Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Ndo mlolongo wenyeweee?? Tobaaaaah
 
Unaamini Watanzania ni wajinga Sababu hawaendi Nje?
Unaamini wote waliopo nje wanauwezo wa kufikiri kuliko waliopo ndani?
 
Home seeking ndio ugonjwa mkubwa ambao huwakuta watu walio mbali na nyumbani.
Yaani unaanza maisha upya kwa kila kitu kisa utumwa wa pesa.
Kumbe kuna maiisha mazuri zaidi ya pesa.
Bahati mbaya sana waafrika wengi waendao ulaya hawana uwezo wa kurudi kusalimia ndugu.
 
Wakoloni weusi wanapenda tuendelee kubakia hapa tusipate akili ili waendelee kutuburuza.

Ila watoto wao wanawapeleka nje kusoma na wao wanakwenda kutibiwa na kufanya shoping.
Magufuli hakutaka uende nje na ulishangilia sana. Vipi unalizungumziaje hili? Au naye alikuwa mkoloni mweusi? Au double standards? Au au au...
 
Unaamini Watanzania ni wajinga Sababu hawaendi Nje?
Unaamini wote waliopo nje wanauwezo wa kufikiri kuliko waliopo ndani?
Watanzania si wajinga, lakini kusafiri kutachangamsha zaidi akili waliyojaliwa na Mungu.

Kumbuka, hata harakati za Waafrika kudai uhuru ziliongezeka zaidi baada ya vita vya dunia. Nini kilichangia kuwa hivyo? Ni Waafrika waliorejea kutoka vitani.

Kutembea na kujumuika na watu wa maeneo mengine huweza kubadilisha mitazamo ya watu katika mambo mbali mbali. Wewe unafikiri ni kwa nini Korea, nchi inayosadikika kuwa ndiyo inayoongoza sasa duniani kwa udikteta inajitahidi sana kuwafungia raia wake ndani ya Korea?

Hata miji yenye maendeleo sana, kumechagizwa na mwingiliano wa watu kutoka maeneo mbali mbali.
 
Ndo maana watu waliambiwa Kamala Harris anakuja kuwalazimisha waingiliane wanaume Kwa wanaume wakaandaa Hadi maandamano... little exposure ni ugonjwa mbaya Sana..
Hadi maandamano ya kupinga Dpworld kisa Wengi wanaamini waarabu wanakuja kueneza dini...
Ongeza na kuua Albino na wazee wenye macho mekundu
 
Ilipaswa kila anayezaliwa apewe passport bila maswali kama ya kipolice. Kupata passport Tanzania ni changamoto sana
Sana, hasa kama hupendi kutoa rushwa. Lakini kama ni mwepesi wa kunyoosha mkono, hata na fomu unaweza ukasaidiwa kujaza. Ukiritimba woote uliopo ni kwa ajili ya kufanikisha project takrima. Ni mradi wa watumishi wabinafsi.
 
Hapana mkuu! Ujinga haujawahi kuwa "bliss". Ujinga hukufanya wajanja wakufaidi huku wewe ukiumia bila kujua!

Fikiria Wamasai ambao Umasai hasa umewakaa ndani kuliko kitu kingine chochote! Wanajitahidi kuudumisha utamaduni wao mpaka wanageuja kivutio cha watalii kwa manufaa ya nchi na wengine, lakini si wao. Bila shaka umeshawaona wengi mijini, labda, wakiwa wapo kwenye malindo huku wamevaa nguo zao za asili.

Usifikiri wanafikiri wao ni wajinga, na usifikiri, kama wewe huufuati utamaduni wao watakuona ni "mjanja!" Usishangae, hata kama imewapa kazi ya ulinzi, wanaweza wakawa wanakuona wewe ni mjinga kwa vile huujui utamaduni wao.

Ujinga ni gharama sana mkuu. Ujinga na umaskini ni pete na chanda.

Tulipokuwa watoto, tulifarijiwa kuwa watoto wa matajiri ni wajinga! Lakini hebu wafananishe maisha ya watu waliokulia katika familia za kitajiri na kimaskini, japo si wote, but you can tell the difference.
 
Ukweli ni kuwa watz wengi hawaongei kiingereza fasaha sababu ya kusoma kwa Kiswahili. Nje kuna fursa nyingi tunazikosa na lugha inayotumika zaidi duniani ni English. Watawala wengi Wana roho mbaya hawataki watz kwenda kunufaika nje! Nchi inakosa remittance na kubaki maskini.
Solution ni kubadili lugha ya kufundishia kutoka Kiswahili kuwa English.
Watz wanapenda kwenda nje hasa vijana wasio na ajira ila Njia zote zimefungwa!
 
Juzi nimeenda Makao Makuu Kurasini ni patupu waombaji hata 10 hawafiki tofauti na zamani watu walikuwa wanajazana.
 
Juzi nimeenda Makao Makuu Kurasini ni patupu waombaji hata 10 hawafiki tofauti na zamani watu walikuwa wanajazana.
Inamaanisha nini?
1. Huduma zimerahishwa sana siku hizi hivyo kila anayefika huhudumiwa haraka sana?

2. Wengi wamekata tamaa kufuatilia?

3. Kila kitu kinafanyikia mtandaoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…