inavaliwa jeshin! Magereza ina kampuni nyingi za viatu. Wengine walipata vyeo wakachezea, saiv wanaish kwa aibu hata hela hawana! Imebakia kila mtu wa kulaumu, Watoto kila kona hata hela ya kuwalea hamna.. 🙏🏽 Ngoja tuwavue hivyo vyeo.. Hauwez kuwa jeneral mstaafu halafu unaendesha genge la kitapel.. 😂
Sasa hivi viongozi wa kijeshi wanajiunga na MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA wakiwa tayari na zawadi zao kutoka WIZARA YA ELIMU [MEM].

328166bbfddb46bd5573d54ee2e60ed8.jpg

​
Kwahiyo zile tabia zenye ukakasi, vishawishi na tamaa ndogondogo hawatakuwa nazo ukilinganisha na wale viongozi wa kijeshi wa miaka iliyopita.
 
Sasa hivi viongozi wa kijeshi wanajiunga na MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA wakiwa tayari na zawadi zao kutoka WIZARA YA ELIMU [MEM].

Kwahiyo zile tabia zenye ukakasi, vishawishi na tamaa ndogondogo hawatakuwa nazo ukilinganisha na wale viongozi wa kijeshi wa miaka iliyopita.
Mzee Makamba apo angenunua Fuso 10! Kila cku anapiga lumbesa Korogwe to Dar, msimu wa matunda ukikaribia.. 😂

Wengne walichezea hela! Saivi gharama ya jezi pair moja pamoja na tracksuit yake inafika 3 million kwa ulaya. Kibongo bongo unanunua bodaboda moja..

Sasa wale wastaafu wa majesh walikuwa wanapeleka watoto wao kwenda kucheza mpira ulaya kwa kufata mkumbo. Saivi hawana hela, ziliwaishia.. 🙏🏽
 
Ukiwa KENYA, kuna timu ya mpira wa miguu inayoshiriki LIGI KUU inaitwa NAIROBI CITY STARS. Pale kuna WATANZANIA wengi sana pale..

538960ffa573bfcaed855ee58ea141fe.jpg

​
Wengine waliamua kupeleka watoto wao ulaya na walifanikiwa kucheza mpira wa miguu kwa mafanikio makubwa.

4f986c4c2f249bedbb806fd93dc224b1.jpg

​
Walijaribu kumudu gharama kwa kipindi kile, ijapokuwa wanamichezo wengine kutoka ULAYA, AMERIKA na ASIA walikuwa chini ya usimamizi wa serikali zao na huwa wanatokea katika MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA.

e6c3bfa87a842868f7a5f549372f9315.jpg

​
Malengo yalitimia kucheza mpira wa miguu barani ulaya, lakini gharama ilikuwa ni kubwa sana kwa wanamichezo wenye asili ya kiafrika.

efc1015bd7c6f7b135c4026f8534b4ba.jpg

​
Hiyo gharama wanayoweza kumudu vizuri bila ya kuwa na vikwazo, huwa ni familia za watawala lakini wengine inabidi tutafute mbadala katika mataifa ya kiafrika.

76b9728250e11252265a16c3604dbead.jpg

​
 
Ukiwa KENYA, kuna timu ya mpira wa miguu inayoshiriki LIGI KUU inaitwa NAIROBI CITY STARS. Pale kuna WATANZANIA wengi sana pale..

Wengine waliamua kupeleka watoto wao ulaya na walifanikiwa kucheza mpira wa miguu kwa mafanikio makubwa.

Walijaribu kumudu gharama kwa kipindi kile, ijapokuwa wanamichezo wengine kutoka ULAYA, AMERIKA na ASIA walikuwa chini ya usimamizi wa serikali zao na huwa wanatokea katika MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA.

Malengo yalitimia kucheza mpira wa miguu barani ulaya, lakini gharama ilikuwa ni kubwa sana kwa wanamichezo wenye asili ya kiafrika.

Hiyo gharama wanayoweza kumudu vizuri bila ya kuwa na vikwazo, huwa ni familia za watawala lakini wengine inabidi tutafute mbadala katika mataifa ya kiafrika.

Ukiwa ulaya had mipira ya timu lazima wachangie wachezaji. Halaf majina yao wanayotumia uwanjani sio majina ya kuzaliwa..

Saiv jamaa ukiwa Nairobi City Stars ana wachezaji wawili wanacheza hapo na msimu uliopita walicheza michuano ya afrika.. 🙏🏽
 
Ukiwa ulaya had mipira ya timu lazima wachangie wachezaji. Halaf majina yao wanayotumia uwanjani sio majina ya kuzaliwa..
IMG_20260426_134102.jpg

​
Tunaambiwa huwa wanafanya hivyo na wana sababu zao za kutumia majina bandia.
Saiv jamaa ukiwa Nairobi City Stars ana wachezaji wawili wanacheza hapo na msimu uliopita walicheza michuano ya afrika.. 🙏🏽
Kweli! Mataifa mengine ambayo ni mazuri kuwekeza na kuishi kwa WATANZANIA ni MSUMBIJI, MALAWI na ZAMBIA.

IMG_20260426_142107.jpg

​
Kuna WATANZANIA wanamiliki timu za mpira wa miguu, ulaya na watakuja kuwekeza katika mchezo wa mpira wa miguu kwa upande wa mataifa ya MSUMBIJI au MALAWI au ZAMBIA.

Huko kwingine, hasa MAREKANI wenyeji wengi wa asili ya kiafrika wanahama na kurudi makwao.
 
Tunaambiwa huwa wanafanya hivyo na wana sababu zao za kutumia majina bandia.

Kweli! Mataifa mengine ambayo ni mazuri kuwekeza na kuishi kwa WATANZANIA ni MSUMBIJI, MALAWI na ZAMBIA.

Kuna WATANZANIA wanamiliki timu za mpira wa miguu, ulaya na watakuja kuwekeza katika mchezo wa mpira wa miguu kwa upande wa mataifa ya MSUMBIJI au MALAWI au ZAMBIA.

Huko kwingine, hasa MAREKANI wenyeji wengi wa asili ya kiafrika wanahama na kurudi makwao.

Wale professional huwa wanakuwa kazin! Wengne wakaingia kichwa kichwa, acha waliwe hela zao na zaman kulikuwa na mashndano ya kupeleka watoto wao ulaya..
 
Wale professional huwa wanakuwa kazin! Wengne wakaingia kichwa kichwa, acha waliwe hela zao na zaman kulikuwa na mashndano ya kupeleka watoto wao ulaya..
Kuna baadhi ya WATANZANIA ambao walifanikiwa kuyafahamu haya masuala tangu miaka ya tisini [1990's], hapo ndiyo ilikuwa mwanzo wa kuanza kujijenga kiuchumi.

WATANZANIA wapo wengi na wengine wanaishi nje ya nchi, tena wengine ni wanasiasa na matajiri wakubwa!

IMG_20260426_220348.jpg

Ukiwa KENYA, TANZANIA ni nyumbani kwao! Ukiwa UGANDA, RWANDA na BURUNDI, TANZANIA ni nyumbani kwao! Ukiwa MSUMBIJI, MALAWI na ZAMBIA, TANZANIA ni nyumbani kwao! Ukiwa AFRIKA YA KUSINI, TANZANIA ni nyumbani kwao! Ukiwa GHANA na TOGO, TANZANIA ni nyumbani kwao!

IMG_20260426_214332.jpg

Tunaambiwa baada ya mwaka 1975, hao WATANZANIA waishio nje ya nchi [DIASPORA] walipata nguvu ya kushiriki na kufanya maamuzi ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI [CCM] na ndani ya SERIKALI YA TANZANIA.

IMG_20260426_214336.jpg

Huwa wanachagua RAIS pamoja na VIONGOZI WA KIJESHI! Bila ya wao kupitisha, hakuna kitakachofanikiwa ndani ya mipaka ya TANZANIA na ZAMBIA ndiyo taifa lenye ushawishi na nguvu kubwa ndani ya SERIKALI YA TANZANIA. Ndiyo maana wenzenu huwa wanapitia BARAZA LA MITIHANI TANZANIA [NECTA]..

IMG_20260426_214445.jpg

Kwahiyo ushindani upo mkubwa, ukizingatia WATANZANIA waishio nje ya nchi [DIASPORA] ni wasomi, wanamiliki uchumi mkubwa na wanasikilizwa sana kuliko WATANZANIA waishio ndani ya nchi.

IMG_20260426_214513.jpg

Hivyo WATANZANIA waishio ndani ya nchi waliofanikiwa kuyafahamu haya masuala tangu siku nyingi waliamua kujipanga vizuri na kusomesha kwa bidii.
 
Wale professional huwa wanakuwa kazin! Wengne wakaingia kichwa kichwa, acha waliwe hela zao na zaman kulikuwa na mashndano ya kupeleka watoto wao ulaya..
IMG_20260426_140212.jpg

​
Pia tunaambiwa KENNETH KAUNDA [the late] alikuwa ni hasimu mkubwa wa HAYATI MWALIMU ~ HAYATI MWALIMU aliposema amesaidia kupatikana kwa uhuru nchini MSUMBIJI na KENNETH KAUNDA [the late] akasema hata ZAMBIA ilisaidia kupeleka askari nchini MSUMBIJI kupitia MALAWI ili kulahisisha harakati za kudai uhuru.

_20260427_125852.JPG

Kwahiyo KENNETH KAUNDA [the late] alifanikiwa kuondoa SHINYANGA VIJIJINI [NINDO actually] na kuendeleza KISHAPU [BUBIKI actually] katika SERIKALI YA MSUMBIJI, ambapo tayari wenyeji wa asili wa KISHAPU [BUBIKI actually] walikuwa wameshatangulia kufika MSUMBIJI tangu utawala wa kikoloni uliokuwa ukiongozwa na MUSSA BIN BIQUE.

Pia chimbuko la jina la kijiji cha BUBIKI limetokana na jina la mfanyabiashara maarufu wa biashara ya utumwa aliyekuwa anaitwa MUSSA BIN BIQUE.
 
Pia tunaambiwa KENNETH KAUNDA [the late] alikuwa ni hasimu mkubwa wa HAYATI MWALIMU ~ HAYATI MWALIMU aliposema amesaidia kupatikana kwa uhuru nchini MSUMBIJI na KENNETH KAUNDA [the late] akasema hata ZAMBIA ilisaidia kupeleka askari nchini MSUMBIJI kupitia MALAWI ili kulahisisha harakati za kudai uhuru.

Kwahiyo KENNETH KAUNDA [the late] alifanikiwa kuondoa SHINYANGA VIJIJINI [NINDO actually] na kuendeleza KISHAPU [BUBIKI actually] katika SERIKALI YA MSUMBIJI, ambapo tayari wenyeji wa asili wa KISHAPU [BUBIKI actually] walikuwa wameshatangulia kufika MSUMBIJI tangu utawala wa kikoloni uliokuwa ukiongozwa na MUSSA BIN BIQUE na chimbuko la jina la kijiji cha BUBIKI limetokana na jina la mfanyabiashara maarufu wa biashara ya utumwa aliyekuwa anaitwa MUSSA BIN BIQUE.
Kumbe mnayajua had haya! Tulifikir hamjui, kishapu yote ile iliondoka na imebakia wageni.. 🙏🏽 Mara ya kwanza walihamia Msumbiji kupitia biashara ya utumwa na mara ya pili walikuja kuhamia Togo kupitia Makwaia.. 😊

Sultan Musa Bubiq alikuwa ananunua watumwa kutoka kishapu, Chif Makwaia akazani wanapelekwa Omani kumbe walikuwa wanapelekwa Banguela..

Saivi Bubiki ndo watawala wa Msumbiji na Chif Makwaia alihamia Togo had leo.. 🙏🏽
 
Back
Top Bottom