Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

kuna link hapo ya wikipedia nimeweka, alafu hakuna habari nyingi sana zilizoandikwa zinazomuhusu kambona nafkiri kizazi kilichopita kilitaka kumpotezea kabisa nitaendelea ku update kila napopata chanzo kipya
 
Bro kazi aliyofanya Nyerere ya kuleta umoja wa kitaifa unaichukuliaje? Congo ni nchi tajiri kuliko nchi yoyote duniani lakini ni nchi mojawapo wananchi hawaelewani na kuishia kuuana wenyewe kwa wenyewe huku ufukara ukiwatafuna. Utajiri wao sio kitu. Hapo Kenya ardhi inamilikiwa na watu wachache... Somalia baada ya kifo cha Siad Bhare hawajawahi kuwa sawa tena. Kwahiyo pamoja na madhaifu yake bado Nyerere ni bora kuwahi kutokea. Isitoshe Nyerere aliamua kung'atuka ambapo angekuwa Rais mwingine angesubiri kuondolewa kwa bunduki au maandamano ya wananchi.
 
Nyerere alikuwa sahihi kwa wakati ule, na kambona alikuwa si sahihi kwa wakati ule.
1. Kwanza mtu mweusi alikuwa mtumwa
2. Mtu mweusi alionaneka mdhaifu, hana akili, asiyejiweza na mpumbavu.
3. Mzungu na wahindi walionekana ndiyo binadamu pekee.
4. Mambo yote mazuri, kula vizuri, kulala pazuri, kumiliki maduka, viwanda, mashamba makubwa na raha zote za dunia ilikuwa kwa no.3
5. Mweusi alikuwa ni bidhaa kama bidhaa zingine.
6. Viongozi wengi weusi walitumika kuwakirisha wazungu au wahindi. Walipewa vijisenti na chai ya maziwa kwa mkate wenye siagi.

Kabla sijaendelea kukukumbusha madhira na mateso waliyopata mababu zetu ndani ya nchi yao ni vizuri rudi tena kasome historia ya Tanganyika na Afrika kwa ujumla.
Ni bora kutembea uchi ukiwa huru, kuliko kuvikwa nguo kwa kuuza utu wako. NYERERE ALITAKA KUONA MTU MWEUSI ANAMILIKI MALI NA KUWA HURU NA KUHESHIMIKA. Tatizo la Kambona lilikuwa kukumbatia sera za weupe.
 
nimesusanya dots za hapa na pale nkasoma stories zake , cha ajabu wale ambao walishuhudia haya yote kwa macho yao huwezi kuskia wakiongelea haya mambo watuambie ukweli
Hata kama walishuhudia bado hawawezi kujua chanzo cha ugomvi,wanaojua ni wahusika Nyerere na Kambona na bahati mbaya kwenye mambo kama hayo Hanna hata moja wao anaweza kusema ukweli kwa mini kilicho wasababisha wakagombana.

Chukulia mfano wa ugomvi wa Kikwete na Lowassa,ingawa hata wewe umeushuhudia lakini huwezi jua ni nini hasa kilichofanya wakosane,yote yanayoandikwa na kusemwa ni gossip na nadharia.ukweli wote unabaki kwa wahusika na hata moja wao hawazi kusema ni siri yao watakwenda nayo kabulini.
 
Sasa hiyo ardhi uliyonayo inakusaidia nini??
 
ulivyo jitapa kwamba umesoma na kufatilia ukaona kambona alikuwa sahihi kumbe ujinga mtupu unaonekana mweupe yaani hujui chochote zaidi ya historia za vijiweni.

iyo ardhi tu ingemilikiwa kibepari tangu enzi hizo hali ingekuwaje
 
Asante kwa kuweka rekodi sahihi!! Vijana wa sasa hawapendi kabisa kusoma vitabu!! Ivyo hawajui kabisa historia ya taifa lao!!! kama wanavyozijua timu za mipira za duniani! starehe na wafanya starehe wa duniani!! Tunasema vijana wana mbio ila hawaijui njia!!
 
Na hili swala watu wengi hawalijui,Nyerere hakupenda kuondoka hali iliyokuwepo ndio iliyosababisha aondoke.
 
Baada ya kugundua upungufu huo nini kifanyike sasa. Kwa maoni yangu, watu waandike vitabu. Hiyo ndiyo itakuwa mwarobaini ya mvutano uliopo. Kwa mfano, hoja za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wachangiaji ni ushuhuda wa wazi kuwa hawajapata muda wa kupitia biography (Volumes 3) ya Mwalimu ambayo imeandikwa na waandishi mahili watatu - Issa Shivji, Saida Yahya-0thman na Ng'wanza Kamata. Tuanzie hapo ili kutoa taarifa sahihi na elimu pana kwa kizazi chetu na kijacho. Malumbano bila 'facts' ni kupoteza muda tu na kuongeza ulimbukeni. Tujitahidi sana kujisomea ili kunoa bongo zetu. Kheri ya mwaka mpya.
 
Jamani Ila yote kwa yote Haya mambo ya mfumo wa kuchumi kati ya ujamaa na ubepari ilikuwa ni bahati nasibu kwa kiongozi afuate upi.

Yote yanatokana na Urusi kuzidiwa nguvu na USA,kama Urusi angemzidi USA katika ugomvi wao na kuendelea kuwa superpower wa dunia hap hakika nchi nyingi zingekuwa katika mlengo wa kijamaa na tungeiona ni bora sana kuzidi ubepari.

Hata vikwazo alivyokuwa nawekewa Nyerere na serikali ya USA na UK ilitokana na msimamo wake wa kuendelea kushikilia Sera ya ujamaa,huku wennyewe wakutaka Sera za ubepari.

So,Nyerere alikuwa sahihi kutokana na mazingira ya kipindi kile kosa lake kubwa hukuona mbele ambapo dunia inaelekea.
 
Alizikwa wapi huyu jamAa
 
Sifa kubwa ya Mwalimu Nyerere tofauti na hao wengine akiwemo Kambona ni kutoigaiga mambo, Bali aliamini kuwa matatizo ya mwafrika yataondokana na mwafrika kuishi Kama desturi yake yani kwa asili mwafrika amekuwa akiishi kijamaa...yeye alisema maendeleo ni kazi na si mikopo Kama ilivyo sasa...Kuna watu humu ni mablind supporter wa capitalism...lakini ukweli ni kwamba hata ubepari haujasaidia nchi za Afrika, ni mfumo uliopelekea nchi nyingi maskini kuwa na madeni makubwa yasiyoweza kulipika na wizi wa rasilimali...china si wakujifananisha nao, eti waliacha ujamaa na kufuata ubepari...china haijawahi kusema kuwa waliacha mfumo fulani wakaenda mfumo mwingine halafu ndo wakafanikiwa, maendeleo ya china mzizi wake ni ujamaa...ujamaa haukatazi kufanya biashara, Ila unaweka control kubwa Sana katika biashara kiasi kwamba msipokuwa na dira nzuri hamuwezi kutoboa...Ila mkijipanga vizuri mnakuwa thabiti zaidi kuliko mfumo wa kibepari ambao ni more fragile na unategemea zaidi external factors kuliko hali ya kiuchumi ya ndani...China kilichokuwa kinamkwamisha ni kutokuwa member wa World Trade Organization miaka ya nyuma...ivo kuathiri uwezo wake wa kufanya biashara...sababu kuu ya kufeli kwa ujamaa kwa nchi nyingi zilizofwata mfumo huo ni vikwazo....na kufaulu kwa ubepari ni mikopo kutoka taasisi za mabepari...na mikopo hii ilichochea rushwa, urasimu, ukiritimba na hatimaye umaskini...kwa kuwa mingi haikutumika kwa kazi mahsusi...Bali iliishia kwa wachache...halafu hawa wanaokuja kwetu na kujinasibu kuwa ni mabepari ni gia tu hiyo...ili waweze kutuibia vizuri lakini terms wanazoingia wao kwa wao wazungu zina elementi nyingi za kisoshalisti...sema hawaziiti majina hayo, kaangalie faida za kuwa mwanachama eu...na jinsi wanavyolimit free trade na nchi zisizo wanachama...tatizo la nchi za Afrika ni zaidi ya aina ya mfumo unaotumika kutawala...unaanzia kwenye nafasi ya mwafrika katika dunia ya leo...yani Kama wakikaa wenye nguvu duniani ni kipi mwafrika ataleta mezani, wao wakimwona kiongozi wa kiafrika katika mikutano yao wanajua kaja kuomba misaada, sasa namna iyo hamuwezi kutoboa...
 

Ukomunistu, udikteta na ujamaa ni pacha kwenye hii mifumo hairuhusiwi mtawaliwa kuwa na pesa tajiri au elimu kuliko anayekutawala thus ni lzm matajiri wafilisiwe na wenye elimu ni lzm washughulikiwe, ujamaa umekazia kutawala watu ubepari umekazia Uhuru wa kiuchumi.
Matatizo ya mwafrika yamesababishwa na watawala wa kiafrica tofauti na tulivyopandikizwa chuki na uongo wa kina Walter Rodney, professor lumumba wa kenya, nk. Ujamaa umekazia kutupia lawama juu ya kushindwa kwao kuwaletea waafrika maendeleo. Kukopa sio tatizo bali tatizo ni kukopa na kuwekeza kwenye miradi isiyo tija kiuchumi mfano kununua wapinzani, kupambana na wapinzani kuliko kupambana na maendeleo, kujenga ikulu mpya Hali ya zamani ipo, kununua ma v8 zinazotafuna Kodi badala ya kununua matreka yazalishe kumbuka v8 ni sawa na trekta 6 horse power 75 brand new na vilimio vyake.Kuiba Pesa za walipa kodi na kuzificha mabenk ya ulaya Ili ufanywa na watawala wa kiafrica, kuwaaminisha watu kwamba uzalendo ni kuwa masikini, kila aliyefanikiwa ni mwizi. Wizi, rushwa, ufisadi baada ya wa chini kuona wakubwa zao wakifisadi nchi,unawapora ardhi raia wako walimao kwa mashine na unawapa makada maveterani wako lengo Ili upate kura zao, kwa yote hizi internal fact hapa unamlaumu vipi bepari ndio amesababisha yote na sio mtawala wa kiafrica.
 

au walichuliana mahawara hawa. maana inasemekana kambona alikuwa kijana msomi, handsome boy na shababi kweli kweli. halafu alikuwa anatema yai safi kuliko nyerere .

https://youtu.be/Qi-LqF86qrA
 

Wote walikuwa na mawazo mazuri. They didn't agree. Take 50% of each person tusifungamane na upande wowote. Tujali maslahi ya watu wetu.

Ilikuwa vigumu sana kufanya hivyo, kupinduliwa, kuuliwa ilikuwa rahisi sana, unaishi kwa machale kila siku.

Wanaiita Cold War sababu USA na USSR hawakupigana.

Ilikuwa Very Hot War in Africa, Latin America and Asia. Mamilioni walikufa au kuuwawa kwa maslahi yao two super powers.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…