Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Tangu nipo shule ya msingi tulikua tunaaminishwa kwamba Mlm Nyerere ndio "icon" pekee apa nchini, tulikua tunaimba nyimbo nyingi ni za kumsifu, lakini hatukuwahi kuambiwa kua kuna watu wengine ambao bila wao mwalimu "asingetoboa" na pengine tusingemjua kabisa mwalimu nyerere, au story yake ingekua "short lived". Mmoja wa hao watu ni OSCAR KAMBONA.

Nimezaliwa hapa Tanzania miaka ya 90 mpaka nimekua mtu mzima kila kitu ni Nyerere tu. Kambona nilimsikia badae sana baada ya kuskia kisa cha huyu mtu nikawa interested sana kufuatilia stories zake.

kwa mujibu wa maandiko Kambona alikua bega kwa bega na mwalimu ktk kudai uhuru yaani ilikua akitoka mwalimu anaefuata ni Kambona lakini huwezi sikia hichi kitu kinasemwa waziwazi na pengine bila mawazo na support ya kambona mwalimu "angefeli vibaya mno". Kambona ndio mtu aliezima mapinduzi yalioilenga serikali ya nyerere kutoka kwa askari waliotaka kuasi, yaani kwa ufupi ni kwamba Nyerere asinge endelea kua mtawala wa nchi hii kama sio Kambona.

Kambona aliona mbali kuliko mwalimu Tanzania ya sasa ndio aliyoiona kambona lakini mwalimu alipinga, Kambona aliona ubepari ndio utafanya kazi lakini mwalimu aliona ujamaa ndio unafaa, mwalimu "failed miserably" akatupeleka chaka mpaka leo we still pay for his "grave mistake". Mwalimu alikua mbishi na aliamini kwamba yeye ndio ana maono bora kuliko wengine ,chochote kile ambacho kilikua hakiendani na sera zake alikipinga hata kama kilikua "viable". Fikiria mtu mmoja tu kaenda urusi akafurahishwa na mfumo wa ujamaa akaja kuufanyia "experiment" hapa nchini na ukafeli kwasababu alikataa kusikiliza maoni ya watu wengine, kwa wakati huo mwalimu ndio alikua "kila kitu"

Kambona akatofautiana na mwalimu , yeye alitaka ubepari mwalimu alitaka ujamaa. Kutokana na ushawishi mwalimu alishinda japo kambona ndie aliekua sahihi lakini hawakumskiliza. Baadae mwalimu alijua amekosea akaturudisha kwenye Ubepari na bado akaonekana ni "hero" . Kitu ambacho oscar alikiona miaka kadhaa kabla wakati huo mwalimu alikua "blind" almost everyone was blind except the very few including Kambona

Haya leo 2021 TZ hii ya leo ndio kambona aliyoiona na tumechelewa sana, kwa mtazamo wangu bado tupo nyuma kwa miaka 15 kutokana na sera mbovu za mwalimu nyerere

Wote ni marehemu wapumzike kwa amani lakini, mwisho wa siku Oscar Kambona ndio AMESHINDA!!!!! Kwangu mimi shujaa wa kweli nchi hii ni OSCAR KAMBONA na sio mwalimu! Na ndio mtu muhimu sana sawa na mwalimu lakini ndio aliesahaulikia kuliko wote nchi hii, natamani watanzania wengi tuliozaliwa miaka ya 90 wajue habari za huyu shujaaa

Aliyeweka Nyerere day kama public holiday alitumia vigezo gani ilihali si kweli kwamba Nyerere ndie mtu pekee aliepigania uhuru wa nchi hii

Ukiniambia nichague kati ya Nyerere na Kambona itakua ni Kambona always

"Oscar Kambona was one of the best presidents Tanzania never had"

Oscar Kambona - Wikipedia
Pumba,Majungu na umbea.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
ujamaa kwa kipinde kile ilikuwa njia sahihi ya kuwaweka pamoja maana watu wengi walikuwa hawana elimu, wanaishi maisha duni sana, wanakaa mbali kutoka nyumba moja hadi nyiungine hata kupeleka huduma za kijamii ilikuwa shida sana, barabara mbovu kama tungeendelea na ubepari bas wananchi wangeendelea kuwa watumwa zaidi. ujamaa uliwaletea heshima zaidi baada ya kuanzisha vijiji vya ujamaa na kujenga umoja na kukuza lugha ya taifa na utaifa.

ujamaa ndio ulisaidia sana kujenga utaifa na kuachana na ubaguzi....ukabila uliondoka sabaabu ya ujamaa watu waliweza kujiona wao ni watanzania, utani wa jadi ukaanza.

nchi nyingi zilizoenda kwenye ubepari hasa Africa zina matatizo mengi ukichunguza.

mtoa maada nakushauri usome vizuri ama ongea na wazee walioishi kipindi hicho maana umesema ulizaliwa kipindi cha 90s. bado una mengi ya kujifunza kuhusu historia ya tanzania.

ni kweli walikjuwepo watu wengi walioshiriki kuleta Uhuru wa nchi japo hawakuwa na Elimu na hostoria imewaacha sana.

Ndio maana mkuu amesema watu wafundishwe historia ya nchi yao... hata ww umepata historia ya kambona kwa kuokoteza tu hujui mambo kwa undani wake. usingefanya hitimisho kwenye andiko lako ili watu wawe huru kujadili na ww kupata mwanga.
 
Acha uvivu, uzembe na upumbavu. Tangu Nyerere aache urais ni muda mrefu sana na tungekuwa tuna uongozi mzuri nchi unayoitamani wewe ingeshatengenezwa. Nyerere ni mmoja ya viongozi wazuri sana kutokea. Nchi gani za Afrika zilikuwa na viongozi wazuri enzi za Nyerere ambazo unaweza kutoa kama mfano leo? Mimi naona nchi nyingi zina changamoto kuliko Tanzania mara kumi.
Kwani yeye si alikuwa ni rais? Alituacha wapi?
 
Kila mrengo unafaida na hasara zake, Mwalimu kwa Sera ya ujamaa angalau Ardhi, elimu na afya tunafaidi japo kadri miaka inavyosonga Elimu inakuwa ghali kuipata ile nzuri, Ubepari nao unamabaya yake waone Kenya na Zambia baada ya Rais Kaunda ndo utajua kwanini kila Sera inamabaya na mazuri yake

Ulifaidi vipi elimu? Wakati wake aliweka sera za kuwa na watu wachache wenye elimu ya juu, hata mataifa yenye watu wachache barani yalitupita kuwa na wasomi
 
Hivi ubepari ni utengano? Mbona kama tunaishi ndani ya propaganda za kikomunist juu ya ubepari.

Twende sawa hapa hii dhana kuwa Ujamaa umetuletea Umoja ni dhana ya ajabu sana.

Mimi nasema System ndio imetufanya tukawa na Umoja, ni Usalama wa taifa na Jeshi la nchi hii ndio waliotupa huu Umoja.

Ina maana kuwa hata ndani ya Ubepari kama System ingekuwa na matamanio ya Umoja tungekuwa na huu huu Umoja.

Hili neno Ujamaa ndio linairemba siasa ya Mwl. Nyerere ila jina halisi ni "Ujima"

Kama Mwl. Nyerere angesubutu kuiita siasa yake kwa jina halisia la "Ujima" nina uhakika ingeonekana ni siasa mbovu ila akaamua kuiita Ujamaa jina linaloonesha kama uhusiano mzuri hivi

Ila tafsiri ya Socialism ni Ujima na sio Ujamaa.
 
ujamaa kwa kipinde kile ilikuwa njia sahihi ya kuwaweka pamoja maana watu wengi walikuwa hawana elimu, wanaishi maisha duni sana, wanakaa mbali kutoka nyumba moja hadi nyiungine hata kupeleka huduma za kijamii ilikuwa shida sana, barabara mbovu kama tungeendelea na ubepari bas wananchi wangeendelea kuwa watumwa zaidi. ujamaa uliwaletea heshima zaidi baada ya kuanzisha vijiji vya ujamaa na kujenga umoja na kukuza lugha ya taifa na utaifa.

ujamaa ndio ulisaidia sana kujenga utaifa na kuachana na ubaguzi....ukabila uliondoka sabaabu ya ujamaa watu waliweza kujiona wao ni watanzania, utani wa jadi ukaanza.

nchi nyingi zilizoenda kwenye ubepari hasa Africa zina matatizo mengi ukichunguza.

mtoa maada nakushauri usome vizuri ama ongea na wazee walioishi kipindi hicho maana umesema ulizaliwa kipindi cha 90s. bado una mengi ya kujifunza kuhusu historia ya tanzania.

ni kweli walikjuwepo watu wengi walioshiriki kuleta Uhuru wa nchi japo hawakuwa na Elimu na hostoria imewaacha sana.

Ndio maana mkuu amesema watu wafundishwe historia ya nchi yao... hata ww umepata historia ya kambona kwa kuokoteza tu hujui mambo kwa undani wake. usingefanya hitimisho kwenye andiko lako ili watu wawe huru kujadili na ww kupata mwanga.

Kwa mantiki hiyo mkuu unataka kusema kuwa Serikali inayofuata Ubepari haujali raia wake? Kama ndio, vipi kuhusu Marekani ambao wanalinda raia wao hata kama ni mmoja yupo mahali akapata tatizo.

Watanzania kuwa wamoja haijaletwa na itikadi ya kisiasa, hii hali ya Umoja kuna watu wametoa damu zao kwa sisi kuwa wamoja sio siasa ya jukwaani au kitabuni inayoitwa Ujamaa.

Ujamaa una mazuri na mapungufu yake ila haimaanishi kuwa Ubepari usingefaa au kutufanya wamoja ndani ya hii nchi.

Kuchukua Kenya kama mfano wa madhara ya Ubepari ni kujielekeza vibaya kwanza turudi nyuma tuangalie historia ya Kenya ilivyo;

Kenya walikuwa na Ubaguzi hata kabla ya Uhuru, Mau Mau walikuwa wanapigania ardhi ya kabila lao wakikuyu baadae wakataka sasa uhuru wa Kenya waitawale

Tanzania ukiangali vita vyaMaji Maji vilipiganwa na makabila zaidi ya moja ya huko kusini ili kumtoa mkoloni hii inaonesha wazi watanganyika baadae watanzania walikuwa na umoja hata kabla ya uhuru.

Hii morali ya kuungana ili kupambana ingeweza kuendelezwa na System hata ndani ya Ubepari.
 
unaingizaje ubapari kwenye utawala wa machifu? machifu walikuwa watu wenye nguvu ujamaa uliweza kuvunja nguvu zao na kutufanya kuwa wamoja. ndani ya ubepari tusingekuwa wamoja kama hivi leo, utawala wa machifu ndio chimbuko la ukabila na ukanda kila mmoja ana linda mila na tamaduni zake, kwa kipindi kile ujamaa ulikuwa na faida,,, kila kitu huwa kuna sehemu ya kuanzia. inawezeka ilitakiwa tuanzie ujamaa then twende kwenye ubepari ambao tayari watu wana elimu, tungeingia kwenye ubepari na watu hawana elimu tungepata taifa la watu wajinga sana, ubepari haukusomeishei watoto wako kama huna hela unabakia kuwa mjinga. tukumbuke ubepari ni unyonyaji kwa lugha nyingine. ukilinganisha ubepari wa marekani na Tanzania haviendani hata historia ya watu wao ni tofauti sana.
huku sisi tulikuwa ni primitive kwa kipindi kile. taifa lolote linatakiwa kuanza na ujamaa kuwaleta watu karibu na serikali yao na kufundishwa mifumo ya nchi then baadae watachagua pa kwenda ila hoja yangu sitaki kulaumu kama tulikosea kuwa na ujamaa kipindi kile.
 
Hakuna shujaa mkuu wawili, wengine wapo kwa ajili ya kumjenga shujaa mkuu, mfano heshima annayopewa Mandela duniani ni sawa na anayopew Waltel Sisulu, wanaomjenga shujaa mkuu ndio uingia field direct,
 
Washindi huwa ndio wanaoandika Historia, na bahati mbaya sana mara nyingi huwa wanaindika jinsi wanavyojisikia.
 
Kupanga ni kuchagua! Wengi wa wale walioanza na ideology ya Ubepari wakati nchi zao bado ni changa wameishia kupata matabaka either ya kikanda au kikabila! Inawezekana ukaona kuwa tumechelewa sana lkn amini kuwa misingi aliyoijenga mwalimu ndio leo tupo wamoja hivi unavyoona hatuulizani makabila wala dini. Sasa kama kujenga nchi tuanzie hapo baada ya kujenga Amani na Umoja wa Kitaifa.
Nani aliesema hatuulizani makabila wala dini????

Hivi mtu mzima unapojitoa ufahamu unakuwa unafanya hivyo ili iweje???
 
Jamanieee mwisho wa siku Hata kiswahili chenyewe kulikuwa bado lugha ngeni, mpya na inayo evolve.

Probably hakukuwa na tafsida au misamiati mizuri kwa wakati huo. Na hayo yalikuwa maneno ya kawaida tu labda
Miaka ya 60 bado kiswahili ni lugha ngeni??

You can't be serious mkuu
 
Kutoka 1985 mpaka leo ni miaka 35 ambayo ingetosha kabisa “kurekebisha” chochote ambacho unaona mwalimu “alikosea”…..
Sio kwa misingi mibovu sanaaaaaa ambayo tayari ilishawekwa.

Miaka 35 ni kidogo mno kuondoa na kufutilia mbali (kisera) yale yote maovu ambayo yalishafanyika

Huoni Leo kila mtu ili apate political mileage lazima amtajetaje mwalimu??? Hizo ni miongoni mwa athari kuu ambazo it will still take years to eliminate
 
Wewe ni mpumbavu
 
Back
Top Bottom