Charles Mandela
JF-Expert Member
- Dec 9, 2011
- 3,694
- 3,309
Ngoja tuachane na stori za Nyerere! Hizo sheria za moko huwa zipo duniani kote, sema watanzania huwa hawazifati na mataifa yaliyoendelea hadi viongoz wa kitaifa akiwemo Rais lazima wawepo tano bora kwenye mitihani ya moko. Kuanzia moko kata, moko wilaya, moko mkoa hadi moko kanda..
Mitihani ya moko huwa ni krimu ya taifa na walioingia tano bora ndo huwa askari magereza na askari usalama! Wanafunzi waliofanikiwa kuingia tano bora kwenye moko ndo huwa wanastahili kupata skolaship za masomo ya juu kupitia ufadhili wa serikal..
Hata mikopo ya vyuo vikuu kwa ngazi ya degree, waliokuwa wanatakiwa kupata ni wale wanafunzi waliofanikiwa kuingia tano bora kwenye mitihani ya moko..
Hizo ndo sheria za sekta ya elimu kupitia wizara ya elimu pamoja na umoja wa mataifa! Moko ndo kila kitu na hao ndo kipaumbele cha kwanza kwa serikal kwenye sekta ya ajira, lakini mtihani wa taifa hufanyika mara moja kwa siku moja na itategemea mwanafunzi ataamkaje siku ya mtihani.. 🙏
Lakini ile kibongo bongo waliacha kuzifuata hizo sheria na kuamua kutunga sheria zao kwa kuzingatia muonekano wa mtu na urefu wa kimo chake.
Ila kwa upande wa viongozi wa kijeshi, lazima mhusika awe ni miongoni mwa wanafunzi waliofanikiwa kufanya vizuri kitaifa kwa ujumla.
Yaani ile kamati inayochagua MKUU WA JESHI LA POLISI [IGP], ndiyo kamati inayopendekeza majina matatu [3] katika nafasi ya UWAZIRI UKUU na kupeleka majina hayo katika ofisi ya rais.