Charles Mandela
JF-Expert Member
- Dec 9, 2011
- 3,694
- 3,309
Huwa tunaambiwa kipindi cha HAYATI MWALIMU walikuwa wanajaribu kufananisha serikali na mti uliokomaa ~ ikiwa na maana ya mizizi ndiyo MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA! Mashina ikiwa na maana ya OFISI, TAASISI na WIZARA ZA SERIKALI! Halafu matawi ikiwa na maana ya VYAMA VYA SIASA!Hao watu ni matajir mno na wanaongoza Tanzania wakiwa nje ya inchi! Ndo maana saivi watu wanatafuta hela kwa nidhamu, wakirudi hao hamna kitu hapa..
Hakuna hata cha mtandao! Hao ni balaa na wanatumia intelijensia zao, hata majeneral diaspora wa Kitanzania wakiingia majeshin wanaheshmika kuliko hawa waliopo Tanzania..
Kwahiyo wapo vizur na Tanzania ndo huwa inaponea huko, hata ikipata vikwazo inaish kupitia hizo serikal za Zambia, Malawi na Msumbij.. 🙏🏽
Siku zote matawi huwa yanastawi na kunyauka kulingana na nyakati na majira ya mwaka. Lakini mizizi na mashina huendelea kubaki hata baada ya majira yote ya mwaka kupita.
Mabadiliko ya VYAMA VYA SIASA huwa inakuwa ni hatua ya mwisho, pale ambapo kila kitu ndani ya serikali kinakuwa kinaenda sawa kwa mujibu wa SHERIA ZA NCHI [DOMESTIC LAWS] pamoja na SHERIA ZA UMOJA WA MATAIFA [INTERNATIONAL LAWS]. Tofauti na hapo mabadiliko ya kisiasa yanaweza kusababisha sintofahamu kwa upande wa serikali na taifa kwa ujumla!