Tanzania yafunguliwa Kesi ya Madai ya Tsh. Trilioni 3.2 kutoka kampuni ya Orca Energy kwa kukiuka Mkataba wa Uwekezaji

Wawekezaji wengine waanzishe migogoro ili waende mahakamani, kazi yetu iwe kuwalipa tu hao wawekezaji uchwara waliokaribishwa na ccm
Yule mweu mnayemuita dada wa Taifa kule Instagram kuna siku nilisoma post yake moja alikuwa anaelezea sasa hivi kuna uhuni mpya wa kupiga pesa kupitia fidia...

Yaani wale wamiliki wa kampuni ambao zilifungwa awamu iliyopita kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kufiriska au ukwepaji kodi, sasa hivi wamekuwa wakishirikiana na viongozi wa serikali wakiwemo wanasheria kufungua kesi za madai kwamba walionewa sana awamu iliyopita na hivyo wanataka fidia....!!

Kinachofanyika hao wawekezaji(walalamikaji) wanakuja na wanasheria wao ambao wanakaa na wanasheria wa serikali kwa siri na kusuka mpango mzima utakavyokuwa na kisha baadae ndio tunaskia habari kama hizi kwamba watu wanadai fidia za mabilion/trillions.

Na mastermind wa huo uhuni wote ni Abduli mtoto wa Samia.

Kwa hiki kinachoendelea naona kabisa hii serikali ni hatari sana kuliko hata kikindi cha waasi
 
Kwa kweli inasikitisha sana
 
January alijua kumchota akili Samia na machawa wake, alikuwa anaamua tu nini kifanyike na nani aondoke hili afanikishe dili zake za udalali.... samia amekuja kushtuka too late
 
Enzi za marehemu mikataba mingi iliathiriwa na sheria zilizokuwa zinashinikizwa na serikali na kupitishwa na bunge. Walionekana wapuuzi kina Lisu walio piga kelele kuhusu ubovu wa sheria hizo na athari yake kwa mikataba ya kimataifa. Lisu alionekana msaliti na asie litakia taifa mema. Mwana sheria wa serikali alikuwepo, waziri wa katiba na sheria alikuwepo, lakini hakuna la maana walilolifanya zaidi ya kila siku kufunga tai na kuingia kwenye V8.
 
Utawala wa nchi hii unatia hasira Sana,ila basi tu!
 
Umepaniki,
Lissu na Mwabukusi wamefikaje kwenye mikataba yenu mliyosaini CCM ?
 
Masheria ya hovyo tuliyojitungia kwenye mali zetu ndio yanayotuumiza wenyewe.

Huwezi kuweka sheria zakusema unavutia wawekezaji wakati hiyo rasilimali yako ni thamani kubwa.

Sijawahi kuelewa kwanini kwenye uwekezaji tusingetengeneza sheria za win win situation.

Mfano dhahabu muwekezaji alete pesa na technolojia yake tuchimbe kitakachopatikana tutoe mtaji wake,tutoe pesa yetu ya dhahabi faida tugawane.

Hadi leo sielewi mbona waarabu wanafaidika na mafuta yao,wengine na gesi yao.

Sidhani kama Marekani na nchi za ulaya nao wanasheria kama za nchi za kiAfrica katika suala lakuvutia wawekezaji.
 
Hili la sasa halihusiani na Sheria za zamani bali wao wenyewe kuharibu
 
Hayo mashwleria yemewekwa na worldbank na IMF Kwa ajili ya Africa kunufaisha ulaya.Sheria za uarabuni na mabara mengine nje ya America ya kusini ni winiwini na ndo maana wanatoka lakini nchi zote zenye Sheria kama Tanzania wote tuko mafukara angalia hata America ya kusini
 
Wanasaini mikataba bila kutushirikisha afu madeni ndio tunaambiwa
 
Kuna mtu kalaumiwa? Hivi unawezaje kusinya mkataba ukishindwa mamuz ya kesi yanaenda kufanyiwa mahakama za nje tena mwekezaji anapanga mahakama ya kuamua? Dipiqed
ndio mambo ya international Law hayo,japo kuwa Tanzania tulifanya marekebisho ya Sheria ya Usuluhishi(Arbitration Act 2020)inayoitaka place of Arbitration/Usuluhishi lazima iwe Tanzania katika migogoro yote inayohusiana na Uwezekaji katika Mafuta,madini n.k
japo kuwa marekebisho hayo yaliyofanyika yataweza kuathiri mikataba iliyokwisha kutekelezwa kabla ya Marekebisho ya Sheria husika(Arbitration Act 2020 na Natural Wealth and REsources (Permanent Sovereignity)Act 2017) .
 
Mgogoro husika hauna uhusiano na Contract law(General)bali linahitaji wabobevu(experts)wa International law katika Trade and Investment
 
Uko sahihi kabisa lakini ukipunguza jazba na personal attacks utakuwa Bora zaidi
 

Sasa wanajivuni Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imejipanga kukabiliana kimataifa
jopo la utetezi liliongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende
TOKA MAKTABA :

SERIKALI YASHINDA SHAURI LA USULUHISHI KATIKA BARAZA LA KIMATAIFA LA BIASHARA (ICC)​



Tarehe 06 Machi, 2024, Baraza la Kimataifa la Biashara (International Chamber of Commerce-ICC) limetoa uamuzi wake na kuipa Serikali ushindi katika Shauri la Usuluhishi Na. 2682/AZO baina ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency-PBPA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Kampuni ya Alchemist Energy Trading DMCC kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu.

Shauri hili lilifunguliwa baada ya Kampuni ya Alchemist Energy Trading DMCC kushindwa kusambaza mafuta kwa mujibu wa Mkataba ulitokana na Zabuni Na. PBPA/CPP/PMC/C3-KOJI/02/2021 wa tarehe 05 Januari 2021 kwa ajili ya kuleta nchini mafuta Metriki za Ujazo 36,192 ambayo yalipaswa kupokelewa kuanzia tarehe 27 Februari, 2021 hadi tarehe 01 Machi, 2021.

Kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jopo la utetezi liliongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende akishirikiana na Mawakili wengine kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).
Katika uamuzi wake, Baraza la ICC limetamka kuwa Kampuni ya Alchemist Energy Trading DMCC ilivunja Mkataba na hivyo kuwaamuru kurejesha fedha kwa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) dola za Marekani milioni tisa, laki saba na kumi elfu, mia sita hamsini na moja na senti arobaini na tano (USD 9,710,651.45) pamoja na riba kabla ya tuzo (pre-award interest) asilimia 7.67% kuanzia tarehe 18 Mei, 2021 hadi Novemba, 2023; kwa kuvunja Mkataba na kushindwa kuleta mafuta nchini.
Pamoja na Kampuni ya Alchemist Energy Trading DMCC kuamuriwa na Baraza hilo kurejesha fedha tajwa hapo juu kwa kuvunja Mkataba, pia Kampuni hiyo inatakiwa kutekeleza yafuatayo:-
  • (i)Kuilipa PBPA dola za Marekani milioni moja, laki moja arobaini elfu, na arobaini na nane (USD 1,140,048.00) ikiwa ni adhabu ya kuharibu mfumo wa ununuzi wa mafuta wa pamoja;
  • (ii) Kuilipa PBPA dola za Marekani laki nane themanini na mbili elfu (USD 882,000.00) ikiwa ni gharama za Baraza;
  • (iii)Kuilipa PBPA shilingi milioni mia nane kumi na nane elfu, laki mbili themanini na tano na mia saba (TZS 818,285,700.00) ikiwa ni gharama za kesi; na
  • (iv)Kulipa riba baada ya tuzo (post award interest) asilimia 7.67% kuanzia tarehe 06 Machi, 2024 hadi atakapokamilisha malipo yote anayodaiwa.
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inatoa shukrani za dhati kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, PBPA na wadau wote walioshiriki katika kuendesha shauri hili la kimataifa kwa kutumia Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali itaendelea kusimamia na kuendesha mashauri ya kimataifa kwa weledi na kulinda maslahi mapana ya Taifa letu.

Source : https://www.osg.go.tz/news/serikali...hi-katika-baraza-la-kimataifa-la-biashara-icc
 
TOKA MAKTABA:
29 February 2024

Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Tanzania, yaelezea mafanikio baada ya kujipanga :


View: https://m.youtube.com/watch?v=PR64ABKqV40Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende Akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliofanyika jijini Tanga.

Source : Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…