Ndiyo elimu ya kijeshi inavyotakiwa kuwa!
Kwa ujumla, inatambuliwa na WAAFRIKA wote pamoja na wataalamu wanaoletwa ili kuwashauri kuhusu elimu, kwamba hitaji kuu la kusonga mbele kuelekea katika ulimwengu wa kisasa ni kuongeza fursa za elimu. Kila serikali ya AFRIKA iliyopata uhuru hivi karibuni inalenga na kupanga kutoa elimu zaidi ya shule pamoja na mafunzo ya ufundi katika kila ngazi - ingawa kwa kawaida baadhi ya serikali zinaonesha hali ya uharaka mkubwa zaidi kuliko serikali nyingine.
Kutokana na shauku kuwa kubwa, mengi yameandikwa kuhusu elimu barani AFRIKA. Jambo hili limechunguzwa kwa kina na tume mbalimbali pamoja na wataalamu binafsi.
Katika kipindi cha utawala wa kikoloni, elimu na mafunzo ya ufundi kwa WAAFRIKA ā yaani, jukumu zima la kuwawezesha kuendesha jamii ya kisasa, tofauti na jamii zilizokuwepo kabla ya ukoloni ā kwa kiasi kikubwa liliangukia kwa serikali za kikoloni, wamisionari na mashirika ya kibiashara ambayo kwa sababu moja au nyingine yaliona umuhimu wa kulitekeleza jukumu hilo. Si jambo la kushangaza kwamba elimu hiyo ilionesha mahitaji na mitazamo yenye upendeleo ya taasisi hizo za watu weupe.
Elimu ya kimisionari ilikuwa kwa kiasi kikubwa ya kujitoa bila kutafuta faida binafsi na yenye mitazamo ya kibinadamu. Ikiwa na misingi ya kidini, huku ikiwa na vipengele vya kifasihi, kitabibu na kijamii. Elimu hiyo ilijikita hasa katika kuwakomboa WAAFRIKA ā iwe mtu mmoja mmoja au jamii nzima ā kutoka katika mitindo yao ya maisha ya kikabila au iwapo tayari walikuwa wameachana nayo, iliwalahisishia kuwapa mfumo mwingine wa maisha ambao ungeridhisha zaidi mahitaji yao ya kiroho.
Katika msingi huu, kazi ya wamisionari wa kikristo inalinganishwa kwa karibu kabisa na kazi ya wafanyabiashara na wengine walioeneza uislamu, ambao pamoja na dini hiyo walieneza pia usafi na afya bora, uwezo wa kusoma na kuandika, pamoja na uaminifu mpya wa kijamii. Wamisionari wengi wanatambua jambo hilo! Hata hivyo, misheni za kikristo bila kuepukika pia ziliwawezesha WAAFRIKA kufahamiana na ulimwengu wa kiteknolojia wa watu weupe, lugha yao, viwango vyao na ujuzi wao.
Mafunzo yanayotolewa na mashirika ya kibiashara yanalenga kuongeza ufanisi na manufaa ya mfanyakazi kwa shirika husika. Bila kujali mfumo wa kiuchumi na kijamii ambao mataifa mbalimbali ya AFRIKA yatachagua kuufuata baada ya kupata uhuru, ni dhahiri kwamba yatahitaji ujuzi wote huo, pamoja na ujuzi mwingine mwingi zaidi, kuliko ule ambao sehemu ndogo ya raia wao wameupata kupitia mafunzo yaliyotolewa na mashirika ya kibiashara ya kigeni.
Matatizo yanayozikabili serikali za kiafrika katika kupanua mifumo yao ya elimu hutofautiana kwa kiasi fulani, kutegemea urithi mbalimbali wa kikoloni waliourithi kutoka kwa mataifa matatu ya kikoloniā UINGEREZA, UBELGIJI na UFARANSA.