Tanzania yagoma kupiga kura ya kuunga mkono Mipaka ya nchi ya Ukraine(Territorial Integrity) huko UN

Kama urusi ni rafiki yetu kuliko mataifa ya magharibi mbona hatuoni . misaada kutoka urusi na hawatuuzi hata mafuta ya bei rahisi. Pumzika kwa amani mwalimu Nyerere, ulikuwa kiongozi mwenye misimamo sahihi.
 
Serikali iwe na msimamo wa wazi ,hata kama unakubaliana na Russia kwa baadhi ya masuala ila kupora ardhi ya sehemu sio sahihi..

Vinginevyo na sie tufanyiwe kura huru Ili Zanzibar wajitoe kwenye Muungano.
 
Kajifunze maswala ya diplomasia na sera za nje za nchi halafu soma historia ya sera ya nje ya Tanzania (foreign policy) halafu njoo urekebishe bandiko lako.
 
Kama irudi ni rafiki yetu kuliko mataifa ya magharibi mbona hatuoni . misaada kutoka irudi na hawatuuzi hata mafuta ya bei rahisi. Pumzika kwa amani mwalimu Nyerere, ulikuwa kiongozi mwenye misimamo sahihi.
Shida mmezoea vya kupewa bure na kuomba omba wakati huo mna resources tele kwa akili hizi tutaendelea kuwa masikini daima.

hakuna taifa ambalo lime endelea dunia hapa kwa kusaidiwa na taifa lingine pasi lenyewe kujiwekea uthabiti na weledi pamoja na nidhamu katika kufanya shughuli za kujiletea maendeleo lenyewe kwa kuweka sera imara zinazo lindwa na sheria na taratibu madhubuti kwa maslahi ya taifa.

kutegemea misaada ni ufinyu wa fikra na kamwe hatuta pata suluhu ya matatizo yetu hili hata Nyerere ,Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa walisha lisema muda mrefu sana.
 
Unafiki wa Serikali ya CCM umejengwa kwenye misingi ya kwamba wanaunga mkono kwa vitendo Sera za Udictator, Ufisadi, na ukandamizaji za huyo kichaa Putin.
 
Safi sana Tanzania🙏🙏🙏🙏🙏
 
Bora hatujapiga kura! washauri wamemshauri VIZURI Sana namba MOJA!!

Huo ni mtego wa kufunga upande mmoja wapo wa vita aidha Russia au Ukraine!

Wamejificha tu kwenye mipaka Lakini lengo ni KUJUA Nani yupo upande gani!!

Hivyo tu!
 
Sasa wewe uko mbagala mipaka ya ukraine unaijuaje embu acha utahira binti
 
Acha kushadadia

Mmewahi piga kura marekani inavoonea watu
 
Inashangaza sana nchi yetu ambayo imewahi kupigana vita kulinda Territorial Integrity ya nchi yetu leo inashindwa kusimama na kuiambia dunia kuwa mipaka ya nchi nyingine iheshimiwe.
Shame! shame!
1979 Idd Amin alidai Kagera ni sehemu ya nchi yake na vita ilikuwa kubwa. Leo hii nchi iliyipotia magumu yale inashindwa kulinda na kuteta haki ya nchi ingine.
 
Inashangaza sana nchi yetu ambayo imewahi kupigana vita kulinda Territorial Integrity ya nchi yetu leo inashindwa kusimama na kuiambia dunia kuwa mipaka ya nchi nyingine iheshimiwe.
Tanzania imefanya uamuzi sahihi kwa sababu, hilo azimio Hata kwa kupigiwa kura kwa asilimia 99.9999. Bado halitafanya kazi ya kutatua Mgogoro huo wa Ukraine! Kwa nini kujiingizia kwenye figisu zisizo na maana!!! Naunga Mkono uamuzi wa Tanzania.
 
Anaewapigisha kura ni US aliomtoa ghadafi, ,huko Iraq palestina anaua kila leo, huyo huyo aliomdhoofisha Mugabe na bado mko Kama mazuzu
 
Kuna nchi ziko upande wa kimalayamalaya heeee. (In kambarage voice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…